Thursday, April 26, 2012

WATU MILION 45 HATARINI KUPATA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE

JUMLA ya watu milioni 45 duniani hasa waishio katika jamii za kifugaji
wako katika hatari ya kupata magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutokana
na kukithiri kwa changamoto mbalimbali ikiwemo uchafu wa mazingira, na
uhaba wa maji

 Juhudi za kuahakikisha kuwa magonjwa  hayo yanathibitiwa wilaya 75
kati ya wilaya zote nchini  tayari zimeshafikiwa na utekelezaji wa
ugawaji wa madawa  kwa mwaka 2011.

Hayo yalisemwa na mkurugenzi katika huduma za kinga kitengo cha
kutibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele  Dr Peter Mbuji wakati
akifungua  mkutano wa wizara ya afya na ustawi wa jamii uliofanyika
mjini hapa.

Alisema kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele  ni pamoja na
matende,kichocho,usubi trakoma na minyoo ya tumbo ambapo haya  ni
magonjwa ambayo yalikuwepo toka awali na yako nchi nzima  lakini
tayari wizara inatoa dawa na mikakati imetumika ili kuhakikisha kuwa
yanatibiwa.

Alieleza kuwa mkakati na sera za wizara zipo za kuhakikisha kuwa
magonjwa hayo yanathibitiwa na moja ya  mikakati hiyo ni kuhakikisha
kuwa kila kijiji kinakuwa na huduma ya kutoa kinga dhidi ya kuthibiti
magonjwa  hayo.

Kwa upande wake mratibu wa kitaifa wa kuthibiti magonjwa yasiyopewa
kipaumbele kutoka wizara ya afya  Dkt. Upendo Mwingira alisema kuwa
ili  magonjwa hayo yaweze kuteketezwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa
maeneo yote ambayo yana magonjwa hayo yanafanyiwa usafi     kwa kuwa
ndio njia pekee ya kuthibiti.
Aidha alisema kuwa ni vema watu wa mazingira wakahakikisha kuwa elimu
ya usafi wa mazingira inawafikia wananchi ili kuweza kuthibiti
magonjwa hayo.

Pia amefafanua kuwa katika magonjwa hayo matano kila wilaya ina
maambukizi ya magonjwa mawili ambapo wilaya 75 zimeshapatiwa dawa
ambapo hadi ifikapo mwaka 2014 nchi nzima itanufaika na utekelezaji
huo.

Naye mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu( NIMR)dr
Mwele Malechela almesema kuwa taasisi hiyo ina mchango mkubwa kutokana
na juhudi zilizotokana nautafiti ili kutafuta majibu ya kuendesha
mipango kwa ufanisi zaidi.
Alisema kuwa mkutano huo utaangalia jinsi ya kuboresha sera na njia
mbali mbali za kutoa huduma kwa watu wenye ugonjwa wa matende .
mwisho


chanzo cha habari na Queen Lema

0758907891

Arusha

No comments:

Post a Comment