Serikali ya Poland yakabithi miradi
yenye thamani ya USD 360,000 kwa chuo cha Mifugo Kampasi ya LITA –Tengeru.
Happy Lazaro, Arusha.
SERIKALI ya Poland imekabithi na kuzindua jumla ya
miradi mitatu yenye thamani ya USD 360,000 iliyopo katika chuo cha mifugo Campus ya LITA Tengeru
, katika hafla iliyofanyika hivi karibuni chuoni hapo.
Aidha hafla
hiyo ya makabithiano ilihudhuriwa na Mwakilishi kutoka wizara ya mambo ya nje
(Poland) ,Dr. Inveterinary and medicine
PHD holder ,Dr. Maciej klockiewicz ,na
Mkurugenzi wa mradi huo, Dr.Eng.Wieslaw Ptach kutoka serikali ya Poland.
Akizungumzia
miradi hiyo katika uzinduzi huo,Mkufunzi wa chuo hicho, David Malishi alisema
kuwa awamu ya kwanza ya miradi hiyo ilianza rasmi mwaka 2009 ambapo wafadhili
hao walianza kwa kununua vifaa mbalimbali vya kufundishia vikiwemo vya maabara.
Ambapo awamu
ya pili mradi ulilenga kuimarisha matumizi mazuri ya maji ili kuboresha
uzalishaji wa mazao katika malisho ya mifugo na chakula ,pamoja na zana za kilimo ambapo waliweza
kuchimba bwawa la kuhifadhia maji ya umwagiliaji na kujenga mifereji ili
kuimarisha umwagiliaji.
Malishi
alisema kuwa, mradi wa awamu ya tatu ulijikita zaidi katika umwagiliaji na
ujenzi wa mitambo ya bioges na upandaji miti ambapo waliweza kukabithi pump za
kumwagilia maji 2,pamoja na kukabithi visima 3 vya maji kila moja ikiwa na
quibick mita 50 .
Aliongeza
kuwa, katika bioges waliweza kukabithi jumla ya mitambo 2 ya bioges kila moja
ikiwa na quibick mita 50 ,ikiwa ni pamoja na upandaji miti ambapo kwa msimu wa
mwezi wa 3 hadi 6 jumla ya miti 4500 ilioteshwa kwa mchango wa serikali ya tanzania
.
Alisema
kuwa, katika miradi hiyo yote mitatu serikali ya Tanzania imeweza kuchangia
asilimia 30 kama mchango wao .
Malishi
alisema kuwa , kupitia miradi hiyo na kupatiwa vifaa mvalimbali hivi sasa
wameweza kuboresha ufundishaji kwa vitendo zaidi kutokana na kuwepo kwa vifaa
mbalimbali tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
‘Unajua hawa
wafadhili wetu wa serikali ya Poland wametusaidia sana kwani chuo hiki ni cha
zamani na kilikuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi sana ili kuweza kutoa elimu iliyo bora hivyo kwa
sasa hivi kupitia miradi hiyo imesaidia chuo chetu kuweza kuonekana cha kisasa
zaidi na kuendelea kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaokuja chuoni hapo kila
mwaka’alisema Malishi.
Alitaja changamoto
kubwa ambayo inawakabili chuoni hapo na taasisi zote za eneo la LITA Tengeru ni uhitaji mkubwa wa maji ambapo kwa makisio
wanahitaji USD 110,000 ili kujenga vizima ,hivyo pendekezo hilo wamelipeleka
kwa wafadhili hao wa serikali ya Poland kuona kama watawawezesha .
Naye mgeni
rasmi katika uzinduzi huo, Naibu Katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi , Dkt
Yohana Badeba alisema kuwa kuwepo kwa uhsirikiano huo mzuri katika ya serikali
ya Poland na Tanzania utawezesha kwa kiasi kikubwa kuzidi kuboresha miradi
mbalimbali katika chuo hicho kwani kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi
sana.
Aliwashuruku
wafadhili hao kwa msaada mkubwa walionyesha chuoni hapo wa kujenga miradi
mbalimbali itakayowezesha chuo hicho kuweza kufikia malengo yake waliyojiwekea
,hivyo kuwasihi kuzidisha ushirikiano huo zaidi.
Alikitaka
chuo hicho la mifugo LITA kutumia vifaa mbalimbali walivyokabithiwa kwa ajili
ya kuboresha chuo hicho kuhakikisha wanazitumia ipasavyo na kwa manufaa ya chuo
hicho kwa ujumla.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment