Wednesday, January 30, 2013

TANZANIA INAKABILIWA NA MAFUNDI SANIFU MAABARA-MULUGO



TANZANIA INAKABILIWA NA MAFUNDI SANIFU MAABARA-MULUGO

TANZANIA inakabaliwa na tatizo la uhaba wa  mafundi Sanifu Maabara ambapo kwa sasa wanaozalishwa na Vyuo vya Ufundi hapa nchini hasa Arusha Techical College(ATC)ni ndogo sana hali ambayo inafanya baadhi ya shule za Sekondari hapa nchini kukosa ufanisi zaidi na Masomo ya Sayansi

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa elimu na Ufundi hapa Nchini Bw Philiph Mulugo wakati akiongea na wadau mbalimbali wa chuo cha ufundi Arusha(ATC)mapema wiki hii

Aidha Mulugo alisema kuwa bado hali si shwari hasa katika sekta hiyo ya mafundi sanifu wa maabara kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi yenye shule za Sekondari zaidi ya 400 wakati wanaozalishwa wakiwa bado ni 15

Alisema kuwa hali hiyo inasababisha kuwepo na uhitaji mkubwa sana wa mafundi sanifu kwa kuwa ili shule yoyote ile iweze kufanya vema katika masomo ya Sayansi ni lazima kwanza wataalamu hao waweze kuandaa vifaa mbalimbali vya maabara ili kuruhusu wanafunzi wasome vizuri

“hapa unaweza kuona kuwa wahitimu  wa hii fani wachache sana kuliko wahitimu wa darasa la saba ambao wanatarajia sasa rasmi kuanza rasmi masomo ya Sayansi sasa kwa hali hii hata wale walimu wa masomo haya kwa kweli wanazidiwa sana na majukumu lakini kama watakuwa na wataalamu wa kutosha tunaamini kabisa  ufaulu wa masomo haya utaongezeka sana hivyo Serikali itaondokana  hata na uhaba wa wataalamu mbalimbali”aliongeza Mulugo

Mulugo pia alisema kuwa pamoja na uhaba huo wa mafundi sanifu wa maabara lakini lengo la Serikali la sasa ni kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na  Wataalamu hao ambao wataweza kushirikiana na walimu wa Sayansi hivi karibuni ambapo pia hata Vyuo vya ufundi navyo vinatakiwa kuhakikisha kuwa vinajiwekea utaratibu wa kuzalisha wataalamu wengi zaidi

Alitoa wito kwa vijana wa Kitanzania kuhakikisha kuwa kamwe hawakimbii fani hiyo badala yake wajiunge na Chuo hicho cha  Ufundi Arusha ili waweze kudahiliwa kama wataalamu  ambapo hali hiyo itaweza kuokoa Jamii ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalamu hao

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt Richard Masika alisema kuwa kwa sasa Jamii inaona Masomo ya Sayansi ni Magumu kwa kuwa hakuna utaratibu wa kuyafundisha kwa vitendo jambo ambalo kwa sasa chuo hicho kimejipanga sana kuweza kujipanga kudahili wahitimu wengi zaidi ili kufanya masomo hayo yasionekane ni magumu

Dkt Masika alisema kuwa ili masomo hayo yasionekane kuwa ni magumu kwa sasa wamejiopanga kwa kuhakikisha kuwa wanazalisha wataalamu wengi zaidi ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 watakuwa wamezalisha wataalamu zaidi ya 150 ambao wataweza kusaidia sana kuokoa shule zenye uhaba wa watalaamu hao

MWISHO

TANZANIA INAKABILIWA NA MAFUNDI SANIFU MAABARA-MULUGO



TANZANIA INAKABILIWA NA MAFUNDI SANIFU MAABARA-MULUGO

TANZANIA inakabaliwa na tatizo la uhaba wa  mafundi Sanifu Maabara ambapo kwa sasa wanaozalishwa na Vyuo vya Ufundi hapa nchini hasa Arusha Techical College(ATC)ni ndogo sana hali ambayo inafanya baadhi ya shule za Sekondari hapa nchini kukosa ufanisi zaidi na Masomo ya Sayansi

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa elimu na Ufundi hapa Nchini Bw Philiph Mulugo wakati akiongea na wadau mbalimbali wa chuo cha ufundi Arusha(ATC)mapema wiki hii

Aidha Mulugo alisema kuwa bado hali si shwari hasa katika sekta hiyo ya mafundi sanifu wa maabara kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi yenye shule za Sekondari zaidi ya 400 wakati wanaozalishwa wakiwa bado ni 15

Alisema kuwa hali hiyo inasababisha kuwepo na uhitaji mkubwa sana wa mafundi sanifu kwa kuwa ili shule yoyote ile iweze kufanya vema katika masomo ya Sayansi ni lazima kwanza wataalamu hao waweze kuandaa vifaa mbalimbali vya maabara ili kuruhusu wanafunzi wasome vizuri

“hapa unaweza kuona kuwa wahitimu  wa hii fani wachache sana kuliko wahitimu wa darasa la saba ambao wanatarajia sasa rasmi kuanza rasmi masomo ya Sayansi sasa kwa hali hii hata wale walimu wa masomo haya kwa kweli wanazidiwa sana na majukumu lakini kama watakuwa na wataalamu wa kutosha tunaamini kabisa  ufaulu wa masomo haya utaongezeka sana hivyo Serikali itaondokana  hata na uhaba wa wataalamu mbalimbali”aliongeza Mulugo

Mulugo pia alisema kuwa pamoja na uhaba huo wa mafundi sanifu wa maabara lakini lengo la Serikali la sasa ni kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na  Wataalamu hao ambao wataweza kushirikiana na walimu wa Sayansi hivi karibuni ambapo pia hata Vyuo vya ufundi navyo vinatakiwa kuhakikisha kuwa vinajiwekea utaratibu wa kuzalisha wataalamu wengi zaidi

Alitoa wito kwa vijana wa Kitanzania kuhakikisha kuwa kamwe hawakimbii fani hiyo badala yake wajiunge na Chuo hicho cha  Ufundi Arusha ili waweze kudahiliwa kama wataalamu  ambapo hali hiyo itaweza kuokoa Jamii ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalamu hao

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt Richard Masika alisema kuwa kwa sasa Jamii inaona Masomo ya Sayansi ni Magumu kwa kuwa hakuna utaratibu wa kuyafundisha kwa vitendo jambo ambalo kwa sasa chuo hicho kimejipanga sana kuweza kujipanga kudahili wahitimu wengi zaidi ili kufanya masomo hayo yasionekane ni magumu

Dkt Masika alisema kuwa ili masomo hayo yasionekane kuwa ni magumu kwa sasa wamejiopanga kwa kuhakikisha kuwa wanazalisha wataalamu wengi zaidi ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 watakuwa wamezalisha wataalamu zaidi ya 150 ambao wataweza kusaidia sana kuokoa shule zenye uhaba wa watalaamu hao

