Sunday, September 22, 2013

WAZIRI KABAKA AZINDUA RASMI MCHAKATO WA MAANDALIZI YA USHIRIKI WA WAJHASIRIA MALI .....

WAZIRI KABAKA AZINDUA RASMI MCHAKATO WA MAANDALIZI YA USHIRIKI WA WAJHASIRIA MALI .......





Waziri wa Kazi na Ajira  Mhe. Gaudentia  Kabaka  leo  tarehe  19/09/2013, amezindua  rasmi  mchakato wa  maandalizi ya ushiriki wa Wajasiria mali wa Tanzania  katika Maonesho ya 14 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo  kama  Nguvu kazi/Jua kali.

Maonesho hayo yaliyoanza kufanyika  mwaka  1999 jijini Arusha  Tanzania wakati wa kusainiwa mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yameendelea kufanyika kila mwaka kwa mzunguko katika nchi ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Dhumuni kuu la maonesho haya ni kuwezesha sekta  isiyo rasmi kukua na kurasimisha shughuli zao katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwapatia fursa Wajasiriamali wa sekta hii kuonesha bidhaa zao, kukutana na wenzao, kubadilishana taarifa, ujuzi, kukuza masoko ya bidhaa na huduma pamoja na kuwezesha kupanuka kibiashara.

Jumla ya Wajasiriamali 1,070 kutoka nchi tano za  Jumuiya ya Afrika Mashariki wanategemewa kushiriki na Tanzania inatarajiwa kupeleka washiriki 250.

Mhe. Waziri Kabaka amesema,ili kurahisisha na kuharakisha ushiriki wa Wajasiriamali wa Tanzania katika maonesho hayo, kuna swala la usajili, na fomu za usajili pamoja na vigezo vya kuangalia kabla ya kujaza fomu ambavyo vinapatikana kwenye  Tovuti ya Wizara ambayo  ni www.kazi.go.tz
IMETOLEWA
Ridhiwan.M.Wema
Msemaji

No comments:

Post a Comment