Monday, January 2, 2012

CHANGAMOTO ZA MWAKA 2011 ZISIWAFANYE MKATEE TAMAA-MCHUNGAJI VOMO



IMEELEZWA kuwa pamoja na nchi kukabiliwa na majanga na changamoto mbalimbali hasa kwa mwaka 2011 wakristo hawapaswi kukata tamaa juu ya changamoto hizo bali wanatakiwa kuangalia imani na maitaji ya Mungu Kwa mwanadamu ili aweze kupunguza na kuondoa changamoto hizo.

Hayo yameelezwa mjini hapa na mchungaji Simion Vomo wakati akiongea na waumini wa kanisa la T.A.G Chrstian all  nation church lilopo katika manispaa ya mji wa arusha mapema wiki hii.

Aidha mchungaji Vomo alisema kuwa katika mwaka 2011 mambo mengi sana yalijitokeza hali ambayo iliwapelekea baadhi ya waumini kukata tamaa lakini katika mwaka huu mpya wa 2012 wanapaswa kumuangalia mungu zaidi kuliko matatizo yao binasi.

Alibainisha kuwa hata katika matatizo mungu yupo na kwa hali hiyo kila mwanadamu anapaswa kuangalia mpango na mikakati mbalimbali ya mungu na kuachana na tabia ya kuona wameshindwa mbele ya Macho ya wanadamu

“maandiko yanasema kuwa mwanadamu ataona yameshindikana lakini Mungu hatashindwa na pale Mwanadamu anapoonekana kuwa ameshindwa ndipo mungu anapoonekana kuwa anaweza nawasihi sana tuangalie imani zetu kwa kuwa ndicho chanzo pekee cha kufanikiwa’alieleza Bw Vomo.

Awali alisema kuwa nao waliofanikiwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatangaza zaidi utukufu wa mungu kuliko mafanikio yao kwa kuwa ndicho chanzo pekee cha kufanikiwa katika maitaji mbalimbali ambayo yanamzunguka mwanadamu wa leo.

Alibainisha kuwa endapo kama wataweza kufanya hivyo ni wazi kuwa mafanikio yatakuwa ni makubwa sana ukilinganisha na mafanikio ambayo hayana utukufu wowote hapa duniani.

“Mungu ana makusudi na kila mmoja wetu na kwa hali hiyo mungu anapswa kupewa utukufu kwa kila jambo hata kama ni dogo kwa kuwa yeye ndiye anayetutoa kutoka ushindi kwenda ushindi, na kwa maana hiyo hatupaswi kukata tama wala kuangalia masuala ya mambo ya hapa duniani tukasahau ya Mungu Wetu”alisema Mchungaji Vomo.


Alimalizia kwa kusema kuwa kwa wale ambao hawajafanikiwa kwa msimu wa mwaka uliopita wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaongeza kiwango cha imani katika maisha yao kwa kuwa Pia Mungu anapenda na kuthamini zaidi Mtu mwenye Imani.

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA
ARUSHA 

O758907891

No comments:

Post a Comment