Thursday, January 30, 2014

UJIO WA HELKOPTA YA CHADEMA ARUSHA WAZUA BALAA KWA CCM

Na Mwandishi wetu, Arusha

Chama cha mapinduzi (CCM)kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)kutumia Helikpota kwenye chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni kujitafutia sifa na umaarufu pekee  kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu mkuu wa CCM ambaye pia ni Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za  udiwani katika kata ya sombetini  mapema jana.
Mwigulu alisema kuwa CCM inashangaa sana Chadema kutumia Helikpota kwenye chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo wanaonesha wazi kuwa wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa kwani gharama ambazo zinatumika hadi kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya Milioni 200.
Alisema kuwa Gharama ambayo inatumika kwenye uendeshaji wa Helkopta ni gharama ambayo ingeweza kuwasaidia wanachama  wao lakini hata matumizi mbalimbali ya chama hicho ambacho bado kinaonekana kukabiliwa na changamoto nyingi sana
Pia aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa kamwe hawatumiki kwenye siasa za sifa na ushahbiki kwani siasa hizo wakati mwingine zinasababisha hata vifo vya watu ambao hawana hatia ya kufa ovyo
Awali Mgombea Udiwani katika kata hiyo ya Sombetini kwa tiketi ya CCM alisema Bw David Mollel alisema kuwa ana mikakati mingi sana ya kuhakikisha kuwa anasaidia kata hiyo endapo kama atapata ridhaa ya kuongoza rasmi kama diwani
David alisema kuwa changamoto ambazo atahakikisha kuwa ameweza kuzitatua ni pamoja na urekebishaji wa barabara, uboreshaji wa masoko, kna uimarishaji wa vikundi vya wanawake na jamii kwa ujumla.
MWISHO

No comments:

Post a Comment