Wednesday, December 4, 2013

SHULE ZA SEKONDARI AMBAZO ZINA MAABARA KUPEWA HUDUMA YA INTERNET BURE



Na Queen Lema, Arusha

KAMPUNI ya Smile ya mawasiliano ya Smile imeweka mikakati ya kusaidia
shule za Serikali ambazo zina maabara kwa kutoa huduma ya
mawasiliano(internet)bure itakayowawezesha wanafunzi waweze kusoma kwa
kupitia mitandao.

Hayo yameelezwa na Deo Ndejembe ambaye ni meneja kitengo cha mauzo
katika kampuni hiyo wakati akiongea kwenye uzinduzi wa mtandao wa
smile kwa mkoa wa Arusha mapema leo.

Deo alisema kuwampango huo unalenga kuimarisha huduma za maabara
katika shule za sekondari za serikali kwani wanafunzi wakiwa na huduma
hizo wataweza kusoma na kwenda pamoja na soko la dunia ambalo
linategemea zaidi huduma za mitandao.

Alidai kuwa mpango huo utaweza kuwanufaisha zaidi shule ambazo zina
maabara pamoja na kompyuta hivyo basi hata kwa shule ambazo hazina
maabara zinatakiwa kuweka mara moja ili ziweze kunufaika na mpango huo
ambao umeshaanza

“tunataka kuona kuwa lile lengo la serikali ambalo lililenga shule
ziwe na maabara linatimia lakini pia maabara ziwe za kisasa zaidi na
ziweze kupata teknolojia ya mawasiliano bure kwani itasaidia hata
ufaulu wa masomo kama sayansi kuweza kuongezeka’alisisitiza Deo

Wakati huo huo alidai kuwa mpango huo wa kutoa huduma za Tekonlojia
umeshaanza kwa shule 10 ndani ya Jiji la Dar es saalam lakini kwa mkoa
wa Arusha shule ya Arusha School tayari imeshanufaika na mpango huo
ambao ni bure

Naye Afisa mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania
(TCRA)Innocent Mongi alidai kuwa bado mkoa wa arusha unahitaji huduma
za mawasiliano zaidi kutokana na mwingiliano wa huduma kama vile
uchumi, na utalii

Mongi alidai kuwa uwepo wa mtandao huo wa Smile kwa mkoa wa arusha pia
utachangia wafanyabiashara  wakubwa na wadogo kuweza kufanya biashra
kutoka katika masoko mbalimbali duniani .

“napenda kuwasihi wakazi wa Arusha kuhakikisha kuwa wanatumia vema
mtandao huo ili kuraisisha shuguli mbalimbali za maendeleo kwa mkoa wa
arusha na kutokana na hili tunaamini kuwa Arusha itapata mabadiliko
makubwa”alisema Mongi

No comments:

Post a Comment