Monday, May 6, 2013

TANROAD ARUSHA YALAZIMIKA KUTUMIA MILION 700 KUKARABATI BARABARA ZILIZOHARIBIKA VIBAYA NA MVUA

Na gladness ,Arusha

TANROAD ARUSHA YALAZIMIKA KUTUMIA MILION 700 KUKARABATI BARABARA ZILIZOHARIBIKA VIBAYA NA MVUA

WAKALA  wa barabara mkoa wa Arusha (TANROAD)umelazimika kutumia kiasi cha zaidi ya Milion 700 kutokana na baadhi ya barabara kuharibiwa vibaya na mvua ambazo zinazoendelea kunyesha Jijini hapa

Akiongea na “Malkia wa matukio”mapema jana meneja wa Tanroad mkoa wa Arusha,Bw Deusdedit Kakoko alisema akuwa wamelazimika kutumia fedha hizo kwa ajili ya kukarabati baadhi ya barabara

Kakoko alisema kuwa kwa kipindi hiki baadhi ya barabara zimeharibika vibaya sana huku hali hiyo ikisababisha baadhi ya watumiaji wa barabara kushindwa kutumia kwa ajili ya shuguli za kila siku.
“hizi milioni 700 zimelazimika kutumika ili kuweza kurekebisha miundo mbinu tena kwa haraka sana na kama tusingefanya hivyo ni wazi kuwa wananchi wanaotumia barabara hizi wasingeweza kupata msaadawa haraka ingawaje bajeti yetu haikuwa hivyo”alisema Kakoko

Alitaja Barabara ambayo zimeharibika vibaya kutokana na mafuriko  pamoja na mvua ambazo zinaendelea kunyesha Jijini hapa ni pamoja na barabara ya Monduli Lokisare,barabara ya pili ikiwa ni Makuyuni Ngorongoro,Barabara ya Tatu ni Karatu Kilimapunda.

Mbali na hayo Kakoko alisema kuwa pamoja na kuwa wamelazimika kutumia kiasi hicho cha fedha lakini pia kuna umuhimu mkubwa sana wa Halmashauri za Mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanatenga maeneo ya maegesho ya magari

Alisema kuwa kwa sasa TANROAD inapata wakati mgumu sana kwa kuwa baadhi ya maeneo ya miji hakuna maegesho hali ambayo wakati mwingine inasababisha  magari makubwa ya mizigo kuegeshwa katikatati ya Mji hali ambayo wakati miwingine inasababisha vurugu kubwa sana


Amezitaka Halmashauri kuacha kuona suala la kutenga maegesho kama ni suala la utani badala yake wahakikishe kuwa hata kama hawana maegesho ya magari wanayatenga kwa haraka sana kwa kuwasasa wapo baadhi ya madereva wanaofanya makosa kwa visingizo kuwa hakuna maegesho ya magari

“ni vema kama halmashauri zikahakikisha kuwa kila halmashauri inakuwa na maegesho lakini kama maeneo ya maegesho yatakwepwa ni wazi kuwa malengo ya Tanroad hayatafikiwa na badala yake yatasababisha vurugu ingawaje Arusha ni Mji wa Kimataifa”alisema Kakoko.

No comments:

Post a Comment