Na gadness, Arusha
IMEELEZWA kuwa tabia ya wazazi kuwaachia watoto uhuru wa
utandawazi hasa simu za mikononi kwa muda mrefu ndio chanzo kikubwa cha
mdonodko wa elimu kwa nchi ya Tanzania
kwani kwa sasa wapo baadhi ya wanafunzi ambao wanatumia muda mrefu sana kwenye utandawazi
kuliko kwenye elimu
Kwa sasa hata mitandao ya kijamii ambayo ipo inatumiwa
wakati mwingine vibaya na wanafunzi hali ambayo wazazi wanatakiwa kuchukulia
tahadhari tena kwa haraka sana.
Hayo yameelezwa na Askofu Erick Mukwenda wakati akiongea na
wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi wa darasa la saba kwenye shule ya
Maranatha iliopo jijini Arusha mapema jana katika maafali ya sita ya shule
hiyo.
Askofu huyo alisema kuwa maana halisi ya utandawazi wakati
mwingine imegeuzwa kabisa na wanafunzi na hivyo wengi wanadhubutu kuwekeza huko
kuliko kuwekeza zaidi kwenye masomo jambo ambalo ni hatari sana
Alisema kuwa ili kuikwepesha jamii na tabia hiyo ni lazima
kwanza wazazi waangalie suala hilo kwa mapana
zaidi kwani wakati mwingine watawakemea
watoto baasi wataogopa na hawatajihusisha sana
na mitandao hiyo au utandawazi
Pia aliongeza nao wazazi wanatakiwa kuhakikisha kuwa
wanaepukana na tabia ya kufikiria zaidi ada kuliko kufikiria malezi ya watoto
kwani kwa sasa walimu pekee ndio wanaoachia suala zima la malezi jambo ambalo
wakati mwingine linakuwa gumu sana
“kama tunataka maendeleo ya elimu kwa nchi ya Tanzania ni
lazima kwanza tuhakikishe kuwa tunashirikiana kwenye malezi kwani malezi ya
wanafunzi sio ada bali hata maadili hivyo basi wazazi sasa mnatakiwa
kubadilika”aliongeza Askofu huyo
Katika hatua nyingine aliwataka wazazi pia kuwapa elimu
wanafunzi juu ya matumizi ya simu za mkononi lakini pia kuachana na tabia ya
kuwapa simu pindi wanapokuwa mashuleni kwani pia jambo hilo
pia linachangia sana
wanafunzi kuwazia simu kuliko masomo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment