WASIOTUMIA ARDHI MERU
KUNYANGANYWA NA KUPEWA WATU WENYE UHITAJI-MKUU WA WILAYA
Na Queen Lema, Meru
WILAYA ya Meru inatarajia kuboresha mipango mbalimbali ya matumizi bora ya ardhi ambapo pia
itawanyanganya mashamba wamiliki wa mashamba makubwa ambao hawayatumii na
badala yake mashamba hayo yatatumika kwa matumizi mbalimbali ya ardhi
Kauli hiyo imetolewa
Wilayani humo na mkuu wa wilaya hiyo bw Munasa Nyirembe wakati kiongea na
wananchi wa wilaya hiyo ndani ya maazimisho ya Miaka hamsini na moja ya wilaya
hiyo mapema jana
Bw Munasa alisema
kuwa mikakati ambayo ipo kw sasa ndani ya wilaya hiyo ni kuhakikisha kuwa kila
mwananchi anajua vema matumizi ya ardhi bora ingawaje wapo baadhi ya wananchi
na wawekezaji ambao hawatumii mashamba na badala yake kuyaacha hivyo hivyo
Alisema kuwa mpngo huo
wa kuchukua ardhi ambazo hazitumiki kwa muda mrefu utaweza kusaidia sana
kuraisisha maendeleo ya wilaya hiyo kwani bado wapo watu wengi sana ambao
wanakabiliw na uhaba wa ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali huku matumizi
hayo ya ardhi bora yakiwa ni moja ya vichocheo vya uchumi wa Nchi
“pamoja na kuwa tuna
mikakati ya aina mbalimbali ya kuhakikisha kuwa tuna kuwa na matumizi bora ya
ardhi lakini pia hii itasadia sana kwa kuhaikisha wale ambao wana nunua ardhi
kwa muda mrefu bila kutumia wataweza kutumia tena kwa njia ambayo itaweza
kukuza na kuimarisha uchumi waWilaya kwa kuwa wengine wananunua ardhi na kuacha
huku wenzao wakikosa ardhi kwa ajili ya
matumizi mbalimbali’aliongeza Bw Munasa.
Pia alisema kuwa
mkakati mwingine ambao utaweza kuboresha wilaya hiyo hasa katika masuala ya
uchumi ni pamoja na suala zima la upimaji wa ardhi ambao utaenda sanjari na
suala zima la utoaji wa hati miliki tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa
hakuna suala la hati miliki za viwanja
“kwa kipindi kirefu
sana wananchi wameteseka hata kwa kunyimwa mikopo ndani ya taasisi mbalimbali
za fedha lakini kama watapata haki miliki basi wataweza kuzitumia kwa ajili ya
mikopo hivyo tunaamini kabisa hili suala litaweza kuongeza ufanisi wa kiuchumi
ndani ya vijiji vyetu na hata wilaya yetu kwa ujumla’alisem Munasa
Katika hatua nyingine
alisema kuwa mbali na kuchukua viwanja ambavyo havitumiki pia wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali hasa kwenye sekta ya Kilimo kwa kuwa kwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la
eneo linalolimwa hasa kwenye mazao ya chakula kutoka hekta 80,000hadi kufikia
hekta 121,387 sawa na asilimia 51.73
Bw Munasa alisema
kuwa ongezeko hilo limesababisha changamoto kama vile kilimo kisichozingatia hifadhi
ya ardhi na maji,bei kubwa za pembejeo na tatizo la soko la kuaminika kutokana
na bei ndogo zinazotolewa.
Alibainisha kuwa
kutokana na hali hiyo Wilaya kwa sasa imeamua kutumia mbinu mbalimbali kama
vile kutumia teknolojia za kisasa,kuanzisha na kuimarisha ushirika wa vyama vya
kuweka na kukopa kwa ajili ya kupata mitaji na kutafuta masoko
MWISHO
No comments:
Post a Comment