WAZIRI WA ZAMANI WA MIPANGO WA RWANDA AHUKUMIWA MIAKA 35 JELA
Na Nicodemus Ikonko, Hirondelle, Arusha
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya
Rwanda(ICTR) imemhukumu kifungo cha mika 35 jela Waziri wa zamani wa
Mipango wa Rwanda,Augustin Ngirabatwara baada ya kumtia hatiani kwa
mashitaka matatu ya mauaji ya kimbari.
Mahakama
iliyokuwa inaongozwa na Jaji William Sekule kwa kauli moja imemtia
hatiani ngirabatware kwa mashitaka ya mauaji ya kimbari, uchochezi na
ubakaji kama uhalifu dhidi ya binadamu.
‘’Augustin
Ngirabatware, mahakama imekuona una hatia kwa mauaji ya kimbari,
uchochezi na ubakaji kama uhalifu dhidi ya binadamu,’’ Jaji Sekule
alisema huku Ngirabatware akielekeza uso wake chini.
‘’Kwa
uhalifu huu na kwa kuzingatia mazingira yote ya kesi hii, mahakama
inakuhukumu kifungo cha miaka 35 jela,’’ alitamka Jaji Sekule.
Katika
hukumu yake,mahakama imemtia hatiani Waziri huyo wa zamani kwa mauaji
ya kimbari kutokana na ukweli kwamba alichochea, kusaidia na kuunga
mkono mashambulizi na mauaji dhidi ya Watutsi katika wilaya yake ya
Nyanyumba, mkoa wa Gisenyi, Kaskazini mwa Rwanda alikozaliwa.
Alitekeleza uhalifu huo kwa kwa kupitia hotuba na vitendo vyake kwa
kugawa silaha Aprili 7, 1994.
Mahakama
ilibaini kwamba baadhi ya silaha zilizogawanywa kwa wanamgambo wa
interahamwe zilitumika katika mashambulizi na mauaji na kwamba maneno
yake na vitendo vyote kwa pamoja vilitoa hamasi kwa wanamgambo hao
kufanya uhalifu huo katika wilaya ya Nyamnyumba.
Ngirabatware
ambaye ni mkwe wa mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ambaye bado anasakwa
vikali na ICTR alijitetea kwa kudai kwamba wakati mauaji hayo
yanafanyika yeye hakuwepo wilayani kwake, utetezi ambao ulitupwa na
mahakama.
Mfungwa
huyo, ambaye kitaaluma ni daktari wa uchumi alitiwa mbaroni nchini
Ujerumani Septemba 17,2007 na kisha kuhamishiwa Arusha, makao makuu ya
ICTR Oktoba 8, 2008. Kesi yake ilianza kusikilizwa Septemba 29, 2009.
No comments:
Post a Comment