MWISHO

WATOTO WA KIKE WAKIPEWA MOYO NA MOTISHA WANA UWEZO WA KUSHIKA NAFASI ZA JUU KATIKA MITHIANI YA KITAIFA





WATOTO WA KIKE WAKIPEWA MOYO NA MOTISHA WANA UWEZO WA KUSHIKA NAFASI ZA JUU KATIKA MITHIANI YA KITAIFA

,Arusha

IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya watoto wa kike wanashindwa kufanya vema katika mithiani ya mwisho pamoja na masomo ya Sayansi kwa kuwa wanakatishwa tamaa na jamii zao hasa walimu na wazazi

Watoto wa kike wana uwezo mkubwa sana wa kufanya vema na kushika nafasi za juu katika masomo na mithiani yao lakini kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya kukatishwa tamaa hali ambayo inawafanya washuke Kitaaluma

Hayo yameelezwa na Mwanafunzi bora  katika  Mthiani wa darasa la saba  mkoa wa Arusha, na Wilaya ya Arusha Vijijini,Pricilla Calvin Marealle wakati akiongea na Majira mapema jana kuhusu kiwango cha Ufaulu wa watoto wa kike kwa mkoa wa Arusha

Alisema kuwa watoto wa kike wana uwezo mkubwa sana wa kufanya vema katika mithiani yao ya Mwisho na hivyo kushika nafasi ya juu Kitaifa endapo kama mfumo ambao upo katika baadhi ya familia na Shule utabadilika

Akielelezea mfumo huo ambao unasababisha wanafunzi wa kike kushindwa kufanya vema ni pamoja na kukatishwa tamaa hasa katika masomo ya Sayansi na hivyo wanafunzi wa kike kuishia kuambiwa kuwa masomo ya Sayansi ni masomo ya wanafunzi wa Kike hali ambayo nayo inachangia sana wanafunzi kubweteka sana

Aliongeza kuwa mfumo mwingine mbaya ambao unasababisha kwa kiwango cha juu sana wanafunzi wa kike kushindwa kufanya vema katika masomo yao ni pamoja na wazazi, na walimu kukaa mbali na wanafunzi wao na hivyo kushindwa kuwapa moyo wa kufaulu huku wazazi wakiona jukumu hilo ni kwa ajili ya walimu na walimu wakiona kuwa jukumu hilo ni kwa ajili ya wazazi hali ambayo inawafanya watoto wa kike kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea

“Mimi naweza kusema kuwa nimekuwa mtoto wa pili Kimkoa na wa Kwanza kimkoa kwa kuwa walimu wangu na wazazi na ndugu zangu walikuwa wanafuatilia maendeleo yangu tangu nilipokuwa madarasa ya awali na pale nilipoanguka walitafuta chanzo  na kunipa moyo na motisha mbalimbali ndio maana niliweza kufika hapa na hivyo wazazi na walezi wanatakiwa kujifunza juu ya suala hili kama wanataka wanafunzi waweze kufaulu”alisema Pricilla

Awali alitoa wito kwa Serikali nayo kuhakikisha kuwa wanaboresha zaidi shule za Kata hasa upande wa Maabara ambapo kwa sasa napo kuna changamoto Lukuki ndani ya shule hizo hali ambayo inafanya hata wakati mwingine wanafunzi wa shule za Kata kuonekana kama ni watoto wa maskini kutokana na uhaba wa vifaa vya kujifunzia.

MWISHO

CCM MERU WATAKELEZA AHADI ZA CHADEMA




CCM MERU WATAKELEZA AHADI ZA CHADEMA

Na Queen Lema,Meru

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Chama cha Mapinduzi  Wilaya ya Meru(CCM) kimetekeleza ahadi iliyotolewa na Viongozi wa Kitaifa wa chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kupitia kwa Mbunge wa jimbo hilo Joshua Nassari, ambapo viongozi hao walitoa ahadi ya kuchimba Visima 11ndani ya siku 90 katika Kata ya Maroroni kijiji cha Samaria lakini ahadi haijatekelezwa

Akiongea na Vyombo vya habari mapema jana Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Meru,Furaini Mungure alisema kuwa Viongozi wa Chadema ambao ni Dkt Slaa,Ndesamburo, na Mbowe walitoa ahadi hizo wakati walipochukua jimbo la Meru Mashariki lakini hawakutekeleza ahadi hiyo ambayo ikuwa inadai kuwa watapeleka na kwenda kuchimba Visima 11 katika eneo Samaria Wilayani Meru

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo Ccm imeona kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi hiyo ambayo walikuwa wameahidiwa wananchi lakini bado haijatekelezwa hali ambayo inasababisha madhara makubwa sana  kutokana na ukame uliokithiri ndani ya maeneo hayo

Alifafanua kuwa pamoja na kuwa Viongozi hao wa Chadema wametoa ahadi hiyo ya uchimbaji wa Visima lakini Ccm imeweza kufanikisha na kutekeleza ilani yake ambayo inasema na kudai kutekeleza mahitaji mbalimbali ya wananchi ambayo  kama hayatatekelezwa chanzo chake ni umaskini uliokithiri sana

“ahadi ilitolewa na Chadema na ilikuwa itekelezwe ndani ya siku 90 mara baada ya Mbunge wao kupewa madaraka na wanananchi haikutekelezwa lakini Sisi Ccm Tumetekeleza tena kwa kiwango cha hali ya juu sana ambapo shida kubwa ya wananchi wa maeneo hayo ilikuwa ni uhaba wa maji sasa sisi kwa kushririkiana na Halmashauri ya Meru  tumeweza kumaliza mchakato huo visima “aliongeza

Akielezea Utekelezaji wa Ahadi hiyo ya Visima 11 ambayo ilitolewa na Chadema alisema kuwa Ccm tayari imeshakamilisha mchakato wa kupeleka maji katika kijiji cha Samaria, ambapo mpaka kufikia mwezi wa tatu wananchi hao watapata maji

Mungure alibainisha kuwa Chama chake kitajenga Tanki la maji lenye ujazo wa lita elfu hamsini ambapo wananchi hao wataweza kupata maji kwa uraisi sana tofauti na sasa ambapo wanalazimika kutembea Umbali mrefu sana kutafuta maji

Mbali na hayo alisema kuwa  nao viongozi wa Ccm hawatakiwi kukaa maofisini na badala yake wanatakiwa kwenda kwenye jamii na kuangalia jinsi ya kutatua changamoto ambazo zinaikabili ili kuweza kutekeleza ilani ya Chama hicho.

MWISHO

POLISI ARUSHA WAKUSANYA BILIONI 1.2 KUTOKANA NA MAKOSA MBALIMBALI



POLISI ARUSHA WAKUSANYA BILIONI 1.2 KUTOKANA NA MAKOSA MBALIMBALI


Na Queen Lema,Arusha

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limefanikiwa kukusanya kiasi cha Bilioni 1.2 kwa mwaka 2012 ambapo mwaka jana jeshi hilo lilikusanya zaidi ya  Milioni  518  kutokana na makosa mbalimbali ambayo yanatozwa mara baada ya wananchi kuvunja sheria za Jeshi hilo

Akiongea na “MALKIA WA MATUKIO”jana kuhusuniana na mapato ya jeshi hilo kwa mkoa wa Arusha kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kuwa kuongezeka kwa fedha hizo kunatokana na jitiada mbalimbali za jeshi hilo za kupambana na uhalifu.

