Monday, December 19, 2011

WENYE WIVU NDIO CHANZO KIKUU CHA MASENGENYO- ASKOFU HOTAY


Baadhi ya wakristo wenye wivu wametakiwa kuacha tabia hiyo kwa kuwa ni chanzo mojawapo cha kuzalisha mawazo ya mtu baki ndani ya mioyo ya watu hali ambayo kwa upande mwingine inazaa dhambi ya wivu

Mtu anapokuwa na tabia ya wivu ni lazima kwanza aweze  kuwa na tabia ya kutopendena kati ya mtu na mtu na hali hiyo ndiyo pia inayozaa matatizo makubwa sana ndani ya jamii

Hayo yamebainishwa mjini hapa katika kanisa la Anglican  St James kaloleni na askofu wa kanisa hilo bw Stanley Hotay wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo mapema wiki hii katika ibada ya kuwabariki watoto

Askofu Hotay alisema kuwa ni vibaya sana kama mkristo aliye hai akiwa na tabia ya masengenyo ambayo ni mtoto wa wivu kwa kuwa hali hiyo ni chukizo kubwa sana mbele za mungu.

Aliongeza kuwa ndani ya dunia ya sasa hakuna kitu chochote kile ambacho kitaweza kufanyika na kufanikiwa kama mkristo atakuwa na tabia za wivu kwa kuwa Mungu ndiye anayegawa vitu.

“hii tabia ya wivu kimsingi imetambaa miongoni mwa watu sana unakuta mtu anafikiria mambo ya mwezake na anacha kufikiria mambo yake sasa kwa hali hii kwa nini shetani asiwe ni kikwazo kwetu jamani nawasihii sana achaneni na dhambi hiyo ya wivu rudini katika utukufu wa bwana”alisema Askofu Hotay

Pia katika hatua nyingine alisema kuwa kamwe wivu hauna nafasi katika maisha ya mwanadamu endapo kama mwanadamu atajiwekea utaratibu wa kusikiliza na kuongozwa na sauti ya roho mtakatifu

Alibainisha kuwa endapo wakristo wote watakuwa na tabia ya kumtumia zaidi roho mtakatifu katika mambo yao mbalimbali ni wazi kuwa roho ambazo kwa sasa zinatembea kwa baadhi ya watu zitaweza kufa kabisa .

Hataivyo katika ibada hiyo ambayo iliweza kuwakusanya wakristo wengi sana iliweza kuwa na manufaa makubwa sana kutokana na  kuwepo kwa mambo mbalimbali wakiwemo walemavu wa ngozi(ALBINO) pamoja na kubariki watoto 80.

MWISHO
CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA

No comments:

Post a Comment