Monday, December 31, 2012

WAOMBA KUPANDISHIWA HADHI ZAHANATI ALIYOZINDUA MAMA NYERERE MWAKA 1964


WAOMBA KUPANDISHIWA HADHI ZAHANATI ALIYOZINDUA MAMA NYERERE MWAKA 1964

Na Queen Lema,MERU

SERIKALI imeombwa kupandisha hadhi zahanati ya kata ya Majengo wilayani Meru mkoani Arusha ambapo zahanati hiyo ilizinduliwa rasmi na kupewa misaada na Mama Maria Nyerere mwaka 1964 huku malengo ya Mama huyo yakiwa ni kubadilika kutoka zahanati na kuja kituo cha afya kwa haraka sana jambo ambalo mpaka sasa halijafanyiwa kazi.

Hayo yamebainishwa na Paulo Mayeke ambaye ni katibu kata ya Majengo,wakati akiongea na Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha waliotembelea Kata hiyo na kuzindua Kata mpya ya chama cha mapinduzi mapema jana.

Aidha bw Mayeke alisema kuwa Zahanati hiyo ya Majengo ilizunduliwa Rasmi na Mama Nyerere huku lengo halisi la Mama huyo likiwa ni zahanati hiyo isidumu kama zahanati na badala yake iwe kwenye mfumo wa kituo cha afya ili kiweze kuhudumia watu wengi zaidi hata wa vijiji vya Jirani kwa kuwa Kata hiyo ipo Karibu sana na Machimbo ya madini ya Tanzanite

Aliendelea kwa kusema kuwa endapo kama Serikali ya sasa itakumbuka na kurejea kauli na ahadi  ya Mama Maria Nyerere basi itachangia kwa kiwango kikubwa sana kuraisisha shuguli za afya ndani ya Kata hiyo ambayo imedumu na zahanati badala ya kituo cha afya kwa muda mrefu sana huku jamii nayo ikiendelea kukabiliwa na Magonjwa mbalimbali.

Alisema kuwa endapo kama itakuwa katika mfumo wa Zahanati basi itachangia sana kuokoa maisha ya watu kwani itakuwa na wataalamu wengi wa afya tofauti na sasa ambapo kutokana na hadhi yake inawahudumu wachache sana wa Afya hali ambayo inachangia sana wananchi kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma hizo.
“jamani hii zahanati ya kata ya Majengo ilizinduliwa na kupewa mikakati mbalimbali na Mama Nyerere kwa mwaka 1964 lakini moja ya msisitizo wake mkubwa ilikuwa ni kuwa katika hadhi ya kituo cha afya lakini toka siku ile ameondoka Kijijini hapa hakuna kilichoendelea hivyo basi tunaomba Serikali itusaidie kwani Wananchi wetu wanapata shida kubwa sana ya matibabu na hivyo kama watafanya hivyo wataweza okoa maisha ya watu wengi zaidi”aliongeza Bw Mayeke

Awali mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Bw Onesmo Nangole alisema kuwa watendaji wa chama hicho kuanzia ngazi ya Vitongoji mpaka mkoa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatatua na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi sanjari na kutafutia ufumbuzi jambo ambalo litaweza kuwafanya wananchi kuwa katika kundi moja la chama hicho

Bw Nangole aliongeza kuwa tabia ya Viongozi kukaa kimya na kusinzia huku wakijiita ni viongozi haipaswi kuvumikila kwani tabia hiyo ndiyo inayochochea Kero kubwa sana kwa wananchi na hata mara nyingine kusababisha ahadi mbalimbali zishindwe kutekelezwa huku wananchi nao wakielekeza lawama kwa Chama cha Mapinduzi(CCM)

“Nawasihi sana Viongozi kuanzia ngazi ya chini kuamka kuanzia sasa acheni kuwapa wapinzani nguvu kwa kero za wananchi mbona mnauwezo wa kuweza kufanya mabadiliko na changamoto hata ahadi mbalimbali mkazifuatilia,kwa kuwa sasa hivi changamoto yoyote ile kwenye jamii ndio nguvu ya wapinzani sasa hakikisheni kuwa hawa wapinzani wanakosa nguvu kabisa”aliongeza Bw Nangole

MWISHO

TUMIENI FURSA IPASAVYO


 NA MWANDISHI WETU MANYARA

JAMII nchini imeaswa kutumia ipasavyo fursa zilizopo na zinazotolewa na Serikali au mashirika mengine ya ndani na nje ya nchi hususani shirika la kazi duniani (ILO) kwa kuwa wabunifu na kujituma ili waweze kujiendeleza kimaisha.

Hayo yameelezwa juzi mjini Kateshi wilayani Hanang’ mkoani Manyara na Ofisa Maendeleo ya mifugo na uvuvi wa wilaya hiyo Dk Tom Maeda,kwenye uzinduzi wa mpango wa ukuzaji wa ujasiriamali kwa vijana wenye kauli mbiu moto wa nyika.

Katika uzinduzi huo ulioandaliwa na asasi ya Disabled and Orphans Hope Centre (Dohoce) ya wilayani Hanang’ kupitia shirika la kazi duniani (ILO) Dk Maeda alisema huu ni wakati wa wajasiriamali nchini kuchangamikia fursa zilizopo.

Alisema wilaya hiyo ni sehemu ya jumuiya ya watanzania wenye kuwajibika kutekeleza malengo ya milennia na dira ya Taifa ya mwaka 2025 na mkakati wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini (Mkukuta) namba mbili.

“Haya yote yanategemea kwa kiwango kikubwa utashi wa jamii hasa vijana kujituma,kuwa wabunifu na kupenda kujiajiri wenyewe kwa kutumia fursa zilizopo na zinazotolewa na Serikali na asasi za kijamii,” alisema Dk Maeda.

Naye,Mratibu wa Dohoce,Kianga Mdundo alisema takwimu zilizotolewa na Waziri wa kazi na ajira Dk Makongoro Mahanga,zinaonyesha kuwa watanzania walioajiriwa kwenye sekta rasmi ni asilimia 30,ajira Serikali asilimia tano,sekta zisizo rasmi asilimia 35 na wasio na ajira asilimia 30.

Mdundo alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mahesabu ya mashirika ya umma,Zitto Kabwe alisema wahitimu wa vyuo vyote nchini kwa mwaka ni 650,000 na wanaopata ajira ni 40,000 na 610,000 waliobaki wanakosa ajira.

“Kwa hiyo soko la ajira isiyo rasmi ndiyo inayotegemewa kuwa mkombozi wa vijana katika kujiletea maisha bora kwa kila mtanzania hivyo Dohoce imeamua kuwajengea uwezo jamii iliyopo wilayani Hanang’,” alisema Mdundo.

Kwa upande wake,mwezeshaji wa mafunzo hayo Julius Slaa alisema kada zilizopatiwa mafunzo hayo na kupatiwa cheti ni mafundi wa ushonaji,seremala, magari,pikipiki,waashi,mamalishe,wakulima,wafugaji na wasindikaji vyakula.

Slaa aliwataja wengine ni wakuzaji miche ya miti,wadau wa sokoni,wana harakati wa mazingira,wafugaji wa nyuki,taasisi za fedha,wasimamizi na waandaji wa mipango,wakuzaji miche ya miti,wana michezo na wana habari.

MWISHO.

Sunday, December 23, 2012

Serikali ya Poland yakabithi miradi yenye thamani ya USD 360,000 kwa chuo cha Mifugo Kampasi ya LITA –Tengeru.

Serikali ya Poland yakabithi miradi yenye thamani ya USD 360,000 kwa chuo cha Mifugo Kampasi ya  LITA –Tengeru.

