Saturday, August 11, 2012

KITUO CHA UTAFITI WA MAZAO CHASHINDWA KUFIKISHA TEKNLOJIA 30 KWA WAKULIMA KWA UKOSEFU WA FEDHA


KITUO CHA UTAFITI WA MAZAO CHASHINDWA KUFIKISHA TEKNLOJIA 30 KWA WAKULIMA KWA UKOSEFU WA FEDHA

KITUO cha Utafiti wa mazao ya kilimo kanda ya kaskazini(SARI) kimeshindwa kufilkisha teknolojia mpya  thelathini kwa wakulima kwa zaidi ya miaka minne mfululizo kutokana na kukabiliwa na uhaba wa Fedha hali ambayo inafanya malengo mbalimbali ya Kilimo kwanza kufikiwa

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mkuu wa Kituo hicho Dkt Mboya Mgendi wakati akiongea na mkuu wa mkoa wa Arusha bw Magesa Mulongo ndani ya viwanja vya Taso Nane Nane Mjini wakati alipotembelea banda la Kituo hicho

Dkt Mgendi alisema kuwa kwa Muda mrefu Serikali imekisahau kituo hicho huku kituo hicho kikiwa ni moja ya vituo ambavyo vinahudumia Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, na Tanga ambapo pia mikoa hiyo ni Mikoa ambayo inaitaji msaada mkubwa sana katika kuimarisha shuguli za kilimo hasa vijijini

Alisema kuwa hapo awali Kituo hicho kilikuwa ni moja ya vituo ambavyo vilikuwa vinamsaidia sana mkulima hasa wa chini na wa kijijini na matunda yake yaliweza kuonekana katika uzalishaji na ukulima tofauti na sasa ambapo baadhi ya Vijiji vinashindwa kufikiwa kutokana na uhaba wa fedha ambao umedumu katika kituo hicho kwa miaka minne sasa.

“tunasikitika sana kwa kuwa tuna buni teknolijia kila siku tena teknolojia ambazo ni mpya kabisa kisha zinashindwa kuwafikia walengwa kwa kuwa tunafikaje ni lazima fedha itumike kusafirisha hata hawa wataalamu, na kutokana na hilo tunabaki na hizi teknolojia wakati walengwa wa hizi teknolojia ni wananchi tena wa  chini sasa Serikali inatakiwa kuliangalia suala hili kwa undani sana ili kuweza kuboresha zaidi Kilimo kwanza”alionngeza Dkt Mgendi.


Aidha Dkt Mgendi alisema kuwa kutokana na hali hiyo imesababisha malengo mbalimbali ambayo yanakusudiwa na kituo hicho kushindwa kufikiwa huku  Serikali nayo ikilia na kuweka Mikakati mbalimbali juu ya Kilimo kwanza hali ambayo kama ingetumika kwa kuwawezesha wataalamu mbalimbali  wa kituo hicho basi Kilimo hasa kwa mikoa ya Kaskazini ingeboreka zaidi.


Pia aliiomba Serikali kuhakikisha kuwa inaangalia kwa undani sana umuhimu wa kituo hicho hassa kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambapo kuna changamoto kubwa sana ya Matumizi sahihi ya  utafiti  wa kilimo, Mbegu bora za kilimo,pamoja na dhana ambazo bado wakulima wanaitaji elimu zaidi kutoka kwa wataalamu hao  wa kilimo bora.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha bw Magesa Mulongo alisema kuwa Kituo hicho kina umuhimu mkubwa sana hasa kwenye Kilimo kwanza na Changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili kituo hicho zitasikilizwa ili kuendelea kuimarisha zoezi zima la Kilimo kwanza hasa kwa Mkoa wa Arusha ambao bado unaitaji sana nguvu ya watalaamu wa Kilimo bora

“Nitakuja katika kituo chenu cha utafiti tutaongea ili tuweze kuona juu ya hili suala ambalo limeongelewa hapa ingawaje na kituo hiki kinatakiwa kuhakikisha kuwa kila kitu ambacho wanakizalisha kinatakiwa kuwepo kwenye mitaa yote ya kanda ya kaskazini ili kuboresha Kilimo kwanza ndani ya Mikoa hiyo husika”aliongeza Bw Mulongo.


MWISHO

No comments:

Post a Comment