Na Queen Lema, ARUSHA
Askofu wa kanisa la KKKT dayosisi ya kaskazini Kati,Dkt