Sabas alisema kuwa mbali na jeshi hilo kuweza kupambana na uhalifu hivyo kukusanya kiwango kikubwa sana cha fedha  lakini hata uhalifu wenyewe, ajali za barabarani nazo zimepungua  tofauti na miaka ya nyuma kutokana na jitiada ambazo zinafanywa na Polisi

Aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2011 matukio ya ajali za barabarani yalikuwa ni 2507 wakati mwaka 2012 matukio yatokanayo na ajali yalikuwa ni 2106 sawa na upungugu wa asilimia 16

Akiendelea kuelezea pia alisema kuwa hata  matukio ya vifo vitokanavyo na ajali navyo vimepungua kwa kiwango cha hali ya juu sana ambapo  kwa mwaka 2011 matukio yalikuwa 211 huku 2012 yalikuwa ni 175 sawa na upungufu wa asilimia 17 ambapo hali hiyo imetokana na Jitiada mbalimbali ambazo zinatokana na Jeshi hilo

Mbali na hayo pia makosa ya barabarani ambayo yamelipiwa nayo yamechangia sana kuinua pato letu la mwaka ambapo yalikuwa ni zaidi ya elfu 42 kwa mwaka 2012 tofauti na mwaka 2011 ambapo makosa hayo yalikuwa ni 1978 sawa na ongezeko la makosa ya barababarani yaliyolipiwa kwa asilimia 119


“Unaweza kuona matukio yamepungua kwa asilimia kubwa sana lakini pia hata mapato yetu nayo yameongezeka sana hivyo basi bado tunakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha kuwa masuala ya uvunjwaji wa sheria yanakwama kabisa ndani ya mkoa wa Arusha kwani uwezekano upo na pia kama tutafanya hivyo tutaongeza mapato lakini tutaokoa maisha ya Watu wa Arusha”aliongeza Sabas

Kutokana na hali hiyo Kamanda Sabas aliwataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanakuwa walindaji wazuri wa sheria za nchi na wala sio wavunjaji wazuri wa sheria za Nchi kwani uvunjwaji wa sheria za nchi ndio chanzo cha vifo ,Umaskini pamoja na Migogoro mikubwa sana ndani ya jamii.

MWISHO

Monday, January 28, 2013

ARUSHA KUZINDUA KAMPENI YA USAFI FEBRUARY MOS,ATAKAYECHAFUA MAZINGIRA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

ARUSHA KUZINDUA KAMPENI YA USAFI FEBRUARY MOS,ATAKAYECHAFUA MAZINGIRA KUFIKISHWA MAHAKAMANI


Na Queen Lema,Arusha

Uongozi wa Jiji la Arusha kwa kushirikiana na kamati ya usafi wa Jiji linatarajia kuzindua Kampeni ya usafi wa jiji ambapo kampeni hiyo itaenda sanjari na utozwaji wa faini kwa wachafuzi wa mazingira

Akiongea na Vyombo vya habari mapema leo mwenyekiti wa kamati ya mazingira Jiji la Arusha,Adolph Ulomi alisema kuwa uzinduzi huo utafanyika FebruaryMosi na utashirikisha wananchi wote

Aidha Ulomi alisema kuwa Umoja ambao umeundwa baina ya jiji na kamati hiyo utaweza kuwasaidia kusafisha Jiji la Arusha ambapo kwa sasa kuna changamoto kubwa sana ya uchafuzi wa mazingira

Alisema kuwa kupitia Kamati hiyo ya usafi wa mazingira ambayo inaanza kampeni zake February Mosi itaweza kuhamiashisha shuguli mbalimbali za usafi sanjari na kutoa,kuratibu,vifaa mbalimbali vya usafi ambavyo  hapo awali havikuwepo

‘Tumeamua kufanya mji wa Arusha kuwa na mabadiliko ya hali ya juu sana ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hadhi ya jiji inarudi mahala pake hivyo February Mosi tutaanza kazi rasmi ndani ya jiji na tunatarajia kampeni hizi zizinduliwe rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha”alisema Ulomi

Katika hatua nyingine alisema kuwa kupitia kamati hiyo ya usafi wa Jiji la Arusha pia wataweza kusimamia sheria na kanuni  mbalimbali za usafi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanaovunja sheria za usafi wanafikishwa mahakamani pamoja na kutozwa faini kubwa

Aliongeza kuwa baadhi ya makosa ambayo yataweza kutiliwa mkazo mkubwa hasa ya usafi wa jiji ni pamoja na kutema mate, kukojoa ovyo ndani ya jiji,kutupa taka ovyo,pamoja na kufanya biashara ndani ya maeneo yasiyo rasmi ambapo wakosaji wote watafikishwa mahakamani.

“unaweza kuona Abiria wanatoka mikoani lakini wanapoingia ndani ya Mji wa Moshi wanaambiwa sasa unaingia Moshi hivyo wasitupe taka lakini wanapoingia katika mji wa Arusha wanaambiwa kabisa wapo huru  kuchafua hili tunataka liwe ni historia  kabisa kwani  uwezo wa kufanya jiji liwe katika hadhi yake upo kabisa”aliongeza Ulomi

Pia alibainisha kuwa Kampeni hiyo ya usafi pia itaweza kwenda sanjari na utoaji wa elimu ya mazingira ndani ya Mitaa zaidi ya 100 ambapo wananchi wataelezewa madhara ya uharibifu wa mazingira.

MWISHO

Friday, January 25, 2013

MBUNGE LEMA AMTUNISHIA MISULI MKUU WA WILAYA,AFUNGA SHULE,MKUU WA WILAYA AIFUNGUA KWA GHAZABU KUBWA

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA JOHN MONGELA AKIFAFANUA JAMBO ARUSHA,PICHA NA MAKTABA YA MALKIA WA MATUKIO




Na  Queen Lema,Arusha

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela ameshukia Mbunge wa Jimbo la Arusha  mjini, Goodbless Lema  mara baada ya mbunge huyo kuifungia shule ya Sekondari Korona mapema  jana na kudai kuwa mbunge huyon hana mamlaka ya kufunga shule na asitumie kofia ya ubunge kuvunja Sheria na kuharibu amani ya Jiji la Arusha

Hatua hiyo imekuja leo mara baada ya Mbunge huyo kufungia shule ya sekondari Korona kwa madai kuwa shule hiyo bado changamoto nyingi sana  na hivyo wanafunzi wanasoma masaa mawili mpaka matatu hivyo ni bora kila mwanafunzi ahamishwe na kwenda shule nyingine


Akiongea katika mkutano uliohitishwa na uongozi wa jiji la Arusha Mkuu wa Wilaya,alisema kuwa,kitendo cha Mbunge Lema kufunga shule sio kitendo cha  kuvumiliwa kwa kuwa yeye ndiye mtungaji wa Sheria lakini yeye pia ndiye mvunjaji mkubwa sana wa Sheria hivyo pamoja na kuwa amefunga shule na kuwataka wanafunzi kuondoka ndani ya shule hiyo bado hajawasaidia wanafunzi hao,kwa kuwa jumatatu asubui watarudi na kuendelea na masomo

