Saturday, September 28, 2013

WATANZANIA WATAKIWA KUACHANA NA DHANA YA KULALAMIKA OVYO JUU YA CHANGAMOTO ZAO BADALA YAKE WATUMIE FURSA WALIZONAZO KUTATUA CHANGAMOTO HIZO




IMEELEZWA kuwa dhana ya ulalamishi juu ya changamoto mbalimbali kwa
watanzania imesababisha watanzania wenyewe kushindwa kuwajibika huku
wengine wakiendelea kukosa mahitaji yao ya msingi na kisha kusingizia
Serikali.

Kwa sasa asilimia kubwa ya watanzania wamebaki wakiwa wanalalamikia
baadhi ya viongozi kwa kushindwa kutimiza na kutatua changamoto zao
bila kujua na kutambua kuwa kila mtanzania anapaswa kutatua kero
mbalimbali

Hayo yameelezwa na Waziri wa  waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu
uwekezaji na uwezeshaji Dkt Mary Nagu wakati mapema wiki hii wakati
akiongea na wanafunzi wa shule ya Haradali katika maafali ya tatu ya
shule hiyo

Dkt Nagu alisema kuwa dhana hiyo ya kulalamikia siyo dhana nzuri kwani
haijengi Nchi badala yake inabomoa kwa kuwa kila mtanzania ana uwezo
mkubwa sana wa kuweza kusaidia maendeleo ya Nchi ya Tanzania

Alifafanua kuwa umefika wakati wa watanzania kubadilika na kujiuliza
maswali kabla ya kuanza lawama na mara baada ya kujiuliza maswali pia
wanatakiwa kubuni aina na mbinu mbadala ambazo zinaweza kuiokoa nchi.

“ni kweli tunao viongozi wa aina mbalimbali lakini hawawezi kusikiliza
kero,shida, na changamotoo za kila mmoja wetu hivyo basi kama kila
mtanzania atawajibika kutatua kero leo nchi ya Tanzania itaweza
kusonga mbele zaidi na malalamishi yataisha”aliongeza Dkt Nagu

Pia alisema hata viongozi wa Serikali nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa
wanawajibika tena kwa kiwango ambacho kinahitajika kwani kama wao
watawajibika vizuri basi watachangia kuharakisha maendeleo ya Nchi
ambayo bado yapo chini sana.

“ukiwa kama kiongozi wa Serikali katika Ngazi yoyote ile unapswa
kuhaakikisha kuwa unawajibika kwa kiwango cha asilimia 100 usilale na
usichague kazi ya kufanya wewe fanya zote ili uweze kuppunguza dhana
hii ya kulalamika ambayo wakati mwingine ndio chanzo cha umaskini
katika maisha yawatanzania wengi”alifafanua zaidi Dkt Nagu

Wakati huo huo mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo ya Haradani,Bw Simon
Kaaya alisema kuwa ili kukuza na kuwekeza kwenye sekta hiyo ya elimu
hapa nchini Changamoto mbalimbali zinatakiwa kutatuliwa kwa haraka
sana kwani bado kuna umuhimu mkubwa wa elimu.

Bw Kaaya alisema kuwa mbali na hayo hata wamiliki wa shule mbalimbali
wanatakiwa kuangalia zaidi suala la mahitaji kuliko suala la maslahi
ambalo wakati mwingine linasababisha baadhi ya watoto kukosa elimu
kabisa.

“nikisema hivyo nina maana kuwa kwa mfano kabla haujaanzisha shule ni
lazima uangalie mahitaji ya eneo lile lakini pia uhakikishe kuwa hata
ada ambayo unaitoza nayo inaendana na uwezo wa wazazi wa maeneo yale
kwani kama utaweka kiwango kikubwa na eneo lile lisipate watoto
utakuwa umefanya kazi ya bure kabisa’aliongeza Bw Kaaya

No comments:

Post a Comment