WAOMBA KUPANDISHIWA HADHI ZAHANATI ALIYOZINDUA MAMA NYERERE
MWAKA 1964
Na Queen Lema,MERU
SERIKALI imeombwa kupandisha hadhi zahanati ya kata ya
Majengo wilayani Meru mkoani Arusha ambapo zahanati hiyo ilizinduliwa rasmi na kupewa
misaada na Mama Maria Nyerere mwaka 1964 huku malengo ya Mama huyo yakiwa ni
kubadilika kutoka zahanati na kuja kituo cha afya kwa haraka sana jambo ambalo mpaka sasa halijafanyiwa
kazi.
Hayo yamebainishwa na Paulo Mayeke ambaye ni katibu
kata ya Majengo,wakati akiongea na Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi
mkoa wa Arusha waliotembelea Kata hiyo na kuzindua Kata mpya ya chama cha
mapinduzi mapema jana.
Aidha bw Mayeke alisema kuwa Zahanati hiyo ya Majengo
ilizunduliwa Rasmi na Mama Nyerere huku lengo halisi la Mama huyo likiwa ni zahanati
hiyo isidumu kama zahanati na badala yake iwe kwenye mfumo wa kituo cha afya
ili kiweze kuhudumia watu wengi zaidi hata wa vijiji vya Jirani kwa kuwa Kata
hiyo ipo Karibu sana na Machimbo ya madini ya Tanzanite
Aliendelea kwa kusema kuwa endapo kama Serikali
ya sasa itakumbuka na kurejea kauli na ahadi ya Mama Maria Nyerere basi itachangia kwa
kiwango kikubwa sana kuraisisha shuguli za afya ndani ya Kata hiyo ambayo
imedumu na zahanati badala ya kituo cha afya kwa muda mrefu sana huku jamii
nayo ikiendelea kukabiliwa na Magonjwa mbalimbali.
Alisema kuwa endapo kama itakuwa katika mfumo
wa Zahanati basi itachangia sana kuokoa maisha ya watu kwani itakuwa na
wataalamu wengi wa afya tofauti na sasa ambapo kutokana na hadhi yake
inawahudumu wachache sana wa Afya hali ambayo inachangia sana wananchi kutembea
umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma hizo.
“jamani hii zahanati ya kata ya Majengo ilizinduliwa na
kupewa mikakati mbalimbali na Mama Nyerere kwa mwaka 1964 lakini moja ya
msisitizo wake mkubwa ilikuwa ni kuwa katika hadhi ya kituo cha afya lakini
toka siku ile ameondoka Kijijini hapa hakuna kilichoendelea hivyo basi tunaomba
Serikali itusaidie kwani Wananchi wetu wanapata shida kubwa sana ya matibabu na
hivyo kama watafanya hivyo wataweza okoa maisha ya watu wengi zaidi”aliongeza
Bw Mayeke
Awali mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Bw
Onesmo Nangole alisema kuwa watendaji wa chama hicho kuanzia ngazi ya Vitongoji
mpaka mkoa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatatua na kusikiliza kero mbalimbali
za wananchi sanjari na kutafutia ufumbuzi jambo ambalo litaweza kuwafanya
wananchi kuwa katika kundi moja la chama hicho
Bw Nangole aliongeza kuwa tabia ya Viongozi kukaa kimya na
kusinzia huku wakijiita ni viongozi haipaswi kuvumikila kwani tabia hiyo ndiyo
inayochochea Kero kubwa sana
kwa wananchi na hata mara nyingine kusababisha ahadi mbalimbali zishindwe
kutekelezwa huku wananchi nao wakielekeza lawama kwa Chama cha Mapinduzi(CCM)
“Nawasihi sana
Viongozi kuanzia ngazi ya chini kuamka kuanzia sasa acheni kuwapa wapinzani
nguvu kwa kero za wananchi mbona mnauwezo wa kuweza kufanya mabadiliko na
changamoto hata ahadi mbalimbali mkazifuatilia,kwa kuwa sasa hivi changamoto
yoyote ile kwenye jamii ndio nguvu ya wapinzani sasa hakikisheni kuwa hawa
wapinzani wanakosa nguvu kabisa”aliongeza Bw Nangole
MWISHO
No comments:
Post a Comment