Alifafanua kuwa endapo kama Mbunge Lema angeona kuwa shule hiyo ya Korona ina matatizo ambayo ameyataja basi angeyatatua kwa kuwa shule hiyo bado ipo ndani ya jimbo na pia ipo ndani ya eneo ambalo anaishi hivyo bado anakuwa chanzo cha kudididimiza maendeleo ya shule hiyo

“haiwezekani mtu akalale na mke wake nyumbani alafu kesho aibuke aseme kuwa shule ya kata haina vigezo kama tutavumilia hili suala la Lema basi kesho na diwani naye atafunga shule kwa kuwa haina vigezo na  viwango  sasa mimi kama mkuu wa wilaya nasema kuwa hili suala halitavumilika ingawaje pia baadhi ya madai ya Lema ni kweli ila kabla ya yote angetakiwa aaangalie sheria ya mwaka 1995 inavyosema juu ya ufungaji wa shule”aliongeza Mongela

Awali Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa madai ambayo Lema ameyatoa ni ya kweli na pia anaungana nae ingawaje anachomlaumu ni kushindwa kushirikiana na Viongozi ili Viongozi wazembe waweze kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Nchi

Mongela alisema kuwa suala la ukosefu wa Maji,Vyoo, na Usafi sio suala la hiari la kutekelezwa na Viongozi wa jiji bali ni suala la lazima kutekelezwa ingawaje mpaka sasa changamoto kama hizo hazijatatuliwa kwenye shule hiyo,na badala yake viongozi wa Jiji wamekaa ndani ya Ofisi zao ilihali wanafunzi wanateseka sana

“Leo tunasema kuwa Lema amefunga shule lakini tuangalie ukweli wa madai yake yupo sawa na mtanisamehe wakati mwingine mimi nitamuunga mkono na kumsaidia katika mambo yake kwa kuwa  wapo baadhi ya watendaji wabovu  ndani ya Halmashauri mnashushia hadhi Serikali na kwa hili mtaondoka mmoja baada ya mwingine na ninaanza na Mkuu wa Shule hii”alisema Mongela

“huyu mkuu wa shule ambaye ni John Ndewila amekuwa ni chanzo kikubwa sana cha haya matatizo ambayo yamepelekea leo shule kutangaziwa kufungwa sasa kwa hali hiyo nasema kuwa naanza nae kwa kumshusha cheo kuanzia sasa ni mwalimu wa kawaida na mpaka jioni barua imfikie’aliongeza Mongela

Awali aliongeza kuwa wanafunzi wa shule hiyo wanatakiwa kurudi shuleni hapo siku ya jumatatu na kuachana na kauli ya Mbunge kuwa shule imefungwa lakini pamoja na hayo Jiji la Arusha kwa kushirikiana na Mkurugenzi,na Afisa elimu sekondari wanatakiwa kuweka maji ndani ya siku moja pamoja na kutatua changamoto  za shule hiyo lakini kama hawatafanya hivyo watavuliwa madaraka

Katika hatua nyingine Lema alisema kuwa kamwe Mkuu wa Wilaya hapaswi kumuingilia katika majukumu yake kwa kuwa yeye amechaguliwa na wananchi wakati Mkuu wa Wilaya ameteuliwa na Raisi

Lema alisema kuwa anachokitafuta machoni mwa watu na Mungu ni haki na wala sio sifa kwa kuwa alipofunga shule hiyo alikuwa na viongozi wa Serikali,kama Vile Afisa elimu Sekondari,Afisa utumishi  na kwa hali hiyo ni vema kama Jiji likasaidia  na kutatua changamoto ambazo zimo kwenye shule za Kata.

MWISHO


Wednesday, January 16, 2013

SHIRIKA LABUNI MBINU MPYA YA KUWAFUATILIA MAMA WAJAWAZITO KWA SIMU ILI KUPUNGUZA VIFO NYAKATI ZA KUJIFUNGUA


SHIRIKA LABUNI MBINU MPYA YA KUWAFUATILIA MAMA WAJAWAZITO KWA SIMU ILI KUPUNGUZA VIFO NYAKATI ZA KUJIFUNGUA

 Jane Edward, ARUSHA

SHIRIKA  la Jhpiego  la jijini Dar es saalam limefanikiwa kubuni aina mpya ya mradi ujulikao kama Maisha ambapo mradi huo utaweza kutumia simu za mkononi kwa ajili ya kufuatilia afya za mama wajawazito  kwa malengo ya kupunguza vifo vya wajawazito

Akiongea na “malkia wa matukio”mjini hapa mapema leo Meneja mradi wa shirika hilo Dkt Dunstan Bishanga alisema kuwa mradi huo wa maisha umeanza kutekelezwa kwa mkoa wa Morogoro

Dkt Bishanga aliongeza kuwa mradi huo una malengo ya kuhakikisha kuwa inapunguza vifo vya mama wajawazito hapa nnchini lakini njia pekee ya kuwakutanisha wahudumu wa afya pamoja na wajawazito ni simu za mkononi hasa  kwa kuwapa wajawazito taarifa mbalimbali


Pia alisema kuwa Mradi huo ambao kwa sasa umeanza kutumika katika Mkoa wa Morogoro lakini wanaendelea kufanya tathimini mbalimbali za kuhakikisha kuwa unasambaa nchi nzima kwani una uwezo mkubwa sana wa kuokoa maisha ya mama wajawazito

Hataivyo aliongeza kuwa mara baada ya mkoa wa Morogoro kunufaika na mradi huo wataweza kwenda mikoani ikiwa ni pamoja na kuongeza zaidi ubunifu zaidi ili kuimarisha zaidi afya ya mama kwa manufaa ya Nchi nzima kwani vifo hivyo vinasababisha sana Umaskini katika jamii.

Awali alisema kuwa suala la mama wajawazito ni suala ambalo linatakiwa kuchukuliwa tahadhari kubwa sana ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu sahihi za afya kutoka kwa wataalamu hivyo nao wazazi wa kiume wana nafasi kubwa sana ya kufanya hivyo

MWISHO

TANZANIA YAANZA RASMI KUTUMIA MFUMO WA KIMATAIFA NA KUACHANA NA MFUMO WA ZAMANI


TANZANIA YAANZA RASMI KUTUMIA MFUMO WA  KIMATAIFA NA KUACHANA NA MFUMO WA ZAMANI

Na Queen Lema,ARUSHA

Tanzania imeanza kutumia rasmi mfumo wa kimataifa katika masuala ya ukaguzi wa ndani ambapo mfumo huo utaweza kupunguza Viashiria mbalimbali vya ubadilifu wa fedha za umma

Hayo yamebinishwa  leo na mkaguzi mkuu wa ndani hapa Nchini Bw Mohamed Mtonga wakati akifungua mafunzo kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika kanda ya kaskazini

Mohamed alisema kuwa mpango huo wa ukaguzi kwa mfumo wa Kimataifa umeanza kutumika rasmi hapa nchini July  Mosi ambapo utaweza kutoa na kuonesha viashiria mbalimbali ambavyo vinakwamisha shuguli za ukaguzi ndani ya Serikali kuu pamoja na  Serikali za Mitaa.

