Na Joseph Ngilisho,MERU
ASKOFU mkuu wa kanisa la
International Evangelism Center lililopo kijiji cha Sakila wilayani
Arumeru mkoani hapa,Elihud Issangya ameitaka jamii kuacha tabia ya kuzaliana hovyo kama
kuku,badala yake ifuate mpango wa uzazi wa majira,ili kuipunguzia mzigo serikali
kukabii changamoto ya ajira na baa la njaa linalolinyemelea Taifa.
Isangya ametoa kauli hiyo leo katika mahafali ya 60 ya
wahitimu wa masomo ya thiolojia ngazi ya diploma, katika chuo cha bibilia
kilichopo Sakila ,ambapo jumla ya wahitimu 87 kutoka nchi mbalimbali za Afrika
walihitimu masomo ya miezi 6 na kutunukiwa vyeti.
Askofu huyo alikemea tabia iliyozoeleka kwa jamii kuzaa bila mpango, huku
akitofautiana na
maandiko matakatifu yaliyopo kwenye
bibilia yanayosema enendeni mkazaliane muijaze dunia,na kusema kuwa kadili hali
inavyokuwa maandiko hayo yanapitwa na wakati, kwani idadi kubwa ya watu
imeongeza umasikini wa familia na taifa kwa ujumla ukiwemo uharibifu wa
mazingira unaosababsihwa na watu.
‘’watu wanashindwa kufahamu maana halisi ya maandiko ya
bibilia yanayosema kuwa , nendeni mkaijaze dunia badala yake jamii imejenga
tabia ya kuzaliana hovyo na halimaye kushindwa kuimudu familia huku watoto
wakiteseka kwa kukosa chakula na elimu’’alisema
Askofu Isangya ambaye ni mwanzilishi wa makanisa ya
kipentekoste wilayani humo,alisema kuwa taifa kwa sasa linakabiliwa sana na
changamoto ya umaskini na ajira kwa wananchi wake na hivyo akaitaka jamii
kuisaidia serikali kwa kupunguza idadi kuzaliana ili iweze kumudu watu wake.
‘’ jamani tusipende kuilaumu sana serikali kwa
suala ya ajira ,lazima na sisi tupunguze
idadi ya kuzaa watoto wengi kwani kwa
kufanya hivyo serikali itaweza kukabili masuala ya njaa ,ajira na umaskini’’alisema
Askofu.
Aidha aliwataka wahitimu hao kuzingatia yale yote waliojifunza
na kwenda kuyatangaza kote duniani,waelimishe jamii kimwili na kiroho iweze
kuishi kwa amani ,hata hivyo Askofu Isangya alijivunia chuo hicho kilichoanzishwa
mwaka 1983 kwa kuhitimisha wanafunzi zaidi ya 6000 hadi kufikia mwaka huu ambao
wamesaidia sana kutangaza amani hapa nchini na nchi za nje.
Kwa upande wao wahitimu hao wakisoma risala yao walisema
kuwa wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ya kukatika katika kwa
umeme mara kwa mara hali inayowafanya kutotimiza ma`lengo yao.
Aidha walitaja changamoto ingine inayowakabili kuwa ni
pamoja na ubovu wa miundo mbinu hasa bara bara ya kutoka maji ya chai hadi
sakila hali inayowafanya kutopata huaduma zao za msingi pindi wanapozihitaji.
Hata hivyo walitaja mafanikio waliyowanayo tangu
kuanzishwa kwa chuo hicho kuwa ni pamoja na kufanikiwa kuwachimba wananchi visima 52 vya maji kwa ajili ya kukabiliana na
upungufu wa maji pamoja na kuwa na mpango wa kuanzisha vyuo vingine afrika ili viweze kuhudumia jamii nzima.
No comments:
Post a Comment