WANANCHI WA ARUSHA VIJIJINI WAWATAKA MAAFISA MALI ASILI
KUFIKA VIJIJINI NA KUACHA TABIA YA KUKAA MIJINI
Na Queen Lema, ARUSHA
IMEELEZWA kuwa kutokana na baadhi ya maafisa mali asili na
mazingira kushindwa kufika vijijini kumesababisha vyanzo vingi vya mazingira
kuendelea kuharibiwa ovyo na wananchi huku serikali ikiwa inadai mazingira
yatunzwe
Asilimia kubwa ya watendaji hawa wa mazingira hawana
mwitikio wa kuja vijijini na kuangalia vyanzo mbalimbali na badala yake wanafanya
kazi zao wakiwa maofisini pekee hali ambayo inasababisha kila mara kuwepo na
uharibifu wa mazingira
Kauli hiyo imetolewa na Wananchi wa wilaya ya Arusha
Vijijini wakati wakiongea katika mdahalo unaohusiana na mabadiliko ya Tabia za
Nchi uliofanyika chini ya mtandao wa asasi binafsi hapa mkoani Arusha
(ANGONET)mapema jana.
Wananchi hao walisema kuwa kila siku ndani ya vyombo vya
habari wanasikia kuwa wanatakiwa kutunza na kuthamini mazingira lakini bado
elimu haiwafikii jamii hali ambayo bado ni sawa na kazi bure huku vijijini
kukiwa na changamoto lukuki sana
za uharibifu wa mazingira.
“suala la utunzaji wa mazingira bado ni suala tete sana
ndani ya halmashauri hii ya Arusha vijijini kwa kuwa wananchi hatuna elimu hata
kidogo ya mazingira na maafisa maliasili wetu wanakaa tu maofisini kwenye
viyoyozi huku sisi tukiwa tunaambiwa kuwa tutunza mazingira na tuhakikishe kuwa
tunakwepa uharibifu sasa sisi wa vijijini mara nyingine huwa tunaharibu
mazingira kwa kuwa hatuna elimu lakini kama tungekuwa tunawaona hawa maafisa
maliasili na mazingira basi vijijini tungekuwa na nafasi sana ya kuweza kutunza
sana mazingira’waliongeza wananchi hao.
Awali Mratibu wa Mtandao wa asasi binafsi mkoani Arusha Bw
Peter Bayo alisema kuwa lengo halisi la kufanya Mdahalo huo kwa Wilaya zote za
mkoa wa Arusha ni kuhakikisha kuwa wananchi hasa wa vijijini wanakuwa na uelewa
halisi wa masuala ya mazingira kwani bado mabadiliko ya Tabia za nchi
yanaathiri sana maendeleo ya Jamii.
Bw Bayo alisema kuwa bado kuna changamoto kubwa sana ya uharibifu wa mazingira hususani ya maeneo ya vijijini ambapo baadhi ya Sera za mazingira
na misitu hazifuatwiu na watendaji wa Serikali hali ambayo inachangia sana kukitihiuri kwa
mabadiliko ya tabia za nchi.
‘suala la mazingira linaendana na uchumi sasa bado kuna
uhitaji mkubwa sana wa kuhakikisha wananchi hasa wale wa vijijini wanakuwa na
elimu ingawaje changamoto kubwa sana kwa sasa ni baadhi ya watendaji kushindwa
kufika vijijini kutokana na uhaba wa usafiri”aliongeza Bw Bayo
Naye afisa misitu katika halmashauri ya Arusha Vijijini Bw
Semu Sikawa alisema kuwa wanauhitaji mkubwa sana wa kufika Vijijini kusaidia jamii dhidi
ya mabadiliko ya tabia za nchi lakini kitu kikubwa kinachowakamisha ni uhaba wa
vifaa vya kazi,pamoja na uhaba wa watumishi hali ambayo inawafanya washindwe
kufika vijijini
No comments:
Post a Comment