Mbunge Nassari wa CHADEMA Meru asusia Baraza la
Madiwani
Na Mary Mwita ,Arumeru .
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia
tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Joshua Nasari amesusia kikao
cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Meru ,baada ya kamati ya
Uchumi ,Ujenzi na Mazingira ,kuelezea nia ya kuwagawa viwanja kwa Vijana
na wananchi kupitia kata zao katika eneo la Soko la Tengeru.
Mbunge huyo alishangaza Baraza hilo ,baada ya kudai
kuwa eneo hilo linapaswa kujengwa vitega uchumi na wawekezaji na siyo kupewa
wananchi na Vijana kama kamati ya uchumi ilivyoazimia na kukubaliwa
na Baraza kuendelea na maamuzi hayo kwa kugawa viwanja kupitia kata.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Frida Kaaya
akielezea sakata hilo aliliambia Baraza hilo kuwa ameshangazwa na maamuzi ya Mbunge huyo ambaye
alisema ni Diwani akiwa katika Baraza hilo
,kuwa alipaswa kukubali maamuzi ya Madiwani wenzake .
Alisema kuwa viwanja vinavyotarajiwa kugawanywa ni
Viwanja 118 ,vitakavyojengwa kuzunguka soko na hivyo kufanikiwa kuwaondoa
wafanyabiashara wanaopanga bidhaa chini .
Alifafanua kuwa kwa sasa Halmashauri hiyo imeanza
kujikita kusaidia Vijana ,na kuwa kugawanywa viwanja hivyo kutalenga vikundi
vya vijana ,ili waweze kufungua miradi ya maendeleo kupitia
vikundi,hatimaye kuweza kujikwamua katika uchumi na kuongeza kipato chao .
Diwani wa Kata ya Nkwarusambo akizungumza katika kikao
hicho alimtaka Diwani Nassari kuheshimu maamuzi ya vikao vya baraza na
kushirikiana na madiwani wenzake kulewatea wananchi maendeleo na siyo kupinga
kila kitu hata kama ni jambo jema .
Alisema kuwa Halmashauri hiyo ,inasifiwa kuwa na
ushirikiano mzuri na wananchi ,na kuwa Mbunge huyo anatakiwa kuepuka migogoro
isiyokuwa na na lazima .
Kwa upande wake Mbunge Nassari aliwaambia waandishi wa
habari kuwa ,hakubaliani na kamati ya Uchumi na Baraza hilo ,kwa kuwa wamekiuka
makubaliano ya awali ya kujenga vitega uchumi katika eneo ,na kudai kuwa
anahisi kuna mchezo unataka kufanyika .
‘Mimi nina historia ndefu ,siku zote ,kuwa Viwanja
vikitolewa wanaokuja kununua ni watu wa Arusha mjini ,watu wa Moshi na watu wa
Meru hawaambulii chochote ,kwa hiyo ,ni mara kumi vikajengwa vitega uchumi ,ili
wananchi waje wafanyie biashara badala ya kugawa kama Kamati ya Uchumi
ilivyopendekeza “ anasema Nassari
‘
No comments:
Post a Comment