Thursday, April 26, 2012

SAKATA la wachungaji wa kanisa la sabato na uongozi wa kanisa hilo umechukua sura mpya mara baada ya wachungaji watatu ambao walikuwa wanashitakiwa kwa makosa ya kudaiwa kurudufu vitabu,kusema kuwa wanatoa muda kwa kanisa hilo kuomba radhi hata kwenye vyomboi vya habari na endapo kama watashindwa kufanya hivyo basi watawapeleka mahakamani.

Akiongea na mjini upako wa habari za ufalme wa mungu  kwa niaba ya wachungaji wengine wawili Dkt Tulla Paul alisema kuwa wameamua kufikia uamuzi huo kwa kuwa Kanisa hilo limepotosha umma na pia wameshindwa kufika hata kituo cha polisi ambapo ndipo waliposhitaki

Dkt Tulla alisema kuwa kwa mara ya tatu tena mfululizo Walalkamikaji ambao ni kanisa hilo wameshindwa kufika katika kituo cha kati cha polisi mjini hapa hali ambayo inafanya hata kesi hiyo ishindwe kupelekwa mahakamani

Alifafanua kuwa kanisa hilo la Sabato ambalo lilisema kuwa lina ushahidi dhidi ya wachungaji hao kurudufu vitabu vya nabii Hellen .G. White ni uongo kwa kuwa kanisa ndilo lilorudufu vitabu

“kanisa la Sabato ndilo lilorudufu vitabu na ushaidi upo kwa maana hiyo basi ni vyema tukaenda mahakamani tukapambane huko huko ila kama hawataki waombe radhi hadharani kwa kuwa wametuweka katika wakati mgumu sana na ni sawa na kifungo cha Nje kwa kuwa mara nyingi sana tunahudhuria kituoni ili kesi iende mahakamani lakini wao hawaji “aliongeza Dkt Tulla

Katika hatua nyingine alisema kuwa tukio hilo ni sawa na uonevu mkubwa sana na hata taasisi nyingine za dini nazo zinatakiwa kujifunza kitu kwa kuwa wamepoteza muda na rasilimali fedha kwa ajili ya madai ambayo si ya msingi

Walifafanua kuwa kwa muda wa zaidi ya Miezi mitatu sasa wamefuatilia kesi hiyo ambayo ni AR/IR/1130/2012 huku shuguli zao za kueneza injili nayo ikikwama hali ambayo ni kichocheo kikubwa sana cha kukata tama

“sasa kama sisi wengine tunatoka Mwanza tunakuja kwa ajili ya kesi ambayo tulifunguliwa sisi kwa kisa kuwa tumerudufu vitabu wakati ni uongo na walalamikaji hawaji ili kesi iende mahakamani basi huu si ni uongo wa ajabu sana jamani nini nafasi ya kanisa hapa na je mtu ambaye haamini anajifunza nini kutoka kwa hawa viongozi wa kanisa ‘alisema Dkt Tulla

 

chanzo cha habari na queen Lema

0758907891

 Arusha

No comments:

Post a Comment