Tuesday, April 29, 2014

TAASISI ZA FEDHA ZAPEWA CHANGAMOTO

TAASISI  za kifedha zimetakiwa kangalia umuhimu  wa kwawezesha
wakulima  kuwakopesha mikopo kwa kutumia dhamana ya hatimiliki za
kimila ili waweze kulima kilimo cha biashara kwa kuwa ndio dhamana
pekee wakulima waliyo nayo.

Hayo yalisemwa jana  na mkuu  wa wilaya ya arumeru Munasa Nyerembe
alipokuwa akifungua maonyesho ya kilimobiashara ya  kuwaunganisha
wakulima na taasisi  kifedha  yanayofanyika katika viwanja vya AVRDC
tengeru mjini Arusha.

Munasa alisema kuwa asilimia kubwa ya ya wakulima wa vijijini
wanategemea dhamana ya hati miliki za kimila katika kujipatia mikopo
na hivyo taasisi zinapaswa kuhakikisha kuwa zinawawezesha wakulima hao
kwa kuwapatia mokopo ili waweze kuendeleza kilimo chao kiweze kuwa cha
manufaa zaidi.

Alieleza kuwa taasis zinazokataa kukopesha wakulima mikopo kwa kupitia
dhamana ya hati miliki za kimila zinachangia sana kuwanyima wakulima
kutofikia malengo yao ya kilimo cha biashara ambacho ndicho
kinachotegemewa kwa sasa.

Aliongeza kuwa taasisi zozote za kifedha zinazokataa kuwawezesha
wakulima kwa kupitia hati miliki za kimila zinavunja sheria na kwamba
watakaobanika kukataa dhamana hiyo watakchukuliwa hatua za kinidhamu.

“naombeni sana ninyi taasisi za kifedha wapeni wakulima mikopo kwa
kutumia dhamana ya hatimiliki za kimila na ni makosa makubwa sana
kuwanyima mikopo kwa dhamana hii maana ndio dhamana waliyo
nayo”alisistiza

Awali meneja uchumi   benki kuu ya Tanzania tawi la arusha Wilfred
Mbowe akizungumza na wakulima  katika maonyesho  hayo alisema kuwa
benki kuu itaendelea kushirikiana na wakulima kwa kuwapatia mikopo
mbali mbali kwa kuwa ndio benki mama ambayo imezaa taasisi nyinginezo
ambazo zimekuwa bega kwa began a wakulima .

Mbowe alisema benki hiyo itahakikisha kuwa inaendelea kutoa elimu kwa
wakulima na hata pia kusisitizia taasisi nyinginezo umuhimu wa
kushirikiana na wakulima ili kuhakikisha kuwa kilimo cha hapa Tanzania
kinakuwa cha manufaa makubwa zaidi.

Nae mkurugenzi wa chama cha wakulima wa mboga mboga,maua matunda na
viungo(TAHA) Jaqline Mkindi alisema kuwa maonyesho hayo yanachangia
kuwapa wakulima fursa za kuwafanya waweze kukopa katika taasisi za
kifedha kwa kuwa wakulima wengi wameshindwa kufikia malengo ya kilimo
chao kutoka na kukosa mitaji ya biashara.

Alieleza kuwa kupitia maonyesho hayo wakulima watapata elimu na mbinu
ambazo zitawafnya kilimo chao kuwa cha manufaa zaidi huku wakiwa
wanapata hata pembejeo za kilimo chao kwa kupitia taasis hizo ambazo
zitakuwa zinatoa mikopo kwa kupitia dhamana walizo nazo .
mwisho

No comments:

Post a Comment