Alisema kuwa kupitia mfumo huo mpya wa kimataifa wa ukaguzi wa ndani utaweza kuboresha  na kuwafanya wakaguzi wa ndani kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi tofauti na mfumo uliokuwa hapo awali ambao ulikua hautoi fursa kwa wakaguzi wa ndani

Alifafanua kuwa hapo awali wakaguzi wa ndani walikuwa wanashindwa kutekeleza  majukumu yao kutokana na viashiria vya vitu mbalimbali kama vile rushwa na uhusiano baina ya mkaguzi na mkaguliwa hali ambayo ilikuwa chanzo cha kukwamisha malengo mbalimbali ya ukaguzi hapa nchini ingawaje  ndani ya mfumo wa ukaguzi kimataifa suala hilo halipo kabisa.


Katika hatua nyingine alisema kuwa wakaguzi wa ndani bado wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa bajeti hali ambayo nayo inafanya washindwe kufanya kazi na kukagua miradi kwa wakati husika

Alisema kuwa kwa sasa wakaguzi wa ndani wanashindwa kufika kwenye miradi tena  kwa wakati kutokana na uhaba wa bajeti ambazo zinatengwa na  Halmashauri huku hali hiyo pia ikichangia sana kutofikia malengo mbalimbali ya kiukaguzi ambayo  yanatakiwa kuwekwa na pia  kusaidia jamii


MWISHO

Tuesday, January 15, 2013

MAKAMU WA RAISI ADAI KUWA VIFO VYA UZAZI VIMEPUNGUA KWA ASILIMIA 50

DKT GHARIB BILALI AKISISTIZA JAMBO LEO KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO,AICC,PICHA NA ASHURA MOHAMED

NA ASHURA MOHAMED,ARUSHA


Idadi ya vifo  vinavyotokana na uzazi imepungua kwa asilimia hamsini ikilinganishwa na mwaka  2009 ambapo takwimu zinaonesha kuwa vifo vilikuwa 500 huku mwaka 2010 vifo vilipungua na kufikia 250 ambapo lengo halisi ni kupunguza vifo vya akinamama na kufikia 193 ifikapo mwaka 2015.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Afya ya Mama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.mohamed Gharibu Bilal alisema kuwa serikali inajitahidi kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa ili kuhakikisha kuwa vifo visivyo vya lazima havitokei tena.

Dkt.Bilal alisema kuwa vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua ni lazima suluhu ipatikane ili kuweza kuzuia matatizo mbalimbali ambayo yanapelekea akinamama hao kupoteza maisha hivyo kupitia mkutano huo ni wazi kuwa watashirikiana vyema katika kupeana utaalam kwa nchi zilizofanikiwa ili kuokoa maisha wa wanawake.

Alisema kuwa baadhi ya nchi ambazo zinashiriki katika mkutano huo wa kimataifa tayari wameshapiga hatua kubwa hivyo kupitia nchi hizo ni wazi kuwa mafanikio yatapatikana na hatimaye Tanzania itaweza kufikia malengo kwa kupunguza vifo vianavyotokana na uzazi.

Aidha amefafafunua kuwa takwimu zinaonesha kuwa nchi za kiafrika zinazoendelea vifo vya akinamama ni vingi sana ambapo kwasasa ni asilimia 99 ya akinamama wanapoteza maisha kutokana na vifo vya uzazi.

“Nataka naomba niwaelezeni kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali ili kuweza kupunguza vifo vya akinamama na kuhakikisha kuwa mama yeyote hafariki dunia kutokana na uzazi na watoto pia wasipoteze maisha kwa magonjwa ambayo yanazuilika.”alisema bilal

Kwa upande wake waziri wa Afya Dkt.Hussein Mwinyi alisema kuwa alisema kuwa wazira yake kwa kushirikiana na serikali ina mikakti ya kuhakikisha kuwa kila mama anapata lishe kabla ya kubeba ujauzito ili aweae kuapata nguvu za kujifungua na kuwa na afya bora.

Alisema kuwa changamoto nyingine inayopelekea vifo kwa akina mama ni usafiri ambapo akina mama wengi wanajifungulia njiani kutokana na umbali pindi wanapotafuta huduma za afya.
Pia kwa sasa serikali itatoa vifaa vya kujifungulia bure ili akina mama wote waweze kujifungulia katika vituo vya  afya kwa kuwa nusu ya akinamama wanajifungulia nyumbani kwa uoga wa  kulipia gharama za vituo vya afya.

Naye Mkurugenzi wa asasi ya (MDH) dkt.Chalamila Guerino alisema kuwa mkutano huo utakuja  na maazimio ya namna  ya kusaidia kupunguza vifo kwa akinamaama kwa kuboresha huduma ya afya ili wanaweze kufikia malengo ya millennia.

Mwisho……………

FRANK LEONARD AKABIDHIWA MIKOBA YA MAREHEMU MWANGOSI IPC

FRANK LEONARD AKABIDHIWA MIKOBA YA MAREHEMU MWANGOSI IPC


Viongozi  wa  IPC  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  wanachama mara baada ya mkutano  huo maalum wa uchaguzi jana kutoka kushoto ni katibu mtendaji  wa IPC Francis Godwin(mwenye suti) ,mwenyekiti  wa IPC Frank Leonard , Mzee Flugence Malangalila mwanachama na aliyekuwa msimamizi  wa uchaguzi huo Frederick Siwale
mwenyekiti mteule  wa IPC  Frank Leonard (kushoto) na katibu mtendaji  wa IPC Francis Godwin kulia tukiteta jambo katika moja kati  ya vikao vyetu mwaka jana
Aliyekuwa mweka hazina wa IPC marehemu Vicky Macha
Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Marehemu Daud Mwangosi na  chini siku alipouwawa  kinyama

KLABU   ya waandishi wa  habari mkoa wa  Iringa (IPC)  imekamilisha  kuziba mapengo ya uongozi yaliyokuwepo  ndani ya IPC  kufuatia  kifo cha aliyekuwa  mwenyekiti wake marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa tarehe 2/9/2012 Nyololo katika vurugu  za polisi na  Chadema kwa  kumchangua Frank Leonard kuwa  mwenyekiti  mpya  wa klabu  hiyo  huku Francis Godwin akiwa katibu mkuu wa IPC.
Mbali ya  kuziba nafasi hiyo ya mwenyekiti kwa Leonard  aliyekuwa katibu mtendaji  kuamua kugombea uenyekiti na Godwi aliyekuwa katibu msaidizi  kugombea ukatibu mkuu pia  wajumbe  wa mkutano huo wame mchagua Janeth Matondo  kushika  nafasi ya mweka hazima  mkuu  wa IPC nafasi  iliyokuwa  wazi  baada ya aliyekuwa mwekahazina Vicky Macha aliyefariki  mwezi  mmoja baada ya  kifo cha Mwangosi .

