HAKIKISHENI KUWA HAMUINGILII HAMUHARIBU KAZI ZA WAFADHILI-
OLE MEDEYE
Na Queen Lema,Arusha
Naibu waziri wa nyumba,ardhi na makazi ambaye pia ni mbunge
wa jimbo la Arumeru Magharibi,Goodlucky Ole Medeye amezitaka Serikali za Mitaa
ukiwemo Uongozi wa Vijiji Mbalimbali ndani ya jimbo hilo kuhakikisha kuwa kamwe hawaangilii
shuguli au miradi mbalimbali ya Wafadhili ambayo ina malengo ya kuwasaidia
wananchi
Medeye aliyasema hayo Jimboni humo wakati akizundua
zahanati ya Ester iliopo katika Kijiji
cha Ngaramtoni ambayo ilijengwa kwa nguvu za wafadhili kutoka nchini Uingereza kwa
malengo ya kudumisha sekta ya afya hasa afya ya mama na mtoto
Medeye alisema kuwa kuwa endapo kama
Vijiji vitakuwa vinaingilia masuala ya Miradi ambayo imetolewa na wafadhili kwa
malengo mbalimbali ni wazi kuwa malengo hayo yatakwama na badala yake umaskini
ndio utakaokirhiri huku jamii ikibaki na mateso mengi
Aliongeza kuwa kazi ya Serikali ya Kijiji ni kuhakikisha
kuwa miradi hiyo inafanya kazi kwenye viwango vya hali ya juu kama yalivyokuwa
malengo ya wafadhili hivyo kama Serikali
za kijiji zitafanya hivyo basi zitachangia sana mabadiliko tena ya hali ya juu huku
mabadiliko hayo yakichangia kupungua kwa umaskini
Awali wanawake ambao ndio walengwa wakubwa sana wa mradi huo walisema kuwa zahanati hiyo
itaweza kuwasaidia kwa kuokoa afya zao kwani walikuwa wanalazimika kutembea
Umbali wa zaidi ya Kilomita Kumi kwa ajili ya kutafuta huduma za afya hali
ambayo wakati mwingine husababisha vifo
“kabla hii zahanati ya ester haijaja tulikuwa tunatoka hapa
mpaka Selian au mara nyingine tunaenda mpaka Mjini au Kaloleni sasa wakati huo
kama unaumwa sana
unaweza kupoteza maisha kutokana na umbali ila kwa sasa tuna uhakika wa kupata
huduma bora tena za afya ya mama na mtoto’waliongeza wanawake hao
Mwisho
No comments:
Post a Comment