Saturday, October 26, 2013

SERIKALI YATAKIWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFUGAJI ILI WASIKONDE WAO NA MIFUGO YAO


|Serikali imetakiwa kuboresha mazingira ya wafugaji wan chi ya
Tanzania pamoja na miundombinu yake kwani kwa sasa wapo baadhi ya
wafugaji ambao hawanufaiki na ufugaji na badala yake wanakonda wao
pamoja na mifugo yao

Hayo yameelezwa Jijini hapa na Naibu waziri wa mawasiliano sayansi na
Teknolojia January Makamba wakati akiongea na wataalamu wa mifugo
Tanzania mapema jana kwenye mkutano wa 36 unaondelea jijini hapa.

Makamba alisema kuwa inaskitisha kuona kuwa wafugaji na mifugo yao
imekondeana kwa kuwa haina mazingira mazuri hivyo kuna umuhimu mkubwa
sana wa Serikali kuwekeza kwenye sekta hiyo ambayo bado inakabiliwa na
changamoto kubwa

Alisisitiza kuwa kama mazingira ya wafugaji wa Tanzania yataweza
kuboreshwa kwa asilimia 100 ni wazi kuwa hata mazao yanayotokana na
mifugo nayo yatakuwa ya hali ya juu sana hivyo kuruhusu kuweza kuingia
hata kwenye soko la dunia.

“katika nchi ya Tanzania wapo baadhi ya wafugaji ambao wanafuga
ilimradi waonekane nao wamefuga sasa hili si jambo jema ni muhimu sana
kwa Serikali kuweza kuboresha mazingira na miundombuni lakini pia
kuweza kuwapa misaada muhimu kwa ajili ya kuhimiza uzalishaji na
ufugaji bora zaidi”aliongeza Makamba

Pia alisema kuwa tabia ya kubaki na idadi ya mifugo hususani ngombe
kwenye takwimu za nchi bado haitoshi na wala haijengi bali Nchi
inatakiwa kuwa na takwimu nzuri sana za uzalishaji na ufugaji bora
kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea katika sauala zima la mifugo.

Naye mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa mifugo Tanzania Stella
Bitende alisema kuwa bado kuna umuhimu mkubwa sana wa Serikali
kuhakikisha kuwa hata wananchi wa Vijijini nao wanapata huduma za
wataalamu wa mifugo kwani idadi ya wataalumu hao(Maafisa Ugani)ni
ndogo sana ukilinganisha na uitaji

Bitende aliongeza kuwa kama Serikali itaweza kuongeza idadi ya
wataalumu wa ugani hasa katika maeneo hayo ya vijijini basi ufugaji
utaweza kuwanufaisha wananchi wengi sana tofauti na sasa ambapo katika
maeneo ya vijijini bado wanatumia mbinu na njia za zamani sana

Alimalizia kwa kusema kuwa pamoja na kuwa chama hicho kimeweza
kujipanga hasa katika masuala ya tafiti mbalimbali lakini bado zipo
changamoto kubwa kama vile nyenzo za uzalishaji ,ambazo zinawanyima
kufanikiwa katika uzalishaji kwenye sekta ya mifugo.

MWISHO

No comments:

Post a Comment