katika  mkutano  huo maalum  wa uchaguzi huo uliofanyika  leo   katika Hotel ya M.R mjini Iringa  msimamizi mkuu  wa uchaguzi huo Frederick Siwale  aliwataja  waliochaguliwa kuwa ni pamoja na aliyekuwa katibu mtendaji  wa IPC Frank Leonard aliyepata  kura  17 kati ya  kura 18 zilizopigwa katika nafasi hiyo ya uenyekiti  iliyokuwa  ikigombewa na mwanachama Zulfa Shomari aliyetangaza  kujitoa na kuomba  wajumbe  kumchagua Leonard kutokana na utendaji wake mzuri .
Wakati makamu mwenyekiti amepita  bila kupingwa Jackson Manga aliyepata  kura  zote 18 za  wajumbe  wa mkutano  huo ambao jumla ya  wanachama  hai  wa IPC ni 24 na  18  ndio  waliofika katika mkutano  huo  nafasi ya katibu mtendaji  wa IPC imechukuliwa na aliyekuwa naibu katibu mkuu wa IPC Francis Godwin ambaye ni mmiliki  wa mtandao  huu  aliyepata  kura  za ndio 16 huku  kura  2 zikimkataa .

Wengine  waliochaguliwa ni pamoja na mweka  hazina mkuu  wa IPC Janeth Matondo  aliyechukua  nafasi ya marehemu  Vicky Macha kwa kupata  kura  zote  za ndio 18  pamoja na mweka hazina msaidizi  Suleiman Boki  aliyepata  kura  zote 18 .

Wajumbe  watatu wa kamati  ya utendaji   waliochaguliwa ni  Hapy Matanji  aliyepata kura  (18) Swiga  Mwaisumbe (18 ) na Selina Ilunga(17).

WILAYA YA ARUSHA VIJIJINI KWA KUSHIRIKIANA NA MBUNGE WAO KUANZA RASMI MKAKATI WA KUJENGA HOSTELI SHULE ZOTE






WILAYA YA ARUSHA VIJIJINI KWA KUSHIRIKIANA NA MBUNGE WAO KUANZA RASMI MKAKATI WA KUJENGA HOSTELI SHULE ZOTE

Na Queen Lema,ARUSHA


Wilaya ya Arusha vijijini kupitia kwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi,inatarajia kufanya mabadiliko katika sekta ya elimu ambapo kwa sasa wanatarajia kujenga na kuimarisha hosteli kwa ajili ya wanafunzi hususani watoto wa kike ambao wanatembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta elimu huku wakiwa mbioni kupatwa na Vishawishi mbalimbali.

Endapo kama tutajenga hosteli za kutosha basi hata kiwango cha elimu yetu nacho kitaweza kupanda kwa hali ya juu sana tofauti na sasa ambapo wanafunzi wanalazimika kupanga nyumba”GETO”ili wasome karibu na shule.

Hayo yameelezwa na Mbunge wa Arumeru Magharibi ambaye pia ni Naibu waziri wa ardhi Goodlucky  ole Medeye wakati akikabidhi hundi kwa halmashauri ya Arusha vijijini  ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Olokii  mapema wiki hii.

Medeye alisema kuwa ameamua kuwa balozi wa hosteli kwenye shule za Jimbo lake kwa kuwa bado watoto wa kike wanakabiliwa na changamoto nyingi sana hasa  ya kutembea umbali  mrefu huku wengine wakipanga nyumba hali ambayo inawafanya washindwe kusoma kwa raha huku hali hiyo nayo ikichangia sana washindwe kufanya vema katika masomo yao.

Alisistiza kuwa lengo lake halisi ni kuona kuwa hosteli zinakuwa ni nyingi sana ambapo wanafunzi watakaa mashuleni na kisha kusoma kwa raha huku pia hosteli hizo nazo zikichangia sana waweze kuondokana na Vishawishi ambavyo wanakutana navyo wakati wakiwa njia kuja au kurudi  majumbani  mwao

“Vishawishi kwa mtoto wa kike ni vingi sana lakini  kama sote tutainuka na kuhaikisha kuwa hawa tunakuwa na hosteli za kutosha basi itaweza kuraisisha sana maendeleo ya elimu lakini kama tutakuwa na tabia ya kujivunia eti wingi wa shule wakati watoto wanatembea umbali mrefu kutafuta elimu na barabarani wanakutana na vishawishi kibao ni wazi kuwa bado tutakuwa hatujafanya chochote kipya kabisa”aliongeza Medeye

Katika hatua nyingine alisema kuwa ili lengo hilo la ujenzi wa hosteli liweze kukamilika tena kwa wakati katika baadhi ya shule ndani ya Jimbo na Halmashauri yake ni lazima kuwepo na Ushirikiano tena wa hali ya juu sana ili kuweza kuwanusuru  watoto kutoka katika nyumba za kupangisha”GETO”

MWISHO.

LEMA ATETA NA MAFISADI WANAOTUMIA MAKANISA NA MISIKITI KWA AJILI YA KUJISAFISHIA

MBUNGE WA ARUSHA MJINI GOODBLESS LEMA AKIHUTUBIA WANANCHI KATIKA MOJA YA MIKUTANO YA HADHARA




LEMA ATETA NA MAFISADI WANAOTUMIA MAKANISA NA MISIKITI KWA AJILI YA KUJISAFISHIA

Na Queen Lema,ARUSHA


MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Bw Goodbless Lema ameyataka makanisa na Misikiti hapa nchini kuachana na tabia ya kuwakumbatia mafisadi kutokana na wingi wa sadaka zao na badala yake kuwaombea mafisadi hao waweze kubadilika

Asilimia kubwa ya mafisadi bila kujali imani zao sasa wanatumia sana Makanisa na Misikiti ili kwenda kujisafisha kwenye jamii kwa kuchangia kiwango kikubwa sana cha fedha huku fedha hizo za sadaka zikiwa ni  fedha chafu

Lema aliyasema hayo Jijini hapa wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo lake mapema jana,huku lengo halisi likiwa ni kukumbuka siku ya January tano ambayo baadhi ya wananchama wa Chadema walipoteza Maisha

Aidha Lema alisema kuwa tabia hiyo ambayo kwa sasa imeibuliwa na mafisadi ya kujisafisha kupitia vyombo vya dini si tabia njema kabisa bali ni tabia ambayo inapeleka nchi na kizazi chake mahala pabaya sana huku pia hali hiyo ikichangia Umaskini mkubwa sana kwenye jamii ya watanzania

Alisema kuwa wananchi kamwe hawapaswi kukubaliana na hali hiyo ya mafisadi sasa kutumia majumba ya ibada na kujisafisha bali na wao wanatakiwa kuamka na kuanza kufanya kazi ili waepukane na fedha chafu ambazo zinatolewa na mafisadi kwenye majumba ya ibada kama harambee

