Wednesday, March 5, 2014

MSIAMBUKIZE VIRUSI KWA MAKUSUDI-RC MULONGO

MKUU WA MKOA WA ARUSHA, MAGESA MULONGO.



mkuu wa mkoa wa Arusha magesa mulongo amewataka baadhi ya wagonjwa
wanaoishi na virusi vya ukimwi kuhakikisha kuwa wanaishi kwa kufauta
masharti ya wataalamu wa afya lakini pia kuachana  na dhana ya
kuambukiza magonjwa hayo kwa makusudi hasa kwa wale ambao bado hawana
maambukizi

mulongo aliyasema hayo wakati akiongea kwenye uzinduzi wa chanjo kwa
kina mama wajawazito mpango ambao unatekelezwa chini ya Shirika la
Egpaf

Alidai kuwa kwa sasa wapo baadhi ya wagonjwa ambao wanatumia mwanya
huo kuwajerui wale ambao hawana ugonjwa jambo ambalo sio jema kwenye
jamii

alifafanua kuwa wagonjwa hao wanapaswa kuhakikisha kuwa wanafuta
taratibu za wataalamu wa afya lakini pia wahakikishe kuwa kamwe
hawaongezi idadi ya wagonjwa zaidi

"jamani ni lazima tufike mahali tuwe na tabia ya uzalendo lakini pia
tuhakikishe kuwa tunajiengua kwa kusababisha mtikisiko kwenye taifa
kwa ajili ya makusudi tuawalinde wale ambao hawana na wala makusudi
kamwe hayawezi kutusaidia sisi bali yanachangia sana
kutuangamiza"aliongeza Mulongo

Naye mganga mkuu wa mkoa wa arusha Frida Mokiti alisema kuwa pamoja na
jitiada mbalimbali ambazo zinaendelea kufanyika lakini bado kasi ya
maambukizi kwa mkoa wa Arusha ipo juu sana.

Mokiti alifafanua kuwa mkoa umeweza kuweka mikakati mbalimbali ya
kupambana na ugonjwa huo ingawaje nao wagonjwa nao wanatakiwa
kuepukana na kusambaza kwa makusudi bali wanatakiwa kuchukua tahadhari
tena kwa haraka sana.

No comments:

Post a Comment