Tuesday, October 1, 2013

MBUNGE LEMA,AFUTIWA MASHITAKA





Na GLADNESS MUSHI, ARUSHA

Mahakama ya hakimu mkazi imefuta kesi iliyokuwa inamkabili mbunge wa jimbo la Arusha Goodbless Lema na kudai kuwa upande wa mashitaka hakuwa na nia ya kuendeleza kesi hiyo.

Aidha kesi hiyo iliyokuwa inamkabili mbunge huyo ilikuwa ni ya uchochezi  katika chuo cha uhasibu Arusha ambapo vurugu hizo zilisababisha chuo hicho kufungwa.

Pia kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo  mbele ya Hakimu Devotha Msofe wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ili kuweza kuitolea ufafanuzi zaidi.

Hataivyio mara baada ya hakimu huyo pamoja na Jopo la mawakili kuingia mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Elianenyi Njiro, aliiomba mahakama kesi hiyo ifutwe chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kama ilivyorekebisha 2002.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa upande wa mashitaka uliona hauna haja wala tija ya kuendelea na kesi hiyo lakini pia ni vema kama kipengele cha sheria kikaangaliwa zaidi.

Pia mara baada ya ombi hilo mahakama iliridhia na kudai kuwa kuanzia sasa Mbunge huyo yupo huru kwa mujibu wa kifungu cha sheria.

Awali Akisoma maelezo ya awali Julai 10 mwaka huu mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Elianenyi alidai Aprili 24 mwaka huu, Lema akiwa eneo la Freedom Square la IAA alifanya kosa la uchochezi wa kutenda kosa kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Akifafanua shtaka hilo, Elianenyi, alidai kuwa Lema aliwaeleza wanafunzi wa chuo hicho ambao walikuwa wamekusanyika kufuatia kuuawa kwa mwenzao na watu wasiojulikana kuwa;

Upande wa mashtaka tayari ulikuwa umewaleta mashahidi watano ambao ni Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Giles Mroto, Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Faraji Kasidi, Inspekta wa Polisi Bernard Nyambalya, Jane Chibuga na Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, John Joseph Nanyaro.

MWISHO

No comments:

Post a Comment