‘mimi nashangaa sana ninyi viongozi wa majumba ya ibada ambao kila kukicha mnakaa na kuomba Rehema lakini Mafisadi wakija na Fedha chafu hamuwaulizi na badala yake ndio mnawawekea mikono ya baraka sasa hamuwezi kuona kuwa mnawawekea mikono waendelee na kazi yao ya kuwaibia wananchi wa Tanzania?alisema Lema

Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kuwa yeye ni Mbunge lakini kamwe hatukubali kuona kuwa anahujumiwa ili awaache wananchi wa jimbo la Arusha mjini kwa kuwa wananchi hao ndio waliomuamini na wakampa kura ili aweze kuwaongoza tena kwa njia ya uhalali kabisa

Alisisitiza kwa wananchi kuwa ipo haja ya watu wote kumrudia zaidi Mungu na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa mwaminiufu kwani uaminifu pekee ndio utakaoleta maendeleo ya Mkoa wa Arusha pamoja na Nchi ya Tanzania tofauti na kutegemea fedha chafu za harambee kutoka kwa Mafisadi

Hataivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Arusha(CHADEMA)kiliweza kutoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu vya watoto yatima huku lengo likiwa ni kukumbuka mauji dhidi ya wanachama wa chama hicho yaliyofanyika January 5 mwaka jana.

MWISHO

VIONGOZI WA NJANJA MBALIMBALI TANZANIA WATAKIWA KUACHA MAOVU ILI KUOKOA TAIFA DHIDI YA LAANA MBALIMBALI


VIONGOZI WA NJANJA MBALIMBALI TANZANIA WATAKIWA KUACHA MAOVU ILI KUOKOA TAIFA DHIDI YA LAANA MBALIMBALI

IMEELEZWA kuwa kutokana na tabia ya baadhi ya Viongozi wa Serikali kujihusisha na utafutaji wa mali ambazo si halali,Rushwa,pamoja na ukatili kumesababisha Umaskini pamoja na Laana kubwa sana kwa baadhi ya watanzania

Asilimia kubwa ya viongozi wan chi katika nyanja tofautitofauti ambao wanajihusisha na masuala hayo kumechangia sana madhara makubwa na hata wengine kufanya wananchi ambao wanawaongoza kufanya matendo ambayo ni ya kikatili na machafu mbele za mungu.

Hayo yamebainishwa na Mchungaji Wilson Laizer wa kanisa la T A G Christian Centre lilopo Enaboishu mkoani hapa wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo wiki iliyopita.

Mchungaji Laizer alisema kuwa Viongozi wa Nchi ambao wanatafuta mali na mafanikio kwa njia ambazo si halali kunachangia sana madhara makubwa sana kwa nchi hivyo viongozi hao sasa wanatamkiwa kuhakikisha kuwa wanamgeukia Kwanza Mungu kabla ya kuvisha Nchi laana ya mafaniko ambayo si ya halali.

Alisema kuwa Viongozi wa nchi ambao tayari wamejihusisha na halin kama hiyo wanatakiwa kwanza kuhakikisha kuwa wanatubu na kujutia ambacho wamekifanya ambapo hali hiyo itaweza kuruhusu Roho ya toba hata kwa wale ambo wamewazulumu kwa njia moja au nyingine katika utafutaji wa mali

“kutafuta mali kwa nguvu huku ukitumia mbinu ambazo zinamkandamiza mwenzako si jambo zuri sana bali ni jambo ambalo linafanya Nchi kuwa na machafuko na mambo ambayo si mazuri ni vizuri hata viongozi wetu wa sasa wakajua kuwa kumzulumu mtu mali yake na hata haki zake ni vibaya sana hivyo nawasihi sana ninyi ndugu zangu mhakikishe kuwa mnaomba toba hata kwa watu wengine ili muweze kuokoa nchi ya Tanzania “alisema Mchungaji huyo

Awali alisema kuwa hata kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa wabinifu tena wa hali ya juu sana hasa katika kumtafuta na kujaribu kuuteka ufalme wa Mungu  ili waweze kufikia malengo yao ya kiroho na hata ya kimwili.

Alibainisha kuwa kwa kufanya hivyo wataweza kuepukana na tabia ya kuwekezewa zaidi fikra na Utukufu wa shetani ambao mara zote ni utukufu wa uongo na badala yake wataweza kuliongoza taifa kwenye mpango wa Mungu ambao unahitajika tena kwa haraka sana kuendelea kutumika ndani ya Nchi ya Tanzania.

MWISHO

MAASKOFU WATAKIWA KURUHUSU WALIMU KUFUNDISHA NYIMBO ZA KUSIFU NA KUABUDU NDANI YA MAKANISA YAO

BAADHI YA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI JIJINI ARUSHA WAKIIMBA  NA KUTUMBUIZA KATIKA MKUTANO WA INJILI




Na bety alex,Arusha

MAASKOFU WATAKIWA KURUHUSU WALIMU KUFUNDISHA NYIMBO ZA KUSIFU NA KUABUDU NDANI YA MAKANISA YAO

MAASKOFU wa makanisa mbalimbali ambao hawana uwezo wa kutunga nyimbo mbalimbali za kusifu na kuabudu wametakiwa kuhakikisha kuwa kamwe hawaachi makanisa yao yakiendelea kupoteza uwepo huo bali wanatakiwa kuwatumia zaidi walimu ambao wana uwezo wa kufundisha nyimbo za kusifu na kuabudu.

Kauli hiyo imetolewa na askofu Aminiel Mgonja wa kanisa la Arusha Praise Centre la jijini hapa wakati akiongea na “MALKIA WA MATUKIO”mara baada ya kutambulisha rasmi Album yake ijulikanayo kama Ueponi mwako

Askofu Mgonja alisema kuwa kipajin cha kutunga kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu si watumishi wote ambao wana uwezo wa kufanya hivyo lakini kutokana na kushindwa kufanya hivyo si sababu pekee ambayo itaweza kuyafanya makanisa kushindwa kusifu na kuabudu

Alisema kuwa kama watumishi wa Mungu wataweza kuwapa fursa baadhi ya walimu kuweza kufundisha na kutunga nyimbo mpya za kusifu na kuabudu hali ambayo itawafanya Uwepo wa Mungu kuweza kusogea tena kwa haraka sana tofauti na sasa ambapo baadhi ya makanisa yanashindwa kufungulia huduma hiyo.


Pia alisema kuwa hata kwa wale ambao wana uwezo wa kutunga nyimbo za kusifu na kuabudu bado wana uwezo mkubwa sana wa kuendelea kuwa wabunifu tena wa hali ya juu sana  kwa kuhakikisha kuwa nyimbo ambazo wanazitunga zinakuwa ni njia mojawapo ya kuwasogeza watu uweponi mwa Bwana.

Katika hatua nyingine Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Album hiyo ya Uweponi mwako,Askofu Olam Mustapha kutoka katika kanisa la Gloryland,alisema kuwa mtumishi wa mungu anapofanya Jambo zuri hata watumishi wengine nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafuraia jambo hilo na Kumuunga mkono na kuachana na tabia ya kuchukiana ovyo

Olamu alisema kuwa wapo baadhi ya watumishi wa Mungu pamoja na Wakristo ambao kila mara wanachukiana kwa ajili ya mafanikio ya Mtu lakini hali hiyo ni mbaya sana na ndio inayomtukuza shetani badala ya Mungu.


