Serikali yatakiwa kuondokana na tabia ya kuwa tegemezi
.
Happy Lazaro, Arusha.
SERIKALI imetakiwa kuondokana na tabia ya kuwa
tegemezi kwa nchi za nje huku ikilinganishwa kuwa Afrika ina fursa nyingi
za kutosha ambazo zinatuwezesha kufikia malengo mbalimbali bila ya kuomba
omba misaada.
Aidha endapo ukusanyaji kodi inayotokana na VAT
itaboreshwa na kulipwa kwa wakati basdi itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kupatikana kwa pato
kubwa la Taifa ambalo litawezesha nchi kujiendesha yenyewe bila kuwa tegemezi.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa fedha , William
Mgimwa alipokuwa akifungua mkutano wa wa mamlaka ya mapto katika nchi za
Afrika (VADA) pamoja na wadau walipa kodi inayotokana na VAT kutoka nchi
za Afrika uliolenga kujadili mbinu mbalimbali za kuboresha ukusanyaji
kodi .
Alisema kuwa, imefika wakati sasa kwa Tanzania
kuondokana na tabia ya kuomba misaada bila sababu wakati tuna fursa nyingi
ambazo zikiboreshwa zitawezesha kuongezeka kwa mapato ya nchi ,hivyo
kuwezesha kuongezeka kwa idadi kubwa ya miradi mbalimbali.
Alisema kuwa, ili kuwezesha kufikia malengo hayo
walipa kodi wa vat hawana budi kulipa kodi zao kwa wakati bila kukwepa kama sheria ya VAT inavyoeleza huku ikiwa ni pamoja
na kuimarisha uzalishaji , unaolenga kuondoa utegemezi huo .
Alisema kuwa, ili kuboresha ukusanyaji wa kodi kuweza
kuongezeka mwaka hadi mwaka na hatimye kufikia malengo waliyojiwekea wanaandaa
mikakati tofauti ambayo itaweza kuwasaidia ubadilishaji wa ukusanyaji kodi ili
kukusanya kodi ya kutosha.
‘Ili tuweze kufikia
malengo yetu na kuondokana na tabia ya kuwa tengemezi kwa kuomba misaada katika
nchi zingine ni lazima kodi aina ya VAT iboreshwe ili kuziba mapungufu yaliyopo
ili kuwawezesha wafanyabiashara ambao hawajalipa kodi waweze kulipa na kwa njia
hiyo tutaweza kufikia malengo yetu’alisema Mgimwa.
Mgimwa alifafanua zaidi kuwa, lengo la kuwakutanisha
wadau hao ni kubadilishana uzoefu wa jinsi ambavyo wenzetu wanavyokusanya kodi
katika nchi zao , na hatimaye kuweza kujiwekea mikakati jinsi ya kuboresha
ukusanyaji kodi inayotokana na VAT ili kuongeza pato la nchi na hatimaye
malengo yaliyowekwa yaweze kufikiwa.
Aliwataka wafanyabiashara wanaolipa kodi inayotokana
na VAT kulipa kwa wakati na kwa hiari ili kuiwezesha nchi kuwa na pato la
kutosha na hatimaye fedha zinazotokana na VAT kuweza kusaidia kuboresha miradi
mbalimbali na hatimaye kufikia malengo yaliyowekwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment