WAKUFUNZI wa Sensa ya
watu na makazi pamoja na wadau mbalimbali ambao watahusika katika zoezi la
kuhesabu watu kwa mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia mbinu za
kisasa zaidi ili kuwezesha zoezi hilo kufanikiwa kwa uraisi kwani kama
halitafanikiwa litasababishia Serikali hasara kubwa sana.
Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo
mapema jana wakati akifungua mkutano wa Wakufunzi wa Sensa kwa Mkoa wa Arusha
Bw Mulongo alisema kuwa endapo kama watalaamu hao watatumia
utaalamu wao vizuri kutokana na mafunzo ambayo wameyapata basi wataweza kuokoa
Serikali dhidi ya hasara mbalimbali ambazo zinaweza kutokea hasa pale zoezi hilo litakapokwama.
Alifafanua kuwa zoezi hilo lina umuhimu mkubwa sana na kwa
hali hiyo ni vema kama watendaji wakuu wakawa makini kwa kuhakikisha kuwa
wanakabiliana na Vikwazo ambavyo vinaweza kutokea wakati wa zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi
linaloanza hivi karibuni.
“kama zoezi hili litakwama ni hasara kubwa sana kwa Serikali
na hata kwa maendeleo ya jamii sasa nawasihi sana ninyi wadau hakikisheni kuwa
mnakuwa makini na kama mdau hanaona kuwa atakuwa moja ya kikwazo cha Sensa ni
bora akasema mapema na ajitoe kuliko kuwa chanzo cha kushindwa kufikia
malengo”aliongeza Bw Mulongo
Pia alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa
wanachangia maendelo ya nchi hasa kwenye zoezi hilo la Sensa kwani Serikali inapojua idadi ya
watu wake inaweza kuraisisha shuguli mbalimbali za maendeleo ya Kijamii.
Awali Mratibu wa zoezi la Sensa kwa Mkoa wa Arusha Bi Magret
Mutaleba alisema kuwa mpaka sasa maandalizi ya muhimu kwa ajili ya shuguli hizo
za Sensa kwa Mkoa wa Arusha zimeshakamilika ambapo pia wanaendelea kutoa elimu
kwa wahusika mbalimbali wa zoezi hilo ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni.
Bi Magret aliongeza kuwa kwa sasa Wakufunzi 158 wanapata
elimu juu ya kukabiliana na zoezi
hilo ndani ya Mkoa wa Arusha ambapo wanatokea katika Halmashauri zote za jiji
la Arusha na watapata mafunzo hayo kwa siku 12 huku lengo likiwa ni kuboresha
zoezi hilo
“hawa Wakufunzi 158 ambao leo wamepewa mafunzo ni kwa ajili
ya kuweza kuwapa na wengineo mafunzo ambapo na
wao watawapa watu kama vile makarani ambao nao watahusika katika zoezi
hilo la Sensa na tunaamini kuwa kwa kutumian njia hii ya mafunzo basi
itachangia sana kuraisisha zoezi hilo kwa uraisi zaidi”aliongeza Bi Magret
MWISHO
No comments:
Post a Comment