Happy Lazaro, Arusha.

SERIKALI  ya Poland imekabithi na kuzindua jumla ya miradi mitatu yenye thamani ya USD 360,000  iliyopo katika chuo cha mifugo Campus ya LITA   Tengeru , katika hafla iliyofanyika hivi karibuni chuoni hapo.

Aidha hafla hiyo ya makabithiano ilihudhuriwa na Mwakilishi kutoka wizara ya mambo ya nje (Poland)  ,Dr. Inveterinary and medicine PHD holder ,Dr. Maciej  klockiewicz ,na Mkurugenzi wa mradi huo, Dr.Eng.Wieslaw Ptach kutoka serikali ya Poland.

Akizungumzia miradi hiyo katika uzinduzi huo,Mkufunzi wa chuo hicho, David Malishi alisema kuwa awamu ya kwanza ya miradi hiyo ilianza rasmi mwaka 2009 ambapo wafadhili hao walianza kwa kununua vifaa mbalimbali vya kufundishia vikiwemo vya maabara.

Ambapo awamu ya pili mradi ulilenga kuimarisha matumizi mazuri ya maji ili kuboresha uzalishaji wa mazao katika malisho ya mifugo na chakula  ,pamoja na zana za kilimo ambapo waliweza kuchimba bwawa la kuhifadhia maji ya umwagiliaji na kujenga mifereji ili kuimarisha umwagiliaji.

Malishi alisema kuwa, mradi wa awamu ya tatu ulijikita zaidi katika umwagiliaji na ujenzi wa mitambo ya bioges na upandaji miti ambapo waliweza kukabithi pump za kumwagilia maji 2,pamoja na kukabithi visima 3 vya maji kila moja ikiwa na quibick mita 50 .

Aliongeza kuwa, katika bioges waliweza kukabithi jumla ya mitambo 2 ya bioges kila moja ikiwa na quibick mita 50 ,ikiwa ni pamoja na upandaji miti ambapo kwa msimu wa mwezi wa 3 hadi 6 jumla ya miti 4500 ilioteshwa kwa mchango wa serikali ya tanzania .

Alisema kuwa, katika miradi hiyo yote mitatu serikali ya Tanzania imeweza kuchangia asilimia 30 kama mchango wao .
Malishi alisema kuwa , kupitia miradi hiyo na kupatiwa vifaa mvalimbali hivi sasa wameweza kuboresha ufundishaji kwa vitendo zaidi kutokana na kuwepo kwa vifaa mbalimbali tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

‘Unajua hawa wafadhili wetu wa serikali ya Poland wametusaidia sana kwani chuo hiki ni cha zamani na kilikuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi sana  ili kuweza kutoa elimu iliyo bora hivyo kwa sasa hivi kupitia miradi hiyo imesaidia chuo chetu kuweza kuonekana cha kisasa zaidi na kuendelea kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaokuja chuoni hapo kila mwaka’alisema Malishi.

Alitaja changamoto kubwa ambayo inawakabili chuoni hapo na taasisi zote za eneo la LITA Tengeru  ni uhitaji mkubwa wa maji ambapo kwa makisio wanahitaji USD 110,000 ili kujenga vizima ,hivyo pendekezo hilo wamelipeleka kwa wafadhili hao wa serikali ya Poland kuona kama watawawezesha .

Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Naibu Katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi , Dkt Yohana Badeba alisema kuwa kuwepo kwa uhsirikiano huo mzuri katika ya serikali ya Poland na Tanzania utawezesha kwa kiasi kikubwa kuzidi kuboresha miradi mbalimbali katika chuo hicho kwani kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi sana.

Aliwashuruku wafadhili hao kwa msaada mkubwa walionyesha chuoni hapo wa kujenga miradi mbalimbali itakayowezesha chuo hicho kuweza kufikia malengo yake waliyojiwekea ,hivyo kuwasihi kuzidisha ushirikiano huo zaidi.

Alikitaka chuo hicho la mifugo LITA kutumia vifaa mbalimbali walivyokabithiwa kwa ajili ya kuboresha chuo hicho kuhakikisha wanazitumia ipasavyo na kwa manufaa ya chuo hicho kwa ujumla.

Mwisho.

WAZIRI WA ZAMANI WA MIPANGO WA RWANDA AHUKUMIWA MIAKA 35 JELA

WAZIRI WA ZAMANI WA MIPANGO WA RWANDA AHUKUMIWA MIAKA 35 JELA
 
Na Nicodemus Ikonko, Hirondelle, Arusha

 Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda(ICTR) imemhukumu kifungo cha mika 35 jela Waziri wa zamani wa Mipango wa Rwanda,Augustin Ngirabatwara baada ya kumtia hatiani kwa mashitaka matatu ya mauaji ya kimbari.

Mahakama iliyokuwa inaongozwa na Jaji William Sekule kwa kauli moja imemtia hatiani ngirabatware kwa mashitaka ya mauaji ya kimbari, uchochezi na ubakaji kama uhalifu dhidi ya binadamu.

‘’Augustin Ngirabatware, mahakama imekuona una hatia kwa mauaji ya kimbari, uchochezi na ubakaji kama uhalifu dhidi ya binadamu,’’ Jaji Sekule alisema huku Ngirabatware akielekeza uso wake chini.
‘’Kwa uhalifu huu na kwa kuzingatia mazingira yote ya kesi hii, mahakama inakuhukumu kifungo cha miaka 35 jela,’’ alitamka Jaji Sekule.

Katika hukumu yake,mahakama imemtia hatiani Waziri huyo wa zamani kwa mauaji ya kimbari kutokana na ukweli kwamba alichochea, kusaidia na kuunga mkono mashambulizi na mauaji dhidi ya Watutsi katika wilaya yake ya Nyanyumba, mkoa wa Gisenyi, Kaskazini mwa Rwanda alikozaliwa. Alitekeleza uhalifu huo kwa kwa kupitia hotuba na vitendo vyake kwa kugawa silaha Aprili 7, 1994.

Mahakama ilibaini kwamba baadhi ya silaha zilizogawanywa kwa wanamgambo wa interahamwe zilitumika katika mashambulizi na mauaji na kwamba maneno yake na vitendo vyote kwa pamoja vilitoa hamasi kwa wanamgambo hao kufanya uhalifu huo katika wilaya ya Nyamnyumba.

Ngirabatware ambaye ni mkwe wa mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ambaye bado anasakwa vikali na ICTR alijitetea kwa kudai kwamba wakati mauaji hayo yanafanyika yeye hakuwepo wilayani kwake, utetezi ambao ulitupwa na mahakama.

Mfungwa huyo, ambaye kitaaluma ni daktari wa uchumi alitiwa mbaroni nchini Ujerumani Septemba 17,2007 na kisha kuhamishiwa Arusha, makao makuu ya ICTR Oktoba 8, 2008. Kesi yake ilianza kusikilizwa Septemba 29, 2009.

