VIJANA 50 WAPEWA ELIMU YA KUTAMBUA SERA NA FURSA KWENYE JAMII
na mwandishi wetu, Arusha
VIJANA zaidi ya 50 kutoka katika kata tano za jiji la Arusha wamefanikiwa kupewa elimu ya matumizi na fursa za sera mbalimbali za nchi ya Tanzania ili waweze kunufaika na sera zilizopo
Aidha mafunzo hayo yametolewa na asasi ya Intiative for youth(INFOY) kwa kushirikiana na asasi ya the Foundation for civil Society yameweza kuwanufaisha vijana kutoka katika kata za Sombetini, Elerai, Sinon, Ngarenaro, pamoja na Sokoni 1huku lengo likiwa ni kujua na kutambua umuhimu wa sera za nchi
Akiongea kwenye mafunzo hayomapema jana mratibu wa asasi ya INFOY Bw Laurent Sabuni alisema kuwa ukosefu wa elimu ya sera umekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa vijana wa sasa
Sabuni alisema kuwa kutokana na ukosefu wa elimu hiyo ya sera umekuwa sababu mojawapo ya vijana kushindwa kutambua fursa mbalimbali ambazo zipo kwenye jamii hali ambayo inachangia umaskini mkubwa kwenye maisha yao
Aliongeza kuwa kwenye mataifa yalioendelea duniani vijana wake huwa wanakuwa na desturi ya kuchambua na kufuatilia sera zao na za nchi jirani hali ambayo inawafanya waibue mambo mbalimbali kwenye jamii
katika hatua nyingine alibainisha kuwa vijana hao 50 ambao wamefanikiiwa kupewa elimu ya kutambua sera na faida zake pia wataweza kuunda mabaraza mbalimbali ambayo nayo yatalenga kuibua fursa za vijana kwenye jamii
Sabuni alidai kuwa kwa sasa ndani ya mkoa wa Arusha hakuna mabaraza ya vijana kitu ambacho wakati mwingine vijana wanakosa sehemu ya kujadilia mambo yao kama ilivyo kwenye nchi ambazo zimeendelea barani Afrika.
Alimalizia kwa kusema kuwa vijana sasa wanatakiwa kujumuika kwenye mabaraza ya kata na hata wilaya na kuachana na tabia ya kukwepa vikundi au umoja kwani umoja unaweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwa nchi ya Tanzania
MWISHO
No comments:
Post a Comment