Monday, January 2, 2012

ASKOFU URIO-WAKRISTO MSIWATEGEMEE ZAIDI WATABIRI TEGEMEENI BIBLIA



Askofu Fitiaely Urio wa makanisa ya Pentekoste Gospel Assemblies church ya mjini hapa amewataka wakristo kuhakikisha kuwa wanatumia zaidi maono ya kibiblia na wala sio maono ya tabiri kutoka kwa watu wanaotabiri kwa kuwa tabiri hizo zinachangia sana wengi wa wakristo kushindwa kukua kiroho na kiimani

Askofu Urio aliyasema hayo wakati wa ibada maalumu ya kuombea mwaka 2012 iliyofanyika katika kanisa la Usa Magadini wilayani Meru mkoani hapa.

Hataivyo Askofu Urio alisema kuwa wakristo wanapswa kuhakikisha kuwa wanatumia zaidi karama mbalimbali ikiwemo karama ya Roho mtakatifu na kuachana na tabia ya kupendelea zaidi Tabiri ambazo zinalenga kuwakatisha moyo.

Alisema kuwa endapo kama watatumia zaidi biblia kama mwongozo kwa mwaka 2012 ni wazi kuwa wataweza kufikia malengo yao mbalimbali ambayo walijiwekea na hata kufanya mabadiliko mbalimbali ambayo yatakuwa na faida kwa jamii na vizazi vyao.

“jamani hakikisheni kuwa mnaacha tabia ya kufuatilia tabiri mbalimbali ambazo zinatolewa hapa nchini juu ya mambo ya mwaka jiulieze biblia inatabiri mema na wao wanatabiri mabaya sasa nini maana yake mkabidhi mungu mizigo yako yote na yeye ataitatua”alisema Askofu Urio

Pia alianisha kuwa mbali na kutegemea zaidi tabiri mbalimbali kutoka kwa wanatabiri pia wapo baadhi ya wakristo katika jamii ambao kamwe hawaridhiki na neema ya mungu ambayo wanapewa hata kama ni kidogo na badala yake wanaanza kutoa malalamiko na lawama mbalimbali.

Alisema kuwa tabia hiyo haimfurashi mungu kwa kuwa mungu ndiye anayetoa na hivyo mungu anaanagalia zaidi kiwango cha imani ambacho mtu anacho hivyo kila mwenye tabia hiyo anapaswa kuacha mara moja ili afungulie zaidi baraka na Mafanikio katika Maisha yake.

“hili si jambo jema hata kidogo mjue mungu anapenda sana kurudishiwa shukurani sasa wewe unapopata halafu hutoi shukurani manaake ni nini asiye shukuru kwa kidogo hata kikubwa hataweza kushukuru hivyo nawasihi hakikisheni kuwa hamuendekezi hii tabia kwani ni mbaya sana’aliongeza Askofu Urio.

Alihitimisha kwa kusema kuwa wanadamu hawapaswi kuangalia kushindwa kwao katika mambo mbalimbali ambayo yanawakabili bali hata katika furaha na shida wanatakiwa kumuita mungu kwa kuwa ndiye kimbilio la kila mtu.

MWISHO

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA
ARUSHA 

0758 9078 91

No comments:

Post a Comment