UKOSEFU WA MIUNDO MBINU IMARA KWA AJILI YA WALEMAVU NDANI YA MAKANISA NA MISIKITI CHANZO CHA
WALEMAVU KUSHINDWA KUHUDHURIA NYUMBA ZA IBADA
Na Queen Lema,Aruha
IMEELEZWA kuwa kutokana na baadhi ya taasisi mbalimbali za
dini hapa nchini kushindwa kujenga majengo ambayo yanakidhi haja za walemavu
kumesababisha walemavu wa viungo kusindwa kupata haki zao za msingi za kuabudu
huku hali hiyo ikisababisha madhara kwa jamii
Changamoto hiyo imetolewa mjini hapa katika kanisa la St
James na walemavu wa viungo mbalimbali ambao walihudhuria ibada maalumu kwa
ajili yao iliyofanyika kanisani hapo mapema jana
Walemavu hao wa Viungo walisema kuwa inasikitisha kuona kuwa
asilima kubwa ya makanisa pamoja na misikiti ikiwa imejengwa bila kukumbuka
aina ya ulemavu wao huku wakiwa wanasisitzwa kwenda kuabudu ingawaje hakun
mazingira rafiki ambayo yanaweza kuwafariji
Walisema kuwa majengo mengi ya ibada ni magorofa na baadhi
ya walemavu hawana viungo kama vile miguu ambapo hali hiyo inawafanya washindwe
kupanda kwenye ngazi kutoana na aina ya ulemavu wao jambo ambalo linawafanya
wakose haki zao za msingi ya kuabudu
‘tunapenda sana kuja makanisani na hata misikitini lakini
tnapofikiria miundo mbinu ambayo siyo rafiki kwetu kweli tunakata tamaa
ingawaje sehemu mojawapo ya kutufariji ingekuwa ni kwenye nyumba hizo za ibada
sasa tunawaomba wakuu wote wa taasisi hizi wawe na tabia ya kutufikiria kwa
kuhakikisha kuwa na sisi tunapewa nafasi ya kuabudu kama ilivyo sheria ndani ya Katiba ya Nchi’waliongeza
walemavu hao wa viungo.
Awali Mchungaji Kiongozi
wa kanisa hilo bw Andrew Kajembe alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana
wa kuhakikisha kuwa kila Taasisi ya dini inawakumbuka walemavu ingawaje kwa sasa asilima kubwa ya taasisi za dini
zimewasahau walemavu kwa hofu mbalimbali hali ambayo inawafanya waone kama
wametengwa na jamii zao huku matendo ya unyanyasaji dhidi yao nayo yakiwa
yanaongezeka siku hadi siku
Bw Kajembe alisema kuwa hata miundombinu ya baadhi ya
makanisa bado si rafiki sana kwa walemavu hivyo basi wakuu wa makanisa
wanatakiwa kuhkikish wakati wanafikiria kujenga pia waweze kuwafikiria
walemavu ambao wamesahulika ingawaje
ndani ya makanisa na taasisi za dini ndipo wanapoweza kupata faraja ya maisha
ikiwemo dhana ya uwajibikaji kwa shuguli za kijamii zaidi.
“Sisi kama wakuu wa makanisa na misikiti bila kujali itikadi
zetu tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunawasaidia hawa walemavu kwa kuimarisha
majengo yetu na yawe rafiki kwa maisha yao na pia hata ndani ya ibada zetu
tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunawatengea hawa walemavu siku maalumu kwaajili
yao na sadaka zote ziweze kuelekezwa kwao kwani
kwa kufanya hivyo bila kujali dini zao itasadia sana kuongeza ufanisi
kwao na hata maisha yao kuweza kuboreka zaidi”aliongeza bw kajembe
Wakati huo huo alisema kuwa siku hiyo ya walemavu pia ilenda
sambamba na siku ya kuwafariji wagonjwa ambapo waumini wa kanisa hilo walitembelea
na kuwafariji wagonjwa na majeruhi wa hospitali ya Mt Meru pamoja na watoto
waliozaliwa katika hospitali ya Levolosi.
No comments:
Post a Comment