Monday, December 3, 2012

MABENKI UNGANISHENI HUDUMA ZA KIFEDHA

GAVANA BENNO NDULU



GAVANA wa benki kuu  ya Tanzania,Benno Ndulu  ameyataka mabenki
mbalimbali nchini kuunganisha huduma za benki na mawakala wa simu za
mkononi ili kuwawezesha wateja kupata huduma kwa urahisi na njia
salama zaidi.

Aliyasema hayo wakati akizungumza  katika mkutano wa 16 wa taasisi za
fedha uliofanyika mjini hapa uliolenga kujadili mbinu mbalimbali za
benki kujiunganisha na huduma za simu ili kuwawezesha wananchi
kupata huduma hizo kwa urahisi
.
Alisema kuwa, huduma hiyo tayari imeshaanza kutumika katika mabenki
mengine na huduma hiyo imeshaonyesha mafanikio makubwa sana ,hivyo
wajibu walioko nao kwa sasa ni kuhakikisha wanahamasisha benki zingine
kuhakikisha zinajiunganisha na huduma za simu.

Profesa Ndulu alisema kuwa, kupitia mkutano huo watajadili mbinu
mbalimbali za kuwahamasisha mabenki kutoa huduma za kibenki kwa
kupitia mawakala wa simu za mikononi kwani kwa kufanya hivyo
kutawezesha kuondokana na changamoto mbalimbali za upotevu wa fedha na
usalama wake kwa ujumla.

‘sisi  tunajitahidi sana kuboresha huduma zetu za kibenki  kwa kubuni
mbinu mbalimbali ikiwemo hiyo ya kutoa huduma za kibenki kwa kutumia
simu za mikononi , na huduma hiyo tunahakikisha imefika katika maeneo
mbalimbali hususani ya vijijini ili kuondokana na changamoto
mbalimbali za kufuata huduma hizo mbali’alisema Ndulu.

Alifafanua zaidi kuwa,kupitia njia hiyo itawezesha kutoa huduma kwa
njia rahisi kwa wananchi wake na kuwezesha kupata huduma hiyo kwa
urahisi zaidi ,na mahali popote kwani hiyo ni njia ya usalama zaidi na
inamwezesha mteja kuweza kupata huduma hiyo wakati wowote anapohitaji.

Aidha aliyataka mabenki kuhakikisha kuwa yanapanua huduma zake kwa
njia hiyo ya simu za mkononi kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha
wananchi wengi  kunufaika na huduma za kibenki kupitia simu za mkononi
kwani njia hiyo ni salama nay a uhakika zaidi.

Aidha Profesa Ndulu alitaja faida zinazotokana na huduma hiyo kuwa ni
usalama wa fedha za wateja kutokana na huduma hiyo kuwa ya bei nafuu
na ya uhakika zaidi , huku ikimwezesha mwananchi kufikiwa na huduma
hiyo popote alipo na kwa  haraka zaidi.

Profesa Ndulu alisema kuwa, huduma hiyo imekuwa ikitumiwa na wananchi
wengi ambapo hadi septemba mwaka huu jumla ya wananchi 20.5 milioni
wametumia huduma ya mpesa ,hivyo  idadi hiyo inazidi kuongezeka siku
hadi siku kutokana na huduma hiyo kupendwa na wananchi walio wengi .

Profesa Ndulu aliwataka  wadau mbalimbali wa benki  kuhakikisha kuwa
wanaiboresha huduma hiyo ili kuongeza kasi zaidi ya kuwahudumia wateja
wake , huku ikilinganishwa kuwa hitaji wa wananchi wanaohitaji huduma
hiyo inazidi kuongezeka siku hadi siku.
Mwisho.


No comments:

Post a Comment