Friday, July 20, 2012

MAKANISA,OMBENI TOBA ILI MPATE UPAKO


,ARUSHA
 
IMEELEZWA kuwa mipango pamoja na mikakati mbalimbali ndani ya makanisa inashindwa kufikiwa kwa uraisi zaidi kwa kuwa baadhi ya wadau wa kanisa hawana tabia ya kufanya toba ya kweli
 
Hayo yamebainishwa na mchungaji Mariamu Mbisse wakati alipokuwa akifundisha neno la Mungu katika kanisa la FPCT Sombetini mkoani hapa Juma lilopita
 
Mchungaji Mbise alisema kuwa asilimia kubwa ya watu wanajijengea tabia ya kusahau sana Toba hali ambayo inafanya kanisa la leo lishindwe kufikia malengo na mikakati yake mbalimbali ambayo wamejiwekea
 
Alifafanua kuwa hali hiyo ndiyo inayochangia sana hata baadhi ya watu kushindwa kufanikiwa kwa uraisi sana hali ambayo inafanya baadhi ya watu kuona kama makanisa hayana upako wa kweli
 
Alisema kuwa ni vema kama kila mkristo akahakikisha kuwa anaishi maisha ya Toba na kila mara kutafuta Toba ili aweze kufungua hata milango ya baraka kutoka kwa mungu kwani Dhambi nazo ni kikwazo cha kutopata mafanikio
 
“kwa sasa kuna mambo mengi sana huku duniani kwa maana hiyo kila mara ni vema kama watu wakajitokeza kwa wingi na kuweza kuomba kwa pamoja maombi ya toba ambayo ndiyo yanayofungua lakini kama kanisa kama kanisa litaomba juu ya toba basi hata upako utaweza kushuka”alisema Mchungaji Mariam
 
Awali mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Bi Elinaisha Abraham alisema kuwa  ili upate mafanikio ya aina yoyote ile hapa duniani ni lazima uombe na utubu kwa toba ya kweli kwa kuwa kwa Mungu kuna misamaha
 
Mchungaji Elinaisha alibainisha kuwa ni vema kama kila kanisa likahakikisha linakuwa na utaratibu wa toba ili makanisa hayo yaweze kufikia hata hatua mbalimbali ambazo wamejiwekea.
 
mwisho

No comments:

Post a Comment