WATANZIA wenye
asili ya Kiasia 300,akiwemo na mwakilishi wa radio uhuru mkoa wa Arusha,
wamejitokeza kuchangia damu kwenye mpango wa taifa wa damu salama kanda ya
kaskazini katika zoezi liliofanyika hospital ya Shree Hindu Union Tample
jijini Arusha iliyoandaliwa na Patel Commonity na Koja Ithinasheri
.
Zoezi hilo linafuatia kuwepo
uhaba wa damu katika hospital ya mkoa wa Arusha, ambayo inakabiliwa na wagonjwa
wengi hasa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano wenye mahitaji ya damu
Mgeni rasmi katika
zoezi hilo ,mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliyewakilishwa na mkuu wa
wilaya ya Arumeru, Mnasa Deusi Sabhi,amesema uchangiaji huo ni kuunga mkono
juhudi za rais Kikwete za kuokoa maisha ya wajawazito, watoto wakati wa
kujifungua pia majeruhi wa pikipiki wanaohitaji kuongezewa damu wakati wa
matibabu.
Mulongo amesema
kuwa hospital ya mkoa inahitaji 80 % ya damu lakini imekuwa ikipokea asilimia
30 hadi 40 tu hivyo mahitaji ya damu bado ni makubwa akawaomba wananchi
kujitokeza kwa wingi ili kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya
wajawazito na watoto chini ya miaka mitano na wanaopata ajali za pikipiki.
“Damu hii
inayotolewa na wananchi haiuzwi na ole wake mtumishi wa hospital
atakayejihusisha na kuiuza ata shughulikiwa mara moja, damu haina mbadala wala
haizalishwi kutoka popote” ,alisema mkuu wa mkoa .
Amesema mpango
huo wa kuchangia damu ni kuunga mkono juhudi za rais Kikwete ambae ni
mwenyekiti wa mpango wa Umoja wa mataifa wa kuhusu afya ya uzazi duniani
Nae mwenyekiti
wa jumuia ya Patel ,Kanu Patel, amesema wamefikia uamzi huo wa kuchangia damu
kwa sababu katika hospital ya mkoa wa Arusha watu wanapoteza maisha kutokana na
kukosa damu
Amesema jumuia
ya Patel inakusudia kuendesha zoezi lingine la kuchangia damu Januari 15 hadi
17 mwakani litakalofanyika mjini Arusha hivyo akawaomba wananchi
kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu.
Mganga mkuu wa
mkoa wa Arusha, Dakta Frida Mokiti, amesema kuwa vifo vng vinavyotokea katika
hospiotal ya mkoa husababishwa na upungufu wa damu.
Amesema upungufu
wa damu unashikilia nafasi ya pili kwa vifo vya wagonjwa wanaolazwa katika
hospital ya mount Meru,hasa wajawazito wanaotokwa na damu nyingi wakati wa
kujifungua na watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano ambapo ugonjwa
wa Ukimwi ndio unashika nafasi ya kwanza kwa vifo .Ameipongeza jumuia hizo za
Patel na Koja Ithinasheri, kwa kuendesha zoezi hilo la kuokoa maisha ya
wananchi ambao wanakosa damu wakati wa matibabu .
No comments:
Post a Comment