Na Mwandishi wetu ,Arusha .
MKUU wa Mkoa wa Arusha
amemzawadia tuzo ya uandishi bora wa habari za jamii na maendeleo Meru , mwandishi
wa habari Mary Mwita wa
magazeti ya Mtanzania na Rai ya Kampuni
ya New habari (2006) LTD.
Mkuu wa Mkoa huyo ametoa tuzo hiyo ,ikiwa ni ahadi yake ,na agizo
alilotoa kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kupeleka jina la Mwandishi wa habari
aliyeandika habari bila kupotosha jamii katika Halmashauri hiyo ,na kuweza
kumpata Mwandishi huyo .
Mkuu alitoa Tshs 500,000
ikiwa ni tuzo na kiasi cha fedha
zilizokabidhiwa kwa wadau wengine mwaka
huu waliobainika kuchangia maendeleo ya Meru.
Mkuu huyo alisema kuwa huwezi kutaja maendeleo bila kuhusisha vyombo
vya habari na waandishi wa habari ,na kuwa kila Halmashauri inatakiwa
kutambua mchango wa maendeleo ya wadau ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari .
Akimpongeza Mwandishi Mary Mwita ,alisema wakati umefika wa
waandishi wa habari kuandika habari za kweli
bila kupotosha umma ,ikiwa ni kuwawezesha wananchi kujifunza na kupata
ujuzi kupitia habari hiyo ,badala ya kuandika habari za uongo .
Mlongo alisema kuwa ni wazi
kuwa kila mtu katika jamii akisimama katika nafsi yake kulingana na karama
aliyopewa Maendeleo ya haraka yatafikiwa na kuwawezesha wananchi kupunguza kasi
ya umaskini katika jamii .
Katika hatua nyingine
alipongeza uongozi wa Halmashauri ya Meru kwa kutambua mchango wa maendeleo ya
wadau na kutaka Halmashauri nyingine
kuiga mfano huo wa kutunikia zawadi wadau waliosaidia maendeleo ya Halmashauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru
Trisas Kagenzi alisema kuwa zoezi la
kuwazawadia wadau ni endelevu ,na kuwa wataendelea kutambua mchango wao kwa
kuwa bila ushirikiano na wadau wa
maendeleo ,maendeleo yanaweza kuchelewa .
Kagenzi alisema kuwa
Mwandishi Mary Mwita ,amekuwa akiandika habari bila kupotosha umma kwa kujituma na kutaka waandishi wengine
kuiga mfano wake.
No comments:
Post a Comment