Saturday, September 28, 2013

ASILIMIA 30 YA WATANZANIA WAISHIO VIJIJINI KUPATA UMEME IFIKAPO MWAKA 2015





SERIKALI imesema kuwa mpaka ifikapo mwaka 2015 asilimia 30 ya
watanzania  waishio vijijini watakuwa wamepata huduma ya umeme kwani
kwa sasa asilimia saba tu ya wananchi waishio vijijini ndio wanapata
huduma hiyo ya umeme.

Kauli hiyo imetolewa jana (leo) jijini hapa na Naibu waziri wa Nishati
na madini hapa nchini Steven Massele wakati akiongea na wadau wa
mashirika yazilishayo umeme katika nchi za kusini mwa jangwa la
sahara(PIESA).

Masele alisema kuwa asilimia 21 ya watanzania ndio wanapata huduma ya
umeme ambapo kati yao asilimia saba ndio wanaishi vijiijini lakini
kupitia mpango wa wakala wa umeme Vijijini (REA)watahakikisha wilaya
zote na vijiji vyote vinapata umeme kwani ni haki yao ya msingi.

“tunataka kuona kuwa kila familia hata kama ni ya kijijini inapata
umeme na pia kama watapata umeme ni wazi kuwa hata maendeleo yatakuja
kwa haraka tofauti na pale ambapo hakuna umeme wala huduma
hizo”alisema Masele

Katika hatua nyimgine aliwataka wakala wa umeme vijijini kuhakikisha
kuwa wafanya kazi kwa haraka sana ikiwa ni pamoja na kutatua
changamoto ambazo zipo kijijini kwani asilimia kubwa ya wananchi wa
vijijini bado hawajaweza kupata huduma hiyo ya umeme lakini pia
hawajatambua umuhimu wake.

Awali mwenyekiti wa PIESA ambaye pia ni Kaimu mkurugenzi wa shirika la
Tanesco hapa nchini Mhandisi Felchesmi Mramba alidai kuwa lengo halisi
la kukutana maeneo hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanajadili namna
ya kutumia matumizi ya Teknolojia katika kupata umeme

Mhandisi Mramba alidai kuwa kama watafanya hivyo basi wataweza
kuruhusu kwa kiwango kikubwa sana upatikanaji wa umeme hasa maeneo ya
Vijijini lakini pia kuangalia namna ya matokeo ya tafiti ambazo
walizifanya na nchi zilizoendelea Duniani.

Ametaja nchi ambazo zitajadili namna ya upatikanaji wa umeme hasa
vijiijini kuwa ni pamoja na Marekani, Mexico,Ausralia, India, Canada,
China, Indonesia,Japani,Kenya ,Malawi Uganda, Botswana , Lesotho
pamoja na Afrika ya kusini.

MWISHO

No comments:

Post a Comment