MBUNGE LEMA ATEKA JIJI LA ARUSHA APOKELEWA NA MAELFU YA WATU


DSCF3646
Pichani ni Mbunge Rasmi wa Jimbo la Arusha mjini Goodblesss Lema,akiongea na wananchi wake rasmi mara baada ya kurudishiwa ubunge rasmi,hapa ni katika viwanja vya stendi ya Kilombero

LEMA WATU ARUSHA
huu ni moja ya msafara wa watu wengi sana waliokuwa wakimuongoza Lema mara baada ya kupokelewa rasmi ndani ya Jiji lake mapema leo
LEMA MNARA WA SAA
Ilikuwa ni ngumu sana kwa Kamanda Lema kuficha hisisa zake hapa Lema alikuwa akikatisha mitaa mbalimbali ya jiji na alionesha furaha kwa mara nyingine
LEMA AKIPUNGIA(1)
Arusha ilifana sana kila mtu alikuwa na furaha,mapokezi ya Kifalme bwana
DSCF3578
Toyo hazikuwa nyuma kama kawa zilipamba njia na kusafisha njia mfalme apite wewe

DSCF3580
kwa kuwa kulikuwa na watu weng sana wengine walilazimika kutumia magari  na miti ili wasipitwe
DSCF3585
Mabango na yenyewe hayakukosekana pamoja na watoto.
DSCF3597
hapa ni viongozi mbalimbali wa Chadema wakitafakari jambo mara baada ya Mh Lema kuwasili katika viwanja vya Kilombero Jijini hapa(picha na Queen Lema,Arusha

Wednesday, December 19, 2012

-WENYEVITI WA VIJIJI VITANO MERU WAMFUKUZA DIWANI MERUWAMPA SIKU 14 KAMA HATAJIUZULU WAO WATAJIUZULU UCHAGUZI URUDIWE UPYA



-WENYEVITI WA VIJIJI VITANO MERU WAMFUKUZA DIWANI MERUWAMPA SIKU 14 KAMA HATAJIUZULU WAO WATAJIUZULU UCHAGUZI URUDIWE UPYA

-KISA WADAI KUWA DIWANI HUYO NI MCHOCHEZI NA ANALIPIZA KISASI KWA KUWA HAWAKUMPA KURA 2010

KATIKA hali  isiyokuwa ya kawaida Wenyeviti wa Vijiji Vitano kutoka katika kata ya Nkoaranga Wilayani Meru mkoani hapa wamemtaka diwani wa kata hiyo kujiuzulu ndani ya siku 14 na endapo kama hawatafanya hivyo basi wao watalazimika kuachia ngazi kwa kuwa wanaonewa sana na diwani huyo

Wenyeviti hao walitoa tamko hilo jana mara baada ya diwani huyo kushindwa kuwasikiliza kero zao pamoja na  za wananchi na badala yake kupewa maneno ya kashfa yakiwemo maneno ya uvaaji wa kimaskini huku pia kila siku kuna kithiri wimbi la migogoro

Wakiongea jana na “MALKIA WA MATUKIO”wilayani humo wenyeviti hao walisema kuwa wanazo sababu maalumu za kumakataa diani huyo ambaye ni Bw Goodfey Kishongo kwa kuwa yeye ndio chanzo pekee cha vurugu na Migogoro ndani ya kata  hiyo ya Nkoaranga hali ambayo imesababisha maendeleo kuwa duni sana

Wenyeviti hao ambao wanatokea katika Vijiji Vitano vya Kata hiyo ambavyo ni Njani, Nshupu,Nkoaranga,Nkoanekoli,na Sangananu walisema kuwa na endapo kama ataendelea kukaa madarakani  hata kama amepitishwa na wananchi basi baada ya siku 14 wao watajiuzulu na kupisha uchaguzi mwingine uanze upya kwani hawapati msaada wala ushirikiano wowote kutoka kwa diwani huyo na badala yake wanaambulia kasfa ya kuitwa maskini

Walisema kuwa zipo sababu maalumu ambazo zinasabababisha wao watamke hayo ingawaje wote ni chama Kimoja (CCM) kwani diwani huyo amekuwa akiwageuka mara kwa mara na hivyo kusisitiza hata migogoro ndani ya jamii huku pia akishirikiana na Vyama vya Upinzani ili waweze kutoka madarakani na kuachia wapinzani badala ya CCM

 Wakielezea kisa halisi cha kuwafanyia hivyo ilihali wao wote ni viongozi wa Serikali ya Kijiji walisema kuwa chanzo halisi diwani huyo anasema kuwa hawakumpa kura kwa mwaka 2010 za udiwani hali ambayo inafanya kila ambaye anamuhisi  hakutoa kura anamuharibia kwa wananchi tena kwa kuwagombanisha na kisha kuibua migogoro ambayo haina ukweli ndani yake .

Waliongeza kuwa mbali na kuwachukia viongozi hao wa Vijiji kama Vitano vya Kata hiyo ilihali wameshapatanishwa kama mara tatu lakini pia diwani huyo amelkuwa na tabia ya kugomea miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Kata hiyo hali ambayo  nayo inachangia sana Umaskini kwa vijiji hivyo.

Wakitaja baadhi ya Miradi ambayo diwani huyo amemwaga Sumu na kusababisha madhara makubwa kwa jamii  ni Pamoja na Mradi wa  mbuzi wa maziwa kutoka katika kijiji cha Nshupu ambao ulitolewa na TASAF ambapo mradi huo ulitekelezwa  na kikundi kimoja  lakini bado diwani huyo aliukata na hivyo kusababisha madhara makubwa  kwa wakazi wa eneo hilo.


Walisema kuwa mbali na eneo hilo la Nshupu lakini pia kwa maeneo kama vile Nkoaranga alisababisha  mwenyekiti wa Kijiji kufungiwa Nje ya Ofisi na wananchi wenye hasira kali lakini baadaye ofisi ilifunguliwa chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri,huku kwa Kijiji cha Sangananu aliwashawishi wananchi kukata zahanati ambayo ilijengwa na wahisani,na kwa upande wa Kijiji cha Nkoanekoli napo aligomea vyanzo mbalimbali vya maji hali ambayo ilizua tafrani kubwa sana

Na katika Kijiji cha Njani napo Mgogoro mkubwa sana kwa sasa ni matumizi ya maji ya kuchimba kwa kutumia mashine ambapo kuna mvutano mkubwa sana lakini hali hiyo imesababisha baadhi ya kazi za kijamii nazo kusimama kwa kuwa hakuna umoja madhubuti.


Awali wenyeviti hao kutoka katika Vijiji vitano ambao wanatarajia kujiuzu endapo kama diwani huyo atajiuzulu ndani ya siku 14 ni pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nkoaranga bw Solomon Sarakikya,Mwenyekiti kijiji cha Njani bw Elishilia Ayo,mwenyekiti wa kijiji cha Sangananu Bw Sangito Mafie,na Mwenyekiti wa kijiji cha Nkoanekoli Bw Christopher Pallangyo

Katika hatua nyingine akiongea na “MALKIA WA MATUKIO”kwa njia ya simu diwani huyo anayetuhumiwa Bw Goodfrey Kishongo alisema kuwa yeye anachokijua ni kuwa wenyeviti hao wamejiunga na kuwa kitu kimoja kwa kuwa wote wana mapungufu tena makubwa sana hasa ya ulaji wa mali za kijiji

Bw Kishongo alisema kuwa bado haogopi kwa kauli ya wenyevit hao kwa kuwa wao si wananchi na wananchi ndio waliomchagua na kumpa kura hivyo kama wananchi watamkataa ndio ataweza kujiuzulu lakini kamwe hawezi kujiuzulu kisa wenyeviti  wa vijiji

“bado hawa wenyeviti hawajaongea jambo la msingi mimi ni ,muwazi tena ni mkweli huwa sina mambo ya kupindapinda  kamwe wajue kuwa suala la kuachia ngazi sio suala la matisho kama wanavyofikiri bali ni suala la wananchi wananchi wakisema hawananitaki hata sasa hivi naacha udiwani”alisema Bw Kishongo


Naye Mkurugenzi Mtendajiwa halmashauri hiyo Bw Trisias Kagenzi alisema kuwa bado hajapata taarifa kuhusiana na tamko hilo la wenyeviti hao lakini atahakikisha kuwa anakaa nao chini na kujua chanzo halisi

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMTUNUKU MWANAHABARI



Na Mwandishi wetu ,Arusha .

