UKOSEFU WA VYOO WASABABISHA WANAFUNZI ZAIDI YA 300
KUJISAIDIA VICHAKANI
ZAIDI ya wanafunzi 300 kutoka katika shule ya msingi
Engatani iliopo Kata ya MakibaWilayani Meru Mkoani Arusha wapo hatarini kupata
magonjwa ya mlipuko kutokana na kuwa shule hiyo haina vyoo na hivyo wanafunzi
wa shule hiyo wanalazimika kujisaidia kwenye vichaka.
Aidha tatizo hilo
la ukosefu wa vyoo katika shule hiyo umedumu kwa miaka miwili sasa mara baada
ya mvua kubwa kufukia matundu ya vyoo katika shule hiyo.
Akiongea na “majira “shuleni hapo mapema jana Mkuu wa shule
hiyo Adamu Kapaya alisema kuwa shule hiyo haina vyoo kabisa na hivyo wanafunzi
wanapojisikia kujisaidia wanalazmika kwenda kwenye vichaka au kwenye mazingira
ambayo yamejificha kwaajili ya kuweza kujisaidia
Alidai tatizo hilo limeanza
mwaka 2012 ambapo mvua kubwa ya masika ilionyesha iliweza kuziba matundu ya
vyoo na hivyo kusababisha kutitia kwa vyoo hivyo na mpaka sasa hakuna huduma ya
vyoo hali ambayo imesababisha madhara makubwa sana kutokea katika shule hiyo.
“baada ya kuona kuwa mvua zimesababisha shule yetu kukosa
vyoo niliandika barua kwa mkurugenzi ambapo naye alihaidi kushugulikia tatizo
hili na kwa uongozi wa serikali ya kijiji nlakini mpaka sasa hali ndio kama hii hakuna choo wanafunzi wanakimbilia zaidi kwenye
Vichaka”alisema Adamu
Pia aliongeza kutokana na hali hiyo imesababisha hata
mazingira ya shule kuwa machafu sana pamoja na
kuwepo kwa hewa chafu kutokana na vinyesi ambavyo vimezagaa kwenye mazingira ya
shule hiyo na pembezoni mwa shule hiyo hivyo jitiada za haraka sana zinatakiwa kufanyika
Awali diwani Viti maalumu wa Kata hiyo ya Makiba.Bi Joycye
Odoko alisema kuwa ukosefu wa choo kwenye shule hiyo umesababishwa na baadhi ya
watendaji kukwepa kuombea bajeti shule hiyo kwa lkuwa ipo mpakani mwa wilaya ya
Meru hali ambayo inasababisha wanafunzi waishi mazingira magumu sana
Bi Joyce amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi katika eneo
hilo ni wafugaaji lakini hawana uwezo kitu
ambacho kama wangekuwa na uwezo basi wangeweza
kuwasaidia wanafunzi hao
“wananchi wa hapa hawana uwezo ingawaje kwa sasa wameshaweka
utartibu hata wa kukusanya mawe , na mchanga ili kuuanza rasmi zoezi hilo
japokuwa bado hawataaweza kujenga mpaka kumalizika kwa matundu ya vyoo sassa
tunaomba kuwepo naushirikiano madhubuti
baina yetu sisi viongozi ili tuweze kuwasaidia wanafunzi hawa kwani wapo
kwwenye hatari kubwa sana ya kuweza kupata magonjwa ya mlipuko hasa
kipindupindu”aliongeza Jocye
Akiongelea sakata hilo kwenye
baraza la madiwani wa halmahauri ya Meru Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye Goodson Majola alisema kuwa kwa
sasa bajeti ya Halmashauri hiyo imelenga kutatua sehemu mbalimbali zenye kero
na hivyo pindi watakapopata fedha kutoka Serikali kuu basi wataweza kutatua
changamoto mbalimbali
No comments:
Post a Comment