WATIENI
MOYO WALE WALIOKATA TAMAA
NA
BETY ALEX,ARUSHA
MAKANISA
mbalimbali hapa nchini yameshauriwa kujiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa
yanawatia moyo waumini wake kwa kuwakusanya sehemu moja kwani kupitia umoja huo
utaweza kuwasaidia hata walio kata tamaa katika mambo mbalimbali kuweza kusonga
mbele zaidi.
Akiongea
na “Nyakati”mara baada ya kuwakusanya waumini wa baadhi ya makanisa ya
PEFA mjini, Mchungaji Noel Urio alisema kuwa kama makanisa hayo yataweza
kufanya hivyo yatasaidia sana
kuwatia moyo
Noel
alisema kuwa asilimia kubwa sana ya waumini
ambao wapo makanisani sio kuwa wote wapo vizuri lakini bado kuna wengine ambao
wanakabiliwa na matatizo ya hali ya juu sana
lakini kama kanisa litatumia nafasi hiyo
litaokoa kondoo wengi zaidi
Aliongeza
kuwa waumini wanapokaa pamoja na kushiriki kwa pamoja masuala mbalimbali hata kama ni chakula cha mchana au usiku kunasababisha hata
waliokata tama kuweza kuibuka tena na kufanya mabadiliko hata ya kimwili na
kiroho
‘hakuna
kiti kibaya sana kama mtu anapokata tama lakini
faraja yake inatakiwa kupatikana makanisani na makanisani ni vema basi hata
siku moja kanisa likatenga siku ya kuhakikisha kuwa wanabadilishana mawazo na kama waumini wataweza kubadilishana mawazo basi muafaka
wa kukua kwa kiroho utapanda sana’aliongeza Noel
Katika
hatua nyingine alisema kuwa nao waumini wanapaswa kujua na kutambua kuwa kamwe
watu hawapaswi kukata tama kwani kukata tama ni dhambi kubwa sana na ukataji wa tama ndiyo nafasi shetani
anayoitumia kuwarudisha watu nyuma katika msingi wa imani za leo
Alifafanua
kuwa hata kama mtu akikumbwa na matatizo ya
aina gani kamwe hapaswi kukata tamaa bali anapaswa kuangalia makusudi ya mungu
yanavyosema na kudai na pia kabla ya kukata tamaa wanatakiwa kuangalia
wachungaji wao wa makanisa ili waweze kutiwa moyo
‘Kazi
kubwa sana ya
kanisa ni kuwatia watu moyo sasa unapokuja kanisa ukiwa umekata tamaa na
kisha ukamlilia Mungu pamoja na kumshirikusha hata Mchungaji wako unaweza
kusonga mbele zaidi kuliko kukaa kimya ,na hapo kazi ya kanisa itajulikana kwa
kuwa utaweza kusimama na kutiwa Moyo hivyo utashinda tu”aliongeza Mchungaji
huyo
MWISHO
No comments:
Post a Comment