MKUU wa Mkoa wa Arusha amemzawadia   tuzo ya uandishi bora  wa habari za jamii na maendeleo Meru , mwandishi wa habari  Mary Mwita   wa magazeti ya Mtanzania na Rai ya  Kampuni ya New habari (2006) LTD.

Mkuu wa Mkoa huyo ametoa  tuzo hiyo ,ikiwa ni ahadi yake ,na agizo alilotoa kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kupeleka jina la Mwandishi wa habari aliyeandika habari bila kupotosha jamii katika Halmashauri hiyo ,na kuweza kumpata Mwandishi huyo .

Mkuu alitoa Tshs 500,000 ikiwa ni tuzo  na kiasi cha fedha zilizokabidhiwa kwa wadau wengine   mwaka huu waliobainika kuchangia maendeleo ya Meru.

Mkuu huyo alisema kuwa  huwezi kutaja maendeleo bila kuhusisha vyombo vya habari na waandishi wa habari ,na kuwa kila Halmashauri inatakiwa kutambua  mchango wa maendeleo ya wadau  ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari .

Akimpongeza Mwandishi  Mary Mwita ,alisema wakati umefika wa waandishi wa habari kuandika habari za kweli  bila kupotosha umma ,ikiwa ni kuwawezesha wananchi kujifunza na kupata ujuzi kupitia habari hiyo ,badala ya kuandika habari za uongo .

Mlongo alisema kuwa ni wazi kuwa kila mtu katika jamii akisimama katika nafsi yake kulingana na karama aliyopewa Maendeleo ya haraka yatafikiwa na kuwawezesha wananchi kupunguza kasi ya umaskini katika jamii .

Katika hatua nyingine alipongeza uongozi wa Halmashauri ya Meru kwa kutambua mchango wa maendeleo ya wadau  na kutaka Halmashauri nyingine kuiga mfano huo wa kutunikia zawadi wadau waliosaidia maendeleo ya Halmashauri.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Trisas Kagenzi alisema kuwa  zoezi la kuwazawadia wadau ni endelevu ,na kuwa wataendelea kutambua mchango wao kwa kuwa bila ushirikiano na wadau  wa maendeleo ,maendeleo yanaweza kuchelewa .

Kagenzi alisema kuwa Mwandishi Mary Mwita ,amekuwa akiandika habari bila kupotosha umma  kwa kujituma na kutaka waandishi wengine kuiga mfano wake.

Mwisho…………………

ASANTE SANA WADAU BADO NAWAHITAJI SANA TENA KWA SANA


TCHAAAAAAAAAAAAAOOOOOOOOOOOOOOOO

MSANII SAJUKI AANGUKA JUKWAANI MKOANI ARUSHA


MSANII SAJUKI AANGUKA JUKWAANI MKOANI ARUSHA

Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikwa na wasanii wenzake mara baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya uwanja wa Sheikh Amri katika tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wale wa filamu.
Msanii huyo akitafakari kwa kina mara baada ya kuanguka chini ya jukwaa huku wenzake wakimpa pole.
Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikiliwa na wenzake wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka alipopewa nafai ya kuwasalimia mashabiki wake
(Picha na mdau wa Fullshangwe Mahmoud Ahmad-Arusha)
………………………………………………………………………….
Mahmoud Ahmad,Arusha
 
HALI ya msanii  wa filamu nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha  mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama.
 
Tukio hilo lilitokea juzi jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika  ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid  wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
 
Mara baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh” na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.
 
Hatahivyo,wasanii hao walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika zaidi.
 
Akihojiwa na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi.
 
”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
 Hatahivyo,baadhi ya mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali ya msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia ili wapate pesa ilhali mwenzao ni mgonjwa.
 
Wakihojiwa kwa nyakati tofauti mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa kupewa muda mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali hiyo inamchosha zaidi.
 
“Hawa watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa wanaambatana na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na si kumtumia kwa kupata pesa”alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba

Monday, December 17, 2012

KATA ZA MBUGUNI NA MARORONI WILAYANI MERU ZIMEATHIRIWA VIBAYA NA MABADILIKO TABIA NCHI

KATA ZA MBUGUNI NA MARORONI WILAYANI MERU ZIMEATHIRIWA VIBAYA NA MABADILIKO TABIA NCHI

Na Queen Lema,MERU

IMEELEZWA kuwa Kata za Mbuguni na Maroroni katika wilaya ya Meru mkoani hapa imeathirika vibaya sana kutoka na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kufanya shuguli mbalimbali za kilimo na mifugo kukwama kwa muda mrefu sana

Hayo yalielezwa na afisa mifugo wa wilaya hiyo Bw Mohamed Hassan wakati akiongea katika mdahalo wa mazingira hususani tabia nchi uliondaliwa na mtandao wa asasi binafsi mkoani hapa (ANGONET)mapema jana

Bw Mohamed alisema kuwa kata hizo ambazo zipo kusini mwa wilaya hiyo ni moja ya kata ambazo zimeonekana kuwa na madhara makubwa sana ya tabia Nchi kutokana na sababu mbalimbali hali ambayo hata kwa upande mwingine imesababisha Ukame

Alisema kuwa kitu kikubwa ambacho kimesababisha maeneo hayo ya kusini mwa wilaya hiyo kukumbwa na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na mabonde pamoja na Mafuruko ambayo yanahamisha hata rutuba ya udongo tofauti na maeneo mengine ndani ya Wilaya ya Meru

Aliongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikizaa matunda mabaya sana ya ukame ambapo baadhi ya mazao yameshindwa kustawi huku baadhi ya mazao kama vile mihogo na Mtama yakistawi kwa shida hivyo kuruhusu umaskini mkubwa sana kwa kata hizo ambazo ni tegemezi ndani ya mkoa wa Arusha.

“kwa kweli hapa Meru hii hali imetuathiri sana kwa kuwa hapo awali haya maeneo yalikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuzalisha lakini sasa hawawezi kuzalisha kwa wakati hivyo ukame na umaskini ndio umekithiri sana ingawaje sisi kama sisi tuna mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa tunaokoa haya maeneo ambayo yameathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi”alisema

Awali mratibu wa mtandao wa asasi binafsi mkoani hapa Bw Peter Bayo alisema kuwa kuna ulazima mkubwa sana wa kuhakikisha kwanza jamii inakuwa na uwelewa wa kutosha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi pamoja na na uharibifu wa mazingira yanachangia sana kudidimiza uchumi wa nchi na
atajamii


Bw Bayo alisema kuwa endapo kama jamii itakuwa na uelewawa mambo hayo itakuwa ni raisi sana kuweza kuchukua tahadhari mapema sana hasa wananchi wa Vijijini tofauti na sasa ambapo asilimia kubwa ya wananchi hawana elimu ya vyanzo vya mabadiliko hayo hali ambayo inachangia sana madhara ndani ya jamii.

