IMEBAINIKA kuwa asilimia kubwa ya wakristo wanashindwa
kufikia malengo yao mbalimbali kwa kuwa wameweka
mawazo yao zaidi kwenye vitu vya kidunia kuliko
kwa Mungu hali ambayo inachangia kwa
kiwango kikubwa sana
Umaskini wa leo
Hayo yameelezwa na Mchungaji Japhet Nanyaro wa kanisa la
T.A.G Patmo Nkoanekoli wilayani
Meru mkoani hapa wakati akiongea na
waumini wa kanisa hilo
wiki iliyopita
Alisema kuwa asilimia kubwa ya watu wanawaza sana fedha na utajiri wa dunia kuliko kuwaza na kutafakari
utukufu wa Mungu hali ambayo inachangia sana kushindwa
kusonga mbele zaidi katika matarajio yao
mbalimbali
Aliongeza kuwa zipo hasara ambazo zinachangia kwa kiwango
kikubwa sana
ambazo zinatokana na kutafakari maisha ya kimwili kuliko maisha yale ya kiroho
ambayo ndiyo yanayodumu zaidi hata baada ya maisha ya hapa duniani.
“ndani ya maisha ya leo unakuta kila mtu anatafakari jinsi
atakavyoweza kupokea mali
na fedha lakini hata kuchukua dakika moja na kumrudishia Mungu utukufu hamna
sasa je tunasahau kuwa ambaye ametupa nguvu zaidi ya kuwaza tunamuacha wakati
yeye ndiye muamuzi wa kila kitu ni vema sasa tukabadilika”alisema Mchungaji
Nanyaro.
Awali alisema kuwa ni vema kama mawazo ya watu wa sasa wakabadilisha
mtizamo wao na kumrudia mungu kwani hata hali ambazo zinawakabili watu wengi
kwa sasa kama vile Umaskini zinachangiwa
sana na kutafakari maisha ya kimwili
kuliko yale ya Kiroho
Pia alisema kuwa ukiwa unataka utajiri wa kudumu hapa
duniani ni lazima kwanza umtumike Mungu kwa moyo wako wote ili uweze
kuzidishiwa yale yote ambayo unayataka ambapo ndio kusudio la mungu kumbariki
yeyote yule ambaye analenga kumtegemea katika maisha yake yote ya hapa duniani
“Maandiko yanasema kuwa tunapswa kujua na kutambua kuwa
tunatakiwa kusumbukia kwanza ufalme wa Mungu ili mengine yote tuweze
kuzidishiwa na unapomsumbukia Mungu unapata hata kwa njia ambazo hauzijui sasa
kwa nini usumbukie maisha yako wakati Mungu anaweza kukusumbukia kwa moyo wake
wote”aliongeza Mchungaji Nanyaro
MWISHO
No comments:
Post a Comment