MRADI wa ujenzi dampo la kisasa wenye thamani ya
shilingi bilioni 3 unofadhiliwa na benki ya dunia katika jiji la Arusha, upo
hatari kuyeyuka kufuatia wananchi wa kata ya Muriet manispaa ya Arusha
kugoma kupisha eneo la mradi huo licha ya kulipwa stahili zao .
Aidha mradi huo ambao ulikuwa uanze tangu april mwaka
jana umeshindwa kuendelea kutokana na mvutano mkali ulipo kati ya wananchi
zaidi ya 200 na manispaa ya jiji la Arusha ,ambapo wananchi hao wameilalamikia
manispaa hiyo kwa kushindwa kuwalipa fidia ya maeneo yao waliyoyaendeleza ,huku manispaa hiyo
ikidai imeshawalipa.
Akizungumzia swala hilo
, Mkurugenzi wa manispaa ya Arusha, Bw Estomih Changa’h alikiri wananchi hao
kuwa kikwazo cha kuanza kwa mradi huo huku akidai kuwa wafadhili wa mradi huo
ambao tayari walionyesha nia na kuja na kupima katika eneo hilo wameanza kukata tamaa.
Alifafanua kuwa , baada ya kufanya tathmini ya awali
mwaka jana walibaini kuwa wananchi 42 ndio waliopo ndani ya eneo
husika la mradi ,hivyo manispaa ya Arusha ilifanya tathimin na kukubali
kuwalipa kiasi cha shilingi milioni 252 kama fidia ya makazi yao.
‘’tulipofanya tathimini ya makazi yao
tulikubaliana kuwalipa wakazi hao 42,na kila mtu alipigwa picha akiwa amesimama
mbele ya eneo ama nyumba yake,sasa tunasikitika sana kuona wakiendelea kunga’ng’ania huku
kundi lingine la watu zaidi ya 200 wakiibuka kutaka nao walipwe fidia’’alisema
Bw Chang’ah
Alisisitiza kuwa,tayari manispaa imeshawalipa wananchi
33 kati ya 42 kwa kiwango tofauti na kubaki wananchi tisa tu ambao walikuja
kurubuniwa na kugomea malipo hayo.
Aliongeza kuwa, wananchi hao wamekuwa wakifika katika
ofisi ya manispaa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha kudai fidia zao ambapo
wamekuwa wakijaribu kuwaelewesha na uendesha vikao kadhaa, lakini wamekuwa
wagumu kuelewa .
Mwenyekiti wa kamati ya waathirika hao ,Jackson
Japhet alisema kuwa, wao wanachotaka ni kutaka kulipwa fidia stahili ya makazi
yao kwani wengi wa wananchi wamekuwa wakiishi hapo muda mrefu na wamekuwa
na makazi ya kudumu ,hivyo ni ngumu sana wao kuondoka katika eneo hilo.
Wakizungumza katika kikao cha hadhara katika eneo hilo la Muriet mwishoni
mwa wiki, wameazimia kwenda mahakamani kusimamisha uanzishaji wa mradi huo
hadi manispaa hiyo itakapofanya tathimini upya kwa kuwashirikisha
wananchi hao na kuwalipa fidia stahili bila kuwapunja.
Mwisho
SERIKALI imesema
kuwa ipo kwenye mchakato wa kuviboresha viwanja mbalimbali vya ndege hapa
nchini ukiwemo uwanja wa ndege wa Arusha kwa kuufanyia matengenezo makubwa
uweze kuruhusu kutua kwa ndege kubwa za kimataifa.
Waziri wa uchukuzi
,dkt Harisson Mwakyembe aliyesema hayo jana baada ya kupokea taarifa fupi
wakati akiongea na wafanyakazi wa kiwanja cha ndege cha Arusha baada ya kufanya
ziara fupi mkoani hapa.
Dkt Mwakyembe
alisema kuwa uwanja wa ndege wa Arusha unaumuhimu wa kipekee katika kuendeleza
utalii wa ndani na kueleza kuwa serikali itafanya kila njia kuhakikisha kuwa
uwanja huo unapanuliwa na kuwa na uwezo wa kutua ndege kubwa.
Alisema amekuwa
akipata malalamiko mengi kuwa uwanja huo umekuwa ukitumika kunyangánya wateja
wa uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) huku maombi hayo yakitaka uwanja huo
ufungwe.
‘’nimepata taarifa
za kutaka kufungwa kwa uwanja huu wa ndege wa Arusha kwa kuwa unatumika
kunyangánya abilia wa uwanja wa KIA ,nimejiridhisha kuwa kiwanja hiki kina
umuhumu wa kipekee na serikali itaangalia uwezekano wa kukiboresha’’alisema
Mwakyembe.
Alisema serikali
itatenga fedha zaidi kwa ajili ya kukiboresha kiwanja hicho ili kiwe cha
kisasa zaidi ,ikiwa ni pamoja na kuviboresha viwanja vingine vya Songwe,Kigoma
na Mwanza.
Awali Kaimu
mkurugenzi wa kiwanja cha ndege cha Arusha,Mhandisi Suleiman Suleiman alisema
kuwa kiwanja hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa eneo la
maegesho ya ndege, jengo la abilia na jengo la zima moto.
Alisema changamoto
zingine ni pamoja na kutokuwa na taa zinazowaka majira ya usiku hivyo
kutoruhusu ndege kutua ama kuruka nyakati za usiku,kituo cha umeme ,Mnara wa
kuongozea ndege ,Jengo la hali ya hewa ,jengo la Mizigo pamoja na
miundombinu yake.
Aidha alisema kuwa
ukarabati wa kiwango cha lami wa barabara ya kuruka na kutua yenye urefu wa
mita 420 uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7umefanya urefu wa
barabara hiyo kufikia mita 1620 hivyo kuwezesha ndege zenye ukubwa wa
kubeba abilia 70 kuweza kutua katika kiwanja hicho.
Mhandisi Sulemeni
aliongeza kuwa kwa sasa kiwanja hicho kinahudumia wastani ndege 1700 kwa
mwaka na abilia wanaohudumia kwa mwezi ni 12,000.
Alisema kuwa
mpango wa sasa ni kuhamisha barabara ya Arusha Babati na tayari wamemweleza
wakala wa barabara mkoani Arusha(Tanroads).
Aliongeza kuwa
hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano uliopo sasa, pamoja na kuhamisha
barabara ya sasa ya kuingia kiwanjani hapo kwani inaingiliana na maegesho.
No comments:
Post a Comment