Mbali na hayo aliwataka nao watandeji wa Serikali kuhakikisha kuwa wanajiwekea utaratibu wa kuwa na midahalo ambayo itawahusisha wananchi na hapo wataweza kujadili masuala mbalimbali yahusiyo mabadiliko hayo tofauti na pale ambapo wananchi wanapopata fursa pindi wanapokutana na asasi binafsi

MWISHO

WANANCHI WA ARUSHA VIJIJINI WAWATAKA MAAFISA MALI ASILI KUFIKA VIJIJINI NA KUACHA TABIA YA KUKAA MIJINI

WANANCHI WA ARUSHA VIJIJINI WAWATAKA MAAFISA MALI ASILI KUFIKA VIJIJINI NA KUACHA TABIA YA KUKAA MIJINI

Na Queen Lema, ARUSHA

IMEELEZWA kuwa kutokana na baadhi ya maafisa mali asili na mazingira kushindwa kufika vijijini kumesababisha vyanzo vingi vya mazingira kuendelea kuharibiwa ovyo na wananchi huku serikali ikiwa inadai mazingira yatunzwe

Asilimia kubwa ya watendaji hawa wa mazingira hawana mwitikio wa kuja vijijini na kuangalia vyanzo mbalimbali na badala yake wanafanya kazi zao wakiwa maofisini pekee hali ambayo inasababisha kila mara kuwepo na uharibifu wa mazingira

Kauli hiyo imetolewa na Wananchi wa wilaya ya Arusha Vijijini wakati wakiongea katika mdahalo unaohusiana na mabadiliko ya Tabia za Nchi uliofanyika chini ya mtandao wa asasi binafsi hapa mkoani Arusha (ANGONET)mapema jana.

Wananchi hao walisema kuwa kila siku ndani ya vyombo vya habari wanasikia kuwa wanatakiwa kutunza na kuthamini mazingira lakini bado elimu haiwafikii jamii hali ambayo bado ni sawa na kazi bure huku vijijini kukiwa na changamoto lukuki sana za uharibifu wa mazingira.

“suala la utunzaji wa mazingira bado ni suala tete sana ndani ya halmashauri hii ya Arusha vijijini kwa kuwa wananchi hatuna elimu hata kidogo ya mazingira na maafisa maliasili wetu wanakaa tu maofisini kwenye viyoyozi huku sisi tukiwa tunaambiwa kuwa tutunza mazingira na tuhakikishe kuwa tunakwepa uharibifu sasa sisi wa vijijini mara nyingine huwa tunaharibu mazingira kwa kuwa hatuna elimu lakini kama tungekuwa tunawaona hawa maafisa maliasili na mazingira basi vijijini tungekuwa na nafasi sana ya kuweza kutunza sana mazingira’waliongeza wananchi hao.

Awali Mratibu wa Mtandao wa asasi binafsi mkoani Arusha Bw Peter Bayo alisema kuwa lengo halisi la kufanya Mdahalo huo kwa Wilaya zote za mkoa wa Arusha ni kuhakikisha kuwa wananchi hasa wa vijijini wanakuwa na uelewa halisi wa masuala ya mazingira kwani bado mabadiliko ya Tabia za nchi yanaathiri sana maendeleo ya Jamii.

Bw Bayo alisema kuwa bado kuna changamoto kubwa sana ya uharibifu wa mazingira hususani ya maeneo ya  vijijini ambapo baadhi ya Sera za mazingira na misitu hazifuatwiu na watendaji wa Serikali hali ambayo inachangia sana kukitihiuri kwa mabadiliko ya tabia za nchi.

‘suala la mazingira linaendana na uchumi sasa bado kuna uhitaji mkubwa sana wa kuhakikisha wananchi hasa wale wa vijijini wanakuwa na elimu ingawaje changamoto kubwa sana kwa sasa ni baadhi ya watendaji kushindwa kufika vijijini kutokana na uhaba wa usafiri”aliongeza Bw Bayo

Naye afisa misitu katika halmashauri ya Arusha Vijijini Bw Semu Sikawa alisema kuwa wanauhitaji mkubwa sana wa kufika Vijijini kusaidia jamii dhidi ya mabadiliko ya tabia za nchi lakini kitu kikubwa kinachowakamisha ni uhaba wa vifaa vya kazi,pamoja na uhaba wa watumishi hali ambayo inawafanya washindwe kufika vijijini

MWISHO

Friday, December 14, 2012

MKUU WA WILAYA AKERWA NA WANAOLALAMIKA OVYO JUU YA UTENDAJI WA SHUGULIZA MAZINGIRA ARUSHA

MKUU WA WILAYA AKERWA NA WANAOLALAMIKA OVYO JUU YA UTENDAJI WA SHUGULIZA MAZINGIRA ARUSHA

MKUU wa Wilaya ya Arusha bw John Mwongela amewataka wananchi wa jiji
la Arusha kuachana na tabia ya kulalamika ovyo juu ya mamlaka ya Jiji
na badala yake wahakikishe kuwa kabla ya kulalamika wanatoa mawazo
ambayo yanachangia maendeleo ya usafi wa Jiji

Bw Mongela aliyasema hayo leo katika mdahalo baina  ya  viongozi
mbalimbali wa Serikali na wadau wa mtandao wa mashirika yasiyokuwa ya
Kiserikali mkoani arusha(ANGONET)ambapo mdahalo huo ulihusiana na
masuala ya mazingira kwa mkoa wa Arusha.

Bw Mongela alisema kuwa dhana kubwa sana ndani ya Mkoa wa Arusha kwa
sasa  ni ulalalamishi na manunguniko juu ya Jiji na utendaji kazi wake
jambo ambalo linafanya hata baadhi ya watu kushindwa kuonesha ufanisi
zaidi katika masuala mbalimbali yakiwemo mazingira.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya watu ambao wanalalamika juu ya
masuala mbalimbali ya Jiji wanasahu kuwa ulalalamishi wao unatakiwa
kwenda sanjari na mawazo ambayo yatachochea vyanzo hivyo vya
ulalamishi kufa ingawaje kwa sasa hadi watendaji wa Serikali nao
wanalalamika juu ya Jiji.

‘kwa sasa kila mahali ambapo utakwenda utasikia watu wanalamika nah ii
sio kwa watu binafsi bali ni hadi kwa watendaji wa Serikali nao
wanalalamika sana sasa kama wote tutaishia kulalamika je nani atakuwa
ni mtendaji wa hayo malalamiko, mimi nadhani kuwa huu ni muda sasa wa
kufanya mabadiliko kwa kuhakikisha kuwa tunatoa mbinu za kukabiliana
na changamoto na wala sio kulalamikalamika ovyo’aliongeza bw Mongela.

Awali Afisa mali asili wa mazingira kwa jiji la Arusha Bw Njwaba
Mwajibe alisema kuwa mbali na dhana hiyo ya kulalamika juu ya utendaji
kazi wa jiji hususani kwenye suala zima la mazingira lakini bado
wananchi wana matatizo ya kutoweka mazingira kwenye hali ya usafi.

Bw Mwajibe alisema kuwa hali hiyo inasababisha sana baadhi ya mitaa
kuonekana michafu ambapo wanaotupa uchafu husingizia jiji chafu huku
magonjwa ya mlipuko nayo yakiwa yanawasonga wananchi .

‘unakuta mtu anatoka na uchafu kwake anautupa nje ya nyumba yake
halafu anadai kuwa jiji ni chafu sasa sisi jamani tutaingia ndani ya
majumba ya watu na kusafisha inabidi wananchi wa Arusha wabadilike na
wahakikishe kuwa wanakuwa wasafi kuanzia ndani ya majumba
yao’aliongeza Bw Mwajibe.

Alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa Jiji limejipanga kuhakikisha kuwa
waharibifu wa mazingira wanafikishwa katika vyombo vya dola ikiwemo
mahakama ya jiji ambayo itaanza kazi hivi karibuni hali ambayo itaweza
kuufanya mji wa Arusha kuwa safi zaidi kama yalivyo  majiji mengine.