Pia katika uzinduzi huo wa Album hiyo zaidi ya Milioni tisa zilikusanywa kutoka kwa watu mbalimbali huku  lengo halisi likiwa ni kumuunga mkono Askofu huyo.

MWISHO

LIPIENI MILIONI MBILI ZA ALAT TUTATUE CHANGAMOTO AMBAZO ZIPO KWENYE JAMII ZENU KWA PAMOJA





LIPIENI MILIONI MBILI ZA ALAT TUTATUE CHANGAMOTO AMBAZO ZIPO KWENYE JAMII ZENU KWA PAMOJA

Na Mwandishi wetu,ARUSHA

HALMASHAURI  za mkoa wa Arusha zimeagizwa kutoa kiasi cha Milioni mbili kama mchango kwenye Jumuiya ya Serikali za mitaa kwa mkoa wa Arusha(ALAT)ambapo michango hiyo itaweza kusadia na kutatua changamoto mbalimbali hasa kwenye Serikali za Mitaa

Agizo hilo limetolewa Mapema wiki hii na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Goodson Majola wakati akiongea na wananchama wa umoja huo mjini hapa

Majola alisema kuwa ni vizuri kwa kila Halmashauri kuhakikisha kuwa inachanga kiasi hicho na kuachana na tabia ya kukwepa michango mbalimbalin kwani kwa kutotoa Michango ndani ya Umoja huo unachangia sana maendeleo kuwa hafifu sana

Alisema kuwa Michango hiyo ina umuhimu mkubwa sana hususani kwa wakati kama huu ambao  jamii inakabiliwa na matatizo makubwa ambayo yanaitaji ufunguzi tena kuanzia ngazi za Serikali za mitaa.

“ni lazima kila halmashauri iweze kutoa na kuchangia kiasi cha Milioni mbili kuanzia sasa na Halmashauri ambayo haitachangia kiasi hicho kwa wakati kwa kweli hautaweza kuwatambua kwani chombo hiki kina nafasi kubwa sana ya kuweza kutatua matatizo ya wananchi hivyo Umoja ni muhimu sana na tutumie chombo hiki katika kutatua kero za wananchi’aliongeza Majola.

Katika hatua nyingine wadau wa Umoja huo walisema kuwa pamoja na kuwa Halmashauri zinatakiwa kuachana na Tabia ya kukwepa Michango mblimbali lakini Jumuiya hiyo inapswa kuhakikisha kuwa inatatua kero ambazo zipo kwenye Serikali za mitaa hasa Migogoro ya ardhi na Mipaka.

Akiongea suala hilo Diwani wa Mwandeti,Boniface Tarakwa alisema kuwa sehemu pekee ya kupata muafaka wa masuala ya migogoro ni kwenye ALAT kwa kuwa ina meno ya kuweza kutoa  majibu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali hali ambayo itachangia sana Amani.

Tarakwa aliongeza kuwa matatizo ya Migogoro ya Ardhi imesababisha madhara makubwa sana na inatakiwa kumalizwa tena kwa haraka kupitia kwenye umoja huo hasa kwa kuyafikisha kwenye sehemu muafaka hasa kwenye vikao vikuu vya mkoa.

“Jambo la msingi hapa ni jumuiya hii ihakikishe kuwa inamulika hata shida ambazo zipo na itusemehee kwenye ngazi za juu kwani zipo baadhi ya ngazi ambazo zinatupiga chenga  na huku kwenye jamii tunaonekana kama wasanii hivyo Matumizi mazuri ya jumuiya hii yatachangia sana maendeleo na nafasi nzuri kwenye jamii ambayo tunaiongoza’aliongeza Tarakwa.

MWISHO

Monday, January 14, 2013

MERU WAPATA HASARA YA MILIONI 30 KUTOKANA NA WAWEKEZAJI KUKIMBILIA KWENYE MPANGO WA EPZ


MERU WAPATA HASARA YA MILIONI 30 KUTOKANA NA WAWEKEZAJI KUKIMBILIA KWENYE MPANGO WA EPZ

Na Queen Lema,MERU

HALMASHAURI ya Meru Mkoani Arusha imepata hasara ya zaidi milioni 30 kwa kipindi cha miaka miwili mara baada ya kukosa kodi katika mashamba makubwa mawili yaliopo ndani ya halmashauri ambapo mashamba hayo yameingia katika mpango rasmi wa maendeleo ya uchumi na viwanda(EPZ)

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Trasias Kagenzi wakati akiongea na Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo katika kikao cha kupitisha bajeti ya Halmashauri hiyo mapema jana.

Kagenzi  alisema kuwa Halmashauri  hiyo imepata hasara ya ukosefu wa kodi kutoka kwa wawekezaji wawili ambao wameingia katika mpango huo wa EPZ ambao walikuwa wanachangia kodi kwa kiasi cha Milioni kumi na tano kwa mwaka.

Aliongeza kuwa  Wawekezaji  wa mashamba hayo  ambao wamehamia katika mpango huo ni pamoja na Doll Esatate, huku Mwekezaji mwingine akiwa ni Delka Bruine ambapo walikuwa wanchangia kiwango kikubwa sana cha kodi hali ambayo imesababisha mapungufu makubwa sana.

Alisema kuwa  hasara hiyo ya Mamilioni ya fedha inachangia sana Halmashauri hiyo kushindwa kufikia malengo yake mbalimbali ambayo wamejiwekea lakini pia mpaka sasa wameshabuni chanzo mbadala ambacho kitaweza kufuta kwa kiwango hasara hiyo kubwa ambayo imetokana na wawekezaji kujiunga na mpango wa EPZ

“hapo awali tulikuwa tunachukua kiasi cha Milioni 15 kwa wawekezaji hawa wawili lakini kwa miaka miwili tumekosa kodi zao kwa kweli hii ni hasara kubwa sana nah ii pia tutaitumia kama changamoto hata kwa hawa wengine ambao nao wanampango wa kujiunga na EPZ kwani kama tusipokuwa wajanja na tukabuni aina mpya ya vyanzo vya mapato basi halmashauri itakuwa katika hali tete”aliongeza Kagenzi

Katika hatua nyingine alisema kuwa mbali na kukosa Milioni 30 kama kodi lakini mpango huo utaweza kuwanufaisha watu wengi hususani Vijana ambapo kwa awali utatoa ajira kwa Vijana zaidi ya 5000 huku hali hiyo ikichangia kwa  kiwango kikubwa sana hata Ukuaji wa Uchumi wa  Meru

Kagenzi alifafanua kuwa wananchi wa Meru wanatakiwa kutumia vema fursa ambazo zipo na wahakikishe kuwa kupitia fursa hizo  na wao wanakuwa wabunifu kwa kuweza kujiandaa hata kuanzia sasa kuboresha bidhaa ili ziweze kuendana na soko la Nchi jirani

MWISHO