Monday, May 6, 2013

TAASISI BINAFSI INAYOENDESHA MAFUNZO YABUNI UZIO WA KIENYEJI WA KUZUIA TEMBO KUINGIA MASHAMBANI UTAKAOGHARIMU MILIONI 400

TAASISI BINAFSI INAYOENDESHA MAFUNZO YABUNI UZIO WA KIENYEJI
WA KUZUIA TEMBO KUINGIA MASHAMBANI UTAKAOGHARIMU MILIONI 400

,Arusha

TAASISI binafsi inayoendesha mafunzo kwa kushirikiana na vyuo vya nje
(University Times Training Insititute )iliyopo mjini hapa imebuni mradi wa
kutengeneza uzio  wa kiasili  utakaogharimu  kiasi cha shilingi milioni mia
nne wa kuzuia tembo kutoharibu mazao ya binadamu mashambani.

Akizungumza na” MALKIA WA MATUKIO “  mkurugenzi wa taasisi hiyo bw Solomon Njiamoja
alisema kuwa mkakati huo  wa kuweka uzio huo utaanza kutekelezeka julai
mwaka huu katika maeneo ya vijiji  vya Serengeti.

Alisema kuwa chuo hicho kimeweza kubuni njia hiyo ya uzio wa kiasili ambayo
itakuwa tofauti na fensi ya umeme ambayo haitaweza kuathiri tembo
wanaozunguka hayo maeneo husika.


Aliongeza kuwa mara nyingi tembo wanapovamia mashamba ya watu ni bunduki
zinatumika kuwaua au kuwafukuza hali ambayo inafanya kupungua kwa idadi ya
tembo hao ambapo kupitia mradi huo utapunguza kwa kiwango kikubwa kwani
tembo hawataweza tena kupita mashambani na kuleta madhara kwa jamii.

 Alitaja faida zitakazotokana na uzio huo wa kienyeji kuwa ni pamoja na
kuokoa chakula ambacho kinaharibiwa na tembo pindi wanapoingia
mashambani,kuokoa maisha ya wakazi walioko maeneo hayo ,kuepusha migogoro
kati ya jamii na tembo pamoja na kuokoa fedha ambazo serikali ingetoa kama
fidia kwa wale walioathiriwa na tembo.

Aidha vijiji vitakavyonufaika na mradi huo ni pamoja na Nata,Mtakuja
,Biafra,Ruhamchanga na Bihonchugu  ambapo uzinduzi wa uzio huo utatangazwa
rasmi katika kongamano litalofanyika mapema nchini Marekani

No comments:

Post a Comment