HABARI NA QUEEN LEMA,Arusha
WANAWAKE wa kikristo wametakiwa kuacha tabia ya
kuwatumia marafiki kwenye ndoa zao kwani takwimu zinaonesha kuwa ndoa nyingi sana za kikristo zinakufa
kutokana na marafiki kuwa ndio vichwa badala ya Mume
Hayo yamebainishwa na Askofu Nassor Ngoy Ngoy wa
kanisa la Reboth Victory Church lilopo Maeneo ya Mianzini wakati akiongea na
waumini wa kanisa hilo katika ibada ya ndoa iliyofanyika kanisa
hapo jumapili iliyopita
Askofu huyo alisema kuwa wanawake wanapswa kujua na
kutambua kuwa hakuna kichwa cha familia bila ya mwanaume na kutokana na hali
hiyo alisema kuwa kwa sasa ndoa nyingi zinaongozwa na marafiki wa kike hali
ambayo inachangia sana
kuvunjika kwa ndoa.
Alifafanua kuwa hali hiyo ambayo ni chukizo na ndio
chanzo kikubwa sana cha kuvunjika kwa ndoa zilizo nyingi zinapswa kuachwa mara
moja na badala yake wanawake wakahakikisha kuwa wanakuwa na vifua ambavyo
vitatunza Siri,
“inasikitisha sana
kuona marafiki wanakuwa wao ndio baba na wao ndio mama kwenye ndoa wakati hata
maandiko hayasemi hivyo sasa hali hii inachangia kwa kiwango kikubwa sana baadhi ya watoto
kuteseka na wengine wanakesha wakiwa wanamtafuta shetani wakati shetani
wanamkaribisha wao wenyewe”aliongeza Askofu Ngoy Ngoy
Pia aliongeza kuwa endapo hata kama ndoa ina shida kwa
kiasi kikubwa sana basi siri ya ndoa ile anatakiwa kuijua na kutambua ni baba
mlezi ambaye ni mchungaji na wala sio Shoga kwani ataweza kukupitisha katika
mpango wa Mungu ambapo ndiko kuna
chimbuko kubwa sana la misingi ya ndoa
Aliongeza kuwa ili ndoa idumu ni lazima kila mwanandoa
hasa wanawake wawe na uwezo wa kujiwekea tabia ya siri sanjari na kutafuta
kweli ya mungu na wala sio kuongea ili kuweza kuwafuraisha marafiki walio wengi
wakati ndio msingi wa kuvunjika kwake
Aidha aliwataka wana ndoa ambao wanatofauti za kidunia
kuendelea kuwaombea wenzao kwa maombi ambayo yatasababisha imani zao za kidunia
kubalika na kuja kwenye mfumo wa kimungu kwa kuwa chanzo cha ufalme wa mungu
pia kinaanzia kwenye ndoa
“ndani ya ndoa unaweza kukuta mtu mmoja ameokoka
lakini kwa kuwa mwenzako wako bado hajamjua Mungu kila mara unamdharau na
kumuona hafai au unakuta hata wengine wanadiriki kuwakimbia na kutaka wapate
wake au wanaume waliokoka sasa hii siyo suluhisho la ndoa ambazo ni imara bali
ndoa imara ni ile inayomjua na kumtafakari zaidi Mungu”aliongeza Askofu Ngoy Ngoy.
MWISHO
No comments:
Post a Comment