WANANCHI WA ARUSHA VIJIJINI WAWATAKA MAAFISA MALI ASILI KUFIKA VIJIJINI NA KUACHA TABIA YA KUKAA MIJINI


WANANCHI WA ARUSHA VIJIJINI WAWATAKA MAAFISA MALI ASILI KUFIKA VIJIJINI NA KUACHA TABIA YA KUKAA MIJINI

Na Queen Lema, ARUSHA

IMEELEZWA kuwa kutokana na baadhi ya maafisa mali asili na mazingira kushindwa kufika vijijini kumesababisha vyanzo vingi vya mazingira kuendelea kuharibiwa ovyo na wananchi huku serikali ikiwa inadai mazingira yatunzwe

Asilimia kubwa ya watendaji hawa wa mazingira hawana mwitikio wa kuja vijijini na kuangalia vyanzo mbalimbali na badala yake wanafanya kazi zao wakiwa maofisini pekee hali ambayo inasababisha kila mara kuwepo na uharibifu wa mazingira

Kauli hiyo imetolewa na Wananchi wa wilaya ya Arusha Vijijini wakati wakiongea katika mdahalo unaohusiana na mabadiliko ya Tabia za Nchi uliofanyika chini ya mtandao wa asasi binafsi hapa mkoani Arusha (ANGONET)mapema jana.

Wananchi hao walisema kuwa kila siku ndani ya vyombo vya habari wanasikia kuwa wanatakiwa kutunza na kuthamini mazingira lakini bado elimu haiwafikii jamii hali ambayo bado ni sawa na kazi bure huku vijijini kukiwa na changamoto lukuki sana za uharibifu wa mazingira.

“suala la utunzaji wa mazingira bado ni suala tete sana ndani ya halmashauri hii ya Arusha vijijini kwa kuwa wananchi hatuna elimu hata kidogo ya mazingira na maafisa maliasili wetu wanakaa tu maofisini kwenye viyoyozi huku sisi tukiwa tunaambiwa kuwa tutunza mazingira na tuhakikishe kuwa tunakwepa uharibifu sasa sisi wa vijijini mara nyingine huwa tunaharibu mazingira kwa kuwa hatuna elimu lakini kama tungekuwa tunawaona hawa maafisa maliasili na mazingira basi vijijini tungekuwa na nafasi sana ya kuweza kutunza sana mazingira’waliongeza wananchi hao.

Awali Mratibu wa Mtandao wa asasi binafsi mkoani Arusha Bw Peter Bayo alisema kuwa lengo halisi la kufanya Mdahalo huo kwa Wilaya zote za mkoa wa Arusha ni kuhakikisha kuwa wananchi hasa wa vijijini wanakuwa na uelewa halisi wa masuala ya mazingira kwani bado mabadiliko ya Tabia za nchi yanaathiri sana maendeleo ya Jamii.

Bw Bayo alisema kuwa bado kuna changamoto kubwa sana ya uharibifu wa mazingira hususani ya maeneo ya  vijijini ambapo baadhi ya Sera za mazingira na misitu hazifuatwiu na watendaji wa Serikali hali ambayo inachangia sana kukitihiuri kwa mabadiliko ya tabia za nchi.

‘suala la mazingira linaendana na uchumi sasa bado kuna uhitaji mkubwa sana wa kuhakikisha wananchi hasa wale wa vijijini wanakuwa na elimu ingawaje changamoto kubwa sana kwa sasa ni baadhi ya watendaji kushindwa kufika vijijini kutokana na uhaba wa usafiri”aliongeza Bw Bayo

Naye afisa misitu katika halmashauri ya Arusha Vijijini Bw Semu Sikawa alisema kuwa wanauhitaji mkubwa sana wa kufika Vijijini kusaidia jamii dhidi ya mabadiliko ya tabia za nchi lakini kitu kikubwa kinachowakamisha ni uhaba wa vifaa vya kazi,pamoja na uhaba wa watumishi hali ambayo inawafanya washindwe kufika vijijini

MWISHO

WAZAZI WAUKATAA UONGOZI WA SHULE YA MWANDETI


Joseph Ngilisho,Arumeru.
 
WAZAZI katika shule ya msingi ya Mwandeti iliyopo wilayani Arumeru,mkoani Arusha,wameukataa uongozi wa shule hiyo pamoja na kamati yake kwa madai ya ubadhilifu wa mali za shule na kueleza kuwa hawatoshiriki shughuli za maendeleo ya shule hiyo  hadi mkuu wa shule hiyo,Elibariki Laizer aondolewe.
 
Aidha wamemtuhumu mkuu huyo washule,kwenda kinyume na taratibu za uongozi wa shule hiyo kwa kuiendesha  kama mali yake,kujimilikisha mashamba ya shule na kuingia ubia wa shambe la shule lenye ukubwa ekari 6  na wafanyabishara bila kufuata utaratibu,kuchangisha michango hovyo kwa wanafunzi ikiwemo kuwalipisha faini wanapochelewa kufika shuleni ama kutofika kabisa.
 
Wakizungumza kwenye kikao cha shule kilichofanyika shuleni hapo jana,wazazi hao wa jamii ya wafugaji wamemtaka mwalimu huyo kuondoka shuleni hapo kwani pamoja na mambo mengine, kiwango cha taaluma kwa wanafunzi kimeshuka.
 
Mmoja wa wazazi hao,Lugion Leshiloi amesema kuwa mwalimu Laizer tangu ahamishiwe kwenye shule hiyo mwaka 2007 shule hiyo ambayo ilijengwa kwa msaada wa wazazi na mashirika mbalimbali, kwa sasa imechakaa,majengo yamepasuka na kuhatarisha maisha ya wanafunzi ,milango na vioo vya madirisha vimeibwa bila kuwemo uangalizi.
 
Alisema kuwa kwa sasa hawana imani na mwalimu huyo, kwani kuendelea kuwepo shuleni hapo kutaifanya shule hiyo ifilisike zaidi huku wanafunzi wakiumia kwa michango mbalimbali ambayo mara nyingi haina hata risiti,na kwamba wengi wa wanafunzi wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kero mbalimbali za mkuu huyo wa shule na kujikuta idadi ya wanafunzi kwa sasa  ikifikia 700 kutoka wanafunzi 1000 waliokuwepo.
 
‘’shule imekufa haina uangalizi ,majengo yamepasuka kila kona ,tunachotaka ni mwalimu mkuu na kamati yake waondoke,bila hivyo hatutatoa ushirikiano na shule hii’’alisem mzazi Samwel Mseyeke ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa kijiji
 
Naye mzazi ,Jonas Klasian alimtuhumu mkuu huyo wa shule kwa kuwachangisha wanafunzi michango nya shilingi 1000 kila wiki huku wanaochelewa kufika shuleni hulipishwa shilingi 500 hadi 1000 na wale wanaoshindwa kufika kabisa shuleni kwa siku moja huwalazimu kulipa shilingi 2000 hadi 2500 huku akiwasisitiza wazazi ambao hawatoi michango ya watoto wao ,kuwaondoa watoto wao shuleni hapo.
 
Wazazi hao wamesusia taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka 2011/12 iliyoandaliwa na mkuu huyo wa shule na kusomwa katika mkutano huo wakidai kwamba imechakachuliwa na imejaa ubabaishaji kwani idadi ya fedha zilizosomwa kutumika zimepandikiziwa na wanawasiwasi hazikutumika kwa matumizi hayo yaliyotajwa.
 
Akijibu tuhuma hizo mkuu wa shule huyo,Elibariki Laizer alisema kuwa tuhuma hizo  ni majungu ya wananchi hao zenye lengo la kumchafua huku akifafanua kwamba utaratibu kuingia ubia wa mashamba ya shule upo wazi kwani walifanya hivyo kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wanafunzi wa kulima mashamba hayo muda wa masomo.
 
Akizungumzia suala la wazazi kukataa taarifa ya mapato na matumizi alisema kuwa fedha zote zilizoingia shuleni hapo zimetumika kama ipasavyo na hakukuwa na taarifa iliyopotoshwa na kwamba suala na shule kuchakaa ni wazazi ndio wameitelekeza na sio jukumu lake.
 
Mwisho.

BARAZA LA MICHEZO TANZANIA LAWATAKA WADAU WA MICHEZO KUJITOKEZA


Joseph Ngilisho,Arusha
 
BARAZA la michezo Tanzania BMT,limewataka wadau wa michezo kote nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki program inayolenga kukusanya maoni juu ya rasimu ya namna ya kuhamasisha na kuendeleza michezo shirikishi  hapa nchini .
 
Akizungumza kwenye warsha ya kukusanya maoni jijini 
Arusha,Afisa mwandamizi wa BMT ,John Chalukulu alisema kuwa lengo la kukusanya maoni kwa wadau wa michezo hapa nchini ni kuhakikisha kuwa michezo inapendwa na jamii kwani kwa kiwango kikubwa jamii imeipa kisogo.
 
Alisema kuwa kwa sasa kumekuwepo na mwamko hafifu kwa jamii kuhusu suala la michezo na kwa kubaini hilo wameamua kuanzisha midahalo katika mikoa mitano hapa nchini itakayowakutanisha wadau wa michezo ili kubaini jamii inahitaji nini kukuza michezo hapa nchini.
 
Akizungumzia hali ya kudorora kwa sekta ya michezo hapa nchi alisema kumekuwapo na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa fedha,mwamko hafifu wa kushiriki michezo,wananchi kupenda michezo ya aina moja nk,ukosefu wa viwanja vya michezo pamoja na vifaa.
 
Kwa upande wa mgeni rasmi katika warsha hiyo,Sifael Ole Ngashwa Mollel ambaye ni kaimu katibu tawala wa wilaya,alilitaka baraza hilo la michezo nchini kujikita kuhamasisha zaidi michezo mashuleni ili jamii ione umuhimu wa kutoa kipaumbele kwenye sekta hiyo.
 
Alisema kuwa, swala la michezo linapaswa kufanyika kwa umakini zaidi huku wakiwafikia walengwa ambao ni wanafunzi wa shule za msingi ,vyuo vikuu na taasisi zote ili kuwezesha kupata wataalamu katika ngazi zote na hatimaye kuwezesha elimu ya michezo kuenea ngazi zote.
 
 ‘’pelekeni walimu wa michezo mashuleni na muongeze hamasa ili jamii ianze kuona umuhimu wa kutoa kipaumbele masuala ya michezo kwa vijana na makundi mengine kwani hivi sasa michezo imezorota sana mashuleni kutokana na kutokuwa na walimu wenye uzoefu wa kutosha ambao wana uwezo wa kutoa elimu hiyo’’alisema.
 
Aliongeza kuwa, swala la michezo katika shule mbalimbali hivi sasa limekuwa likifanyika kwa kuigiza hali  ambayo imechangia kupotea kwa maana halisi ya michezo mashuleni ,hivyo baraza hilo lina changamoto kubwa kuhakikisha kuwa linajiwekea mikakati na utaratibu mzuri wa kuandaa michezo mashuleni .
 
Mollel aliongeza kuwa, umefika wakati sasa wa halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa zinashirikiana na baraza hilo kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa viwanja, katika shule mbalimbali za msingi ili kuwezesha wanafunzi kupata haki zao za msingi.
 
BMT,tayari imeshaifikia mikoa ya Zanzibar,Mwanza na Arusha ikifuatiwa na mikoa ya Songea na Dar es salaam.

Mwisho.

Monday, December 10, 2012

ASKOFU ISANGYA AITAKA JAMII KUTUMIA ZAIDI UZAZI WA MPANGO

 Na Joseph Ngilisho,MERU
 
ASKOFU mkuu wa kanisa la  International Evangelism Center lililopo kijiji cha Sakila wilayani Arumeru mkoani hapa,Elihud Issangya ameitaka jamii kuacha tabia ya kuzaliana hovyo kama kuku,badala yake ifuate mpango wa uzazi wa majira,ili kuipunguzia mzigo serikali kukabii changamoto ya ajira na baa la njaa linalolinyemelea Taifa.
 
Isangya ametoa kauli hiyo leo katika mahafali ya 60 ya wahitimu wa masomo ya thiolojia ngazi ya diploma, katika chuo cha bibilia kilichopo Sakila ,ambapo jumla ya wahitimu 87 kutoka nchi mbalimbali za Afrika walihitimu masomo ya miezi 6 na kutunukiwa vyeti.
Askofu huyo alikemea tabia iliyozoeleka kwa jamii  kuzaa bila mpango, huku 
akitofautiana na maandiko matakatifu yaliyopo  kwenye bibilia yanayosema enendeni mkazaliane muijaze dunia,na kusema kuwa kadili hali inavyokuwa maandiko hayo yanapitwa na wakati, kwani idadi kubwa ya watu imeongeza umasikini wa familia na taifa kwa ujumla ukiwemo uharibifu wa mazingira unaosababsihwa na watu.
 
‘’watu wanashindwa kufahamu maana halisi ya maandiko ya bibilia yanayosema kuwa , nendeni mkaijaze dunia badala yake jamii imejenga tabia ya kuzaliana hovyo na halimaye kushindwa kuimudu familia huku watoto wakiteseka kwa kukosa chakula na elimu’’alisema
 
Askofu Isangya ambaye ni mwanzilishi wa makanisa ya kipentekoste wilayani humo,alisema kuwa taifa kwa sasa linakabiliwa sana na changamoto ya umaskini na ajira kwa wananchi wake na hivyo akaitaka jamii kuisaidia serikali kwa kupunguza idadi kuzaliana ili iweze kumudu watu wake.
 
‘’ jamani tusipende kuilaumu sana serikali kwa suala  ya ajira ,lazima na sisi tupunguze idadi ya kuzaa watoto wengi kwani kwa  kufanya hivyo serikali itaweza kukabili masuala ya njaa ,ajira na umaskini’’alisema Askofu.
 
Aidha aliwataka wahitimu hao kuzingatia yale yote waliojifunza na kwenda kuyatangaza kote duniani,waelimishe jamii kimwili na kiroho iweze kuishi kwa amani ,hata hivyo Askofu Isangya alijivunia chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1983 kwa kuhitimisha wanafunzi zaidi ya 6000 hadi kufikia mwaka huu ambao wamesaidia sana kutangaza amani hapa nchini na nchi za nje.
 
Kwa upande wao wahitimu hao wakisoma risala yao walisema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ya kukatika katika kwa umeme mara kwa mara hali inayowafanya kutotimiza ma`lengo yao.
 
Aidha walitaja changamoto ingine inayowakabili kuwa ni pamoja na ubovu wa miundo mbinu hasa bara bara ya kutoka maji ya chai hadi sakila hali inayowafanya kutopata huaduma zao za msingi pindi wanapozihitaji.
 
Hata hivyo walitaja mafanikio waliyowanayo tangu kuanzishwa kwa chuo hicho kuwa ni pamoja na kufanikiwa kuwachimba wananchi  visima 52 vya maji kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa maji pamoja na kuwa na mpango wa kuanzisha vyuo vingine  afrika ili viweze kuhudumia jamii nzima.
 
Mwisho

UKOSEFU WA MIUNDO MBINU IMARA KWA AJILI YA WALEMAVU NDANI YA MAKANISA NA MISIKITI CHANZO CHA WALEMAVU KUSHINDWA KUHUDHURIA NYUMBA ZA IBADA



UKOSEFU WA MIUNDO MBINU IMARA KWA AJILI YA WALEMAVU  NDANI YA MAKANISA NA MISIKITI CHANZO CHA WALEMAVU KUSHINDWA KUHUDHURIA NYUMBA ZA IBADA

Na Queen Lema,Aruha

IMEELEZWA kuwa kutokana na baadhi ya taasisi mbalimbali za dini hapa nchini kushindwa kujenga majengo ambayo yanakidhi haja za walemavu kumesababisha walemavu wa viungo kusindwa kupata haki zao za msingi za kuabudu huku hali hiyo ikisababisha madhara kwa jamii

Changamoto hiyo imetolewa mjini hapa katika kanisa la St James na walemavu wa viungo mbalimbali ambao walihudhuria ibada maalumu kwa ajili yao iliyofanyika kanisani hapo mapema jana

Walemavu hao wa Viungo walisema kuwa inasikitisha kuona kuwa asilima kubwa ya makanisa pamoja na misikiti ikiwa imejengwa bila kukumbuka aina ya ulemavu wao huku wakiwa wanasisitzwa kwenda kuabudu ingawaje hakun mazingira rafiki ambayo yanaweza kuwafariji

Walisema kuwa majengo mengi ya ibada ni magorofa na baadhi ya walemavu hawana viungo kama vile miguu ambapo hali hiyo inawafanya washindwe kupanda kwenye ngazi kutoana na aina ya ulemavu wao jambo ambalo linawafanya wakose haki zao za msingi  ya kuabudu

‘tunapenda sana kuja makanisani na hata misikitini lakini tnapofikiria miundo mbinu ambayo siyo rafiki kwetu kweli tunakata tamaa ingawaje sehemu mojawapo ya kutufariji ingekuwa ni kwenye nyumba hizo za ibada sasa tunawaomba wakuu wote wa taasisi hizi wawe na tabia ya kutufikiria kwa kuhakikisha kuwa na sisi tunapewa nafasi ya kuabudu  kama ilivyo sheria ndani ya Katiba ya Nchi’waliongeza walemavu hao wa viungo.

Awali Mchungaji Kiongozi  wa kanisa hilo bw Andrew Kajembe alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa kila Taasisi ya dini inawakumbuka walemavu ingawaje  kwa sasa asilima kubwa ya taasisi za dini zimewasahau walemavu kwa hofu mbalimbali hali ambayo inawafanya waone kama wametengwa na jamii zao huku matendo ya unyanyasaji dhidi yao nayo yakiwa yanaongezeka siku hadi siku

Bw Kajembe alisema kuwa hata miundombinu ya baadhi ya makanisa bado si rafiki sana kwa walemavu hivyo basi wakuu wa makanisa wanatakiwa kuhkikish wakati wanafikiria kujenga pia waweze kuwafikiria walemavu  ambao wamesahulika ingawaje ndani ya makanisa na taasisi za dini ndipo wanapoweza kupata faraja ya maisha ikiwemo dhana ya uwajibikaji kwa shuguli za kijamii zaidi.

“Sisi kama wakuu wa makanisa na misikiti bila kujali itikadi zetu tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunawasaidia hawa walemavu kwa kuimarisha majengo yetu na yawe rafiki kwa maisha yao na pia hata ndani ya ibada zetu tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunawatengea hawa walemavu siku maalumu kwaajili yao na sadaka zote ziweze kuelekezwa kwao kwani  kwa kufanya hivyo bila kujali dini zao itasadia sana kuongeza ufanisi kwao na hata maisha yao kuweza kuboreka zaidi”aliongeza bw kajembe

Wakati huo huo alisema kuwa siku hiyo ya walemavu pia ilenda sambamba na siku ya kuwafariji wagonjwa ambapo waumini wa kanisa hilo walitembelea na kuwafariji wagonjwa na majeruhi wa hospitali ya Mt Meru pamoja na watoto waliozaliwa katika hospitali ya Levolosi.

WASIOTUMIA ARDHI MERU KUNYANGANYWA NA KUPEWA WATU WENYE UHITAJI-MKUU WA WILAYA



WASIOTUMIA ARDHI MERU KUNYANGANYWA NA KUPEWA WATU WENYE UHITAJI-MKUU WA WILAYA

Na Queen Lema, Meru

WILAYA   ya Meru inatarajia kuboresha  mipango mbalimbali  ya matumizi bora ya ardhi ambapo pia itawanyanganya mashamba wamiliki wa mashamba makubwa ambao hawayatumii na badala yake mashamba hayo yatatumika kwa matumizi mbalimbali ya ardhi

Kauli hiyo imetolewa Wilayani humo na mkuu wa wilaya hiyo bw Munasa Nyirembe wakati kiongea na wananchi wa wilaya hiyo ndani ya maazimisho ya Miaka hamsini na moja ya wilaya hiyo mapema jana

Bw Munasa alisema kuwa mikakati ambayo ipo kw sasa ndani ya wilaya hiyo ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anajua vema matumizi ya ardhi bora ingawaje wapo baadhi ya wananchi na wawekezaji ambao hawatumii mashamba na badala yake kuyaacha hivyo hivyo

Alisema kuwa mpngo huo wa kuchukua ardhi ambazo hazitumiki kwa muda mrefu utaweza kusaidia sana kuraisisha maendeleo ya wilaya hiyo kwani bado wapo watu wengi sana ambao wanakabiliw na uhaba wa ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali huku matumizi hayo ya ardhi bora yakiwa ni moja ya vichocheo vya uchumi wa Nchi

“pamoja na kuwa tuna mikakati ya aina mbalimbali ya kuhakikisha kuwa tuna kuwa na matumizi bora ya ardhi lakini pia hii itasadia sana kwa kuhaikisha wale ambao wana nunua ardhi kwa muda mrefu bila kutumia wataweza kutumia tena kwa njia ambayo itaweza kukuza na kuimarisha uchumi waWilaya kwa kuwa wengine wananunua ardhi na kuacha huku wenzao wakikosa ardhi  kwa ajili ya matumizi mbalimbali’aliongeza Bw Munasa.

Pia alisema kuwa mkakati mwingine ambao utaweza kuboresha wilaya hiyo hasa katika masuala ya uchumi ni pamoja na suala zima la upimaji wa ardhi ambao utaenda sanjari na suala zima la utoaji wa hati miliki tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa hakuna suala la hati miliki za viwanja

“kwa kipindi kirefu sana wananchi wameteseka hata kwa kunyimwa mikopo ndani ya taasisi mbalimbali za fedha lakini kama watapata haki miliki basi wataweza kuzitumia kwa ajili ya mikopo hivyo tunaamini kabisa hili suala litaweza kuongeza ufanisi wa kiuchumi ndani ya vijiji vyetu na hata wilaya yetu kwa ujumla’alisem Munasa

Katika hatua nyingine alisema kuwa mbali na kuchukua viwanja ambavyo havitumiki pia wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa kwenye sekta ya Kilimo  kwa kuwa kwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la eneo linalolimwa hasa kwenye mazao ya chakula kutoka hekta 80,000hadi kufikia hekta 121,387 sawa na asilimia 51.73

Bw Munasa alisema kuwa ongezeko hilo limesababisha changamoto kama vile kilimo kisichozingatia hifadhi ya ardhi na maji,bei kubwa za pembejeo na tatizo la soko la kuaminika kutokana na bei ndogo zinazotolewa.

Alibainisha kuwa kutokana na hali hiyo Wilaya kwa sasa imeamua kutumia mbinu mbalimbali kama vile kutumia teknolojia za kisasa,kuanzisha na kuimarisha ushirika wa vyama vya kuweka na kukopa kwa ajili ya kupata mitaji na kutafuta masoko

MWISHO