Joseph Ngilisho,Arumeru.
WAZAZI katika shule ya
msingi ya Mwandeti iliyopo wilayani Arumeru,mkoani Arusha,wameukataa uongozi wa
shule hiyo pamoja na kamati yake kwa madai ya ubadhilifu wa mali za shule na
kueleza kuwa hawatoshiriki shughuli za maendeleo ya shule hiyo hadi mkuu wa shule hiyo,Elibariki Laizer aondolewe.
Aidha wamemtuhumu mkuu huyo
washule,kwenda kinyume na taratibu za uongozi wa shule hiyo kwa kuiendesha kama mali yake,kujimilikisha mashamba ya shule
na kuingia ubia wa shambe la shule lenye ukubwa ekari 6 na wafanyabishara bila kufuata
utaratibu,kuchangisha michango hovyo kwa wanafunzi ikiwemo kuwalipisha faini
wanapochelewa kufika shuleni ama kutofika kabisa.
Wakizungumza kwenye kikao
cha shule kilichofanyika shuleni hapo jana,wazazi hao wa jamii ya wafugaji wamemtaka
mwalimu huyo kuondoka shuleni hapo kwani pamoja na mambo mengine, kiwango cha
taaluma kwa wanafunzi kimeshuka.
Mmoja wa wazazi hao,Lugion
Leshiloi amesema kuwa mwalimu Laizer tangu ahamishiwe kwenye shule hiyo mwaka
2007 shule hiyo ambayo ilijengwa kwa msaada wa wazazi na mashirika mbalimbali,
kwa sasa imechakaa,majengo yamepasuka na kuhatarisha maisha ya wanafunzi ,milango
na vioo vya madirisha vimeibwa bila kuwemo uangalizi.
Alisema kuwa kwa sasa
hawana imani na mwalimu huyo, kwani kuendelea kuwepo shuleni hapo kutaifanya
shule hiyo ifilisike zaidi huku wanafunzi wakiumia kwa michango mbalimbali
ambayo mara nyingi haina hata risiti,na kwamba wengi wa wanafunzi wameshindwa
kuendelea na masomo kutokana na kero mbalimbali za mkuu huyo wa shule na
kujikuta idadi ya wanafunzi kwa sasa ikifikia
700 kutoka wanafunzi 1000 waliokuwepo.
‘’shule imekufa haina
uangalizi ,majengo yamepasuka kila kona ,tunachotaka ni mwalimu mkuu na kamati
yake waondoke,bila hivyo hatutatoa ushirikiano na shule hii’’alisem mzazi
Samwel Mseyeke ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa kijiji
Naye mzazi ,Jonas Klasian
alimtuhumu mkuu huyo wa shule kwa kuwachangisha wanafunzi michango nya shilingi
1000 kila wiki huku wanaochelewa kufika shuleni hulipishwa shilingi 500 hadi
1000 na wale wanaoshindwa kufika kabisa shuleni kwa siku moja huwalazimu kulipa
shilingi 2000 hadi 2500 huku akiwasisitiza wazazi ambao hawatoi michango ya
watoto wao ,kuwaondoa watoto wao shuleni hapo.
Wazazi hao wamesusia taarifa
ya mapato na matumizi ya mwaka 2011/12 iliyoandaliwa na mkuu huyo wa shule na
kusomwa katika mkutano huo wakidai kwamba imechakachuliwa na imejaa ubabaishaji
kwani idadi ya fedha zilizosomwa kutumika zimepandikiziwa na wanawasiwasi hazikutumika
kwa matumizi hayo yaliyotajwa.
Akijibu tuhuma hizo mkuu wa
shule huyo,Elibariki Laizer alisema kuwa tuhuma hizo ni majungu ya wananchi hao zenye lengo la
kumchafua huku akifafanua kwamba utaratibu kuingia ubia wa mashamba ya shule
upo wazi kwani walifanya hivyo kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wanafunzi wa
kulima mashamba hayo muda wa masomo.
Akizungumzia suala la wazazi
kukataa taarifa ya mapato na matumizi alisema kuwa fedha zote zilizoingia shuleni
hapo zimetumika kama ipasavyo na hakukuwa na taarifa iliyopotoshwa na kwamba
suala na shule kuchakaa ni wazazi ndio wameitelekeza na sio jukumu lake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment