Monday, May 6, 2013

SIMANJIRO YATAKIWA KUTUNGA SHERIA AMBAZO ZITAWALZIMISHA MIFUGO KUOGESHWA

SIMANJIRO YATAKIWA KUTUNGA SHERIA AMBAZO ZITAWALZIMISHA MIFUGO KUOGESHWA

Na Queen Lema,Simanjiro

Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,imetakiwa kutunga
sheria ndogo zitakazowalazimisha wafugaji kuogesha mifugo yao kwenye
majosho ili kuiepusha na vifo vinavyotokana na magonjwa ya kupe.

Hayo yalielezwa juzi na Mkurugenzi wa shirika la Cedesota,Jackson Muro
kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo,kusimamia mipango na ufufuaji wa
majosho,madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

Muro alisema endapo sheria hiyo ndogo ikipitishwa na halmashauri ya
wilaya hiyo,wafugaji watayatumia majosho hayo ambayo yapo kwenye
maeneo mengi lakini hayatumiki kwa kuoshea mifugo.



Alisema kwenye wilaya ya Simanjiro kuna majosho mengi ya kuoshea
mifugo lakini wafugaji hawayatumii ipasavyo,hivyo wanapaswa
kuwashinikiza ili wayatumie majosho yao kwa kuoshea mifugo yao.



“Bila hivyo itakuwa kazi kubwa kwani wafugaji wengine watakuwa
wanaogesha mifugo yao na inapokuwa kwenye malisho inachanganyana na
isiyoogeshwa hivyo kuambukizana na watakuwa wanawapa hasara wenzao,”
alisema Muro.



Hata hivyo,Diwani wa kata ya Shambarai Alais Edward alisema tayari
Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo wameshapitisha azimio
la kupitisha sheria ndogo ya kuwataka wafugaji waogeshe mifugo yao.



“Tumeshapitisha azimio hilo na kutoa maagizo kwa maofisa watendaji
wote wa vijiji kuhakikisha mchakato wa kupitishwa sheria hizo ndogo
kwenye mikutano ya vijiji ili wafugaji wetu watumie majosho yaliyopo,”
alisema Edward.

No comments:

Post a Comment