Sunday, September 22, 2013

CHAMA CHA WAFANYAKAZI MASHAMBANI NA KILIMO TANZANIA CHAANZISHA KAMPENI YA KUONDOA BUGHUDHA SEHEMU ZA KAZI

CHAMA CHA WAFANYAKAZI MASHAMBANI NA KILIMO TANZANIA CHAANZISHA KAMPENI
YA KUONDOA BUGHUDHA SEHEMU ZA KAZI



Na Queen Lema, Arusha



Chama cha wafanyakazi mashambani na kilimo Tanzania(TPAWU)kimezindua
kampeni ya kuweka mazingira huru yasiyo nnughudha za kijinsia mahala
pa kazi huku lengo likiwa mi kutokomeza kabisa unyanyasaji



Akizundua Kampeni hiyo mapema jana naibu Katibu mkuu wa chama hicho
hapa nchini Bw John vahaya alisema kuwa kampeni hiyo italenga
wafanyakazi wa maeneo mbalimbali hapa nchini



Bw Vahaya alisema kuwa lengo halisi la kampeni hiyo ni kuhakikisha
kuwa inatokomeza kabisa masuala ya unyanyasaji hasa mahala pa kazi
kwani unyanyasaji wakati mwingine umesababisha madhara mengi sana hasa
kwa wafanyakazi wa kike



“chama hiki kinatamani kuona kuwa suala la unyanyasaji hasa ule wa
kijinsia linakuwa ni ndoto kabisa kwani pia tulikuwa na tafiti
mbalimbali ambazo zinaonesha mazingira mabaya sana kwa wanawake ambapo
mpaka sasa suluhu ya mambo haya kupitia kampeni hii
yatagundulika”aliongeza bw Vahaya



Vile vile alisema kuwa utafiti ambao umezaa kampeni hiyo uliweza
kufanywa kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa,Kilimanjaro na Arusha ambapo
umeweza kubaini mambo mbalimbali ambayo wakati mwingine ndio chanzo
kikubwa cha umaskini hasa kwa maisha ya wanawake



Akiongelea matokeo ya tafiti hiyo alisema kuwa ni pamoja na wanawake
wengi kushindwa kusema hadharani jinsi ambavyo wanafanyiwa na wanaume
hasa wale wenye madaraka huku hali hiyo ikichangia kuongezeka kwa
akina mama wa majumbani



Pia alidai kuwa tafiti hiyo imeweza kugundua kuwa bado wafanyakazi wa
mashambani na viwandani bado nao wanakabiliwa na changamoto ya ngono
mahala pa kazi huku hali hiyo pia ikipunguza kasi ya utendaji kazi
hasa kwa jinsia ya kike



Kutokana na hali hiyo alitoa wito kwa wamiliki wa viwandani lakini pia
wale wa mashamba ya maua kuhakikisha kuwa wanapinga vikali tabia hiyo
lakini wanawachukulia hatua kali wakuu wa idara ambao wataonekana
kujihusisha na unyanyasaji mahala pa kazi kwa visingizio vya Jinsia ya
kike au ya Kiume.



MWISHO

No comments:

Post a Comment