Thursday, April 26, 2012

CHONDE CHONDE ONGEZEKO LA VIJANA MANISPAA YA ARUSHA

MANISPAA YAKABILIWA NA ONGEZEKO LA VIJANA

Na queen lema, arusha

Manispaa ya mkoa wa arusha kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya
ongezeko kubwa la vijana ambapo ongezeko hilo linasababishwa na baadhi
ya vijana wa vijijini kukimbilia mijini kwa ajili ya kutafuta ajira.

Hayo yamebainishwa jana na mkurugenzi wa taasisi ya maendeleo ya
vijana (YDN) Bw Elipokea Urio wakati alipokuwa akiongea na Majira
kuhusu mabadiliko ya maitaji ya vijana kwa mkoa wa arusha hususani
ndani ya halmashauri ya manispaa ya arusha

Bw Elipokea alibainisha kuwa ongezeko hilo ambalo limeongezeka kwa
kipindi cha miaka mitano sasa linasababishwa na matatizo mbalimbali
likiwemo tatizo la hali ngumu ya maisha hasa ya vijijini


Alisema kuwa mwaka 2002 vijana katika manispaa ya arusha kulikuwa na
vijana chini ya laki moja wakati kwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la
vijana laki moja sabini elfu mia tano na hamsini na saba ambapo napo
nusu yao hawana ajira.

“tukijaribu kuangalia sana tunaweza kuona kuwa nusu ya hawa vijana
hawana ajira kutokana na matatizo na changamoto mbalimbali
ukilinganisha manispaa na jiji la arusha ni mji wa kitalii hivyo kuna
umuimu mkubwa wa serikali kuliangalia suala hili kwa undani”aliongeza
Bw Elipokea.

Katika hatua nyingine bw Elipokea alisema kuwa nusu ya vijana hao
ambao hawana ajira kwa sasa wamekosa  ajira kutokana na changamoto
mbalimbali  ambapo changamoto kubwa ni pamoja na vijana kushindwa
kutumia na kutambua fursa mbalimbali zilizomo kwenye ngazi ya
vijiji,kata,na halmashauri

Alisema kuwa kama vijana wa leo wataweza kutambua fursa mbalimbali
ambazo zimo kwenye ngazi hizo basi wataweza kunufaika hata kwa njia ya
mikopo  hali ambayo itaweza kuinua hata kiwango cha maisha.

“katika ngazi ya halmashauri unakuta kwa mfano fedha zimetengwa kwa
ajili ya vijana lakini fedha hizo vijana hawazitumii wala
hawazifuatlii kwa visingizio kuwa sio mali yao basi fedha hizo
zinaenda kwenye matumizi mengine sasa  kwa hali hiyo tatizo la uhaba wa ajira linazidi kuku asana katika jamii”aliongeza bw Elipokea.

Aliwataka vijana wa hususani katika manispaa ya arusha kuhakikisha
kuwa wanajijengea tabia ya kufuatilia fursa mbalimbali ambazo zimo
kwenye ngazi za serikali ikiwa ni pamoja na kutafuta mbinu ya
kujiajiri wao wenyewe ili kuepukana na tatizo la uhaba wa ajira.

MWISHO

chanzo cha habari na Queen Lema,Arusha

0758907891

Arusha

No comments:

Post a Comment