MATUKIO YA UKUSANYAJI MAONI YA KATIBA MPYA MKOA KUSINI UNGUJA.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ukusanyaji wa Maoni ya Katiba mpya Mohd Yussuf
Mshamba akitoa Ufafanuzi wa namna ya Utoaji wa maoni unavyotakiwa huko
katika kijiji cha Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni siku ya Pili
tokea kuanza kwa mchakato huo huko Zanzibar kushoto yake ni Mjumbe wa
Kamati Salim Ahmed Salim na kulia yake ni Mjumbe wa kamati Richard
Lyimo.
Mjumbe wa Kamati ya Ukusanyaji wa Maoni ya Katiba mpya Richard Lyimo
akifahamisha nmna ya mchakato mzima wa kukusanya na kutoa maoni kwa
wananchi unavyotakiwa huko katika Kijiji cha Kibuteni Mkoa wa Kusini
Unguja kushoto yake ni Mwenyekiti wa Kamati hio Mohd Yussuf Mshamba.
Mwananchi wa Kijiji cha Kibuteni Riziki Wakili Haji akipeleka maoni yake
kwa njia ya Barua mbele ya kamati ya ukusanyaji maoni huko katika
kijiji hicho Mkoa wa Kusini Unguja.
No comments:
Post a Comment