KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mtume mmoja wa jijini
Arusha amesema kuwa kwa sasa zipo huduma kubwa za watumishi mashuhuri Tanzania ambao wanajihusisha na Nguvu za giza huku wakiwa
wanatangaza Injili
Mtume huyo ambaye anatokea katika kanisa la Yesu ni bwana na
mwokozi wa mataifa yote Bw Herbon Kisamo aliyasema hayo jana wakati akiongea na
“UPAKO WA HABARI”mapema wiki hii jijini Arusha
Mtume huyo allisema kuwa Wamilikiu hao wa makanisa na wakuu
wa huduma ambao wapo wengi sana na huku wengine wakiwa ni watu mashuhuri sana
hapa nchini wanajiingiza kwenye ufalme wa Ki Freemasons ili waweze kupata fedha
na waumini wengi sana
Aliongeza kuwa mpaka sasa ana ushaidi dhidi ya watumishi wa
mungu wakubwa ambao wapo Kuzimu lakini wanaongoza ibada na kutoa ushuhuda wa
uongo na bila kujua na kutambua kuwa wana mkasirisha sana Mungu
“hawa watumishi ambao wengine wanaonekana kama ni watumishi
wa ukweli wanajiambatanisha na nguvu za giza
na kisha wanatoa damu zao ili waweze kupata fedha na hata kwenye mitandao ya ki
freemasons wanaonekana je hii ndio kazi ya Mungu kweli”alihoji Mtume huyo
Mbali na hayo aliongeza kuwa Mungu amempa ufunuo wa kuwasema
hadharani wale wote ambao wanatumika kuzimu lakini wanashika biblia ya Mungu
huku wakidai kuwa wanampenda na hatimaye wanawapeleka waumini wao kuzimu bila
ya wao kujua
Alifafanua kuwa hapo awali alishawai kusema lakini Majeshi
ya Kishetani ambayo yanaongozwa na watumishi hao yakaibuka lakini kwa kuwa
ametumwa na Mungu hakuogopa hali kabisa
Alibainisha kuwa nao wakristo wanatakiwa kuhakikisha kuwa
kila mara wanajilinda na kuomba sana Uweza wa
Mungu uweze kuwatala kwa kuwa wengi wamekufa macho ya rohoni na ndio chanzo cha
kupelekwa kwenye utawala mwingine wa giza
Aliongeza kuwa mbali na ,kuwa na macho ya rohoni pia
wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kuwachunguza zaidi viongozi
wao kwa njia ya roho mtakatifu na pia kujua kweli ya Mungu
“wapo baadhi ya wakristo ambao kila mara wanakimbilia zaidi
muujiza bila kujiuliza muujiza huo umetoka wapi na sasa hawa ambao wanakimbilia zaidi muujiza ndio hawana
ambao wanatekwa na mambo kama haya”aliongeza
Mtume Hebron
No comments:
Post a Comment