Monday, May 6, 2013

Bilion 9.8 zatengwa kwa ajili mikopo kwa wachimbaji wadogo

Na Wankyo Gati,arusha

Serikali imetenga  sh.bilioni 9.8 kwa ajili ya mikopo ya vifaa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima ili kuboresha uchimbaji wao na watakopeshwa kupitia vikundi watakavyojiunga na itakuwa mkopo endelevu ili kuinua sekta hiyo ya madini kupitia wachimbaji hao.
Hayo yalisemwa leo na Kamishna wa madini wa kanda ya kaskazini Eng.Benjamini Mchwampaka  wakati wa mahojiano na waaandishi wa habari yaliyofanyika katika ofisi za kanda hiyo zilizoko mkoani arusha.

Alisema kuwa kupitia mikopo hiyo itatoa fursa mbalimbali kwa wachimbaji hao kupata vifaaa hivyo ili kuweza kuinua uchimbaji wao na kuwa wa kisasa zaidi ili kuongeza uzalishaji wa madini nchini ambapo hivi sasa wamekuwa wakikwamishwa na ukosefu wa vifaa vya kisasa hali ambayo wanachimba ila hawapati madini ya kutosha.

Ameongeza kuwa wachimbaji wadogo wa kanda ya kaskazini  bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali  katika uzalishaji madini ikiwemo  kutokuwa na vifaa vya uchimbnaji vya kisasa ,bei kubwa ya milipuko na elimu ndogo ya uchimbaji madini hayo  hali ambayo inakwamisha jitihada zao za kuchimba madini hayo na kuwarudisha nyuma katika kujikwamua kiuchumi
.
Alisema kuwa hivi sasa wachimbaji wadogo walio wengi wanachimba kwa mazoea na vifaa duni ambapo elimu ya utambuzi madini  sehemu yalipo ni ndogo hali ambayo inasababisha kutopata madini yakutosha na kutumia gharama kubwa zaidi.

Eng.Mchwampaka alisema kuwa katika kanda hii wachimbaji wamekuwa wakichimba kiholela bila lessen hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao na hata kusababisha kifo na madhara mbalimbali ambapo  maeneo hayo yanachimbwa kwa kesi sana  hali ambayo ni hatari kwa  badala yake wachimbaji wafate taratibu za kuchimba eneo tengefu kwa madini kwa maendeleo yao na usalama wa maisha yao kuepuka kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Aidha aliongeza kuwa hivi sasa ofisi ya kanda imejiwekea mkakati mbalimbali ikiwemo kusogeza huduma karibu na wachimbaji katika kanda hii hususan kutoa elimu ,ya uchimbaji wa madini kitaalamu zaidi,hali ya masoko ,afya migodini  ,ajira na kutoa mafunzo kwa vitendo ya namna ya ulipuaji  mogodini sambamba na watatoa fursa ya namna ya uchimbaji salama na wenye tija na maendeleo kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.

Eng.Mchwampakka alisema kuwa hivi sasa wako kwenye mchakato wa kuandaa maonyesho ya vito ,na madini mbalimbali  yatakayofanyika oktoba 28 hadi 30 mwaka huu mkoani hapa  ambapo watahiusisha wafanyabiashara wote ncnini na nchi jiran ikiwemo Kenya ,DRC kongo ,Zambia ,Madagascar ,Malawi ,Ethiopia ,Afrika ya kusini na Msumbiji ili kuweza kubadilishana uzoefu na kuweza kuongeza ushindani katika sekta ya madini nchini.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment