Saturday, October 26, 2013

MSIWAACHIE WATOTO UHURU WA UTANDAWAZI NDIO CHANZO CHA KUFELI


Na gadness, Arusha

IMEELEZWA kuwa tabia ya wazazi kuwaachia watoto uhuru wa utandawazi hasa simu za mikononi kwa muda mrefu ndio chanzo kikubwa cha mdonodko wa elimu kwa nchi ya Tanzania kwani kwa sasa wapo baadhi ya wanafunzi ambao wanatumia muda mrefu sana kwenye utandawazi kuliko kwenye elimu

Kwa sasa hata mitandao ya kijamii ambayo ipo inatumiwa wakati mwingine vibaya na wanafunzi hali ambayo wazazi wanatakiwa kuchukulia tahadhari tena kwa haraka sana.

Hayo yameelezwa na Askofu Erick Mukwenda wakati akiongea na wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi wa darasa la saba kwenye shule ya Maranatha iliopo jijini Arusha mapema jana katika maafali ya sita ya shule hiyo.

Askofu huyo alisema kuwa maana halisi ya utandawazi wakati mwingine imegeuzwa kabisa na wanafunzi na hivyo wengi wanadhubutu kuwekeza huko kuliko kuwekeza zaidi kwenye masomo jambo ambalo ni hatari sana

Alisema kuwa ili kuikwepesha jamii na tabia hiyo ni lazima kwanza wazazi waangalie suala hilo kwa mapana zaidi kwani wakati mwingine  watawakemea watoto baasi wataogopa na hawatajihusisha sana na mitandao hiyo au utandawazi

Pia aliongeza nao wazazi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaepukana na tabia ya kufikiria zaidi ada kuliko kufikiria malezi ya watoto kwani kwa sasa walimu pekee ndio wanaoachia suala zima la malezi jambo ambalo wakati mwingine linakuwa gumu sana

“kama tunataka maendeleo ya elimu kwa nchi ya Tanzania ni lazima kwanza tuhakikishe kuwa tunashirikiana kwenye malezi kwani malezi ya wanafunzi sio ada bali hata maadili hivyo basi wazazi sasa mnatakiwa kubadilika”aliongeza Askofu huyo

Katika hatua nyingine aliwataka wazazi pia kuwapa elimu wanafunzi juu ya matumizi ya simu za mkononi lakini pia kuachana na tabia ya kuwapa simu pindi wanapokuwa mashuleni kwani pia jambo hilo pia linachangia sana wanafunzi kuwazia simu kuliko  masomo.

MWISHO

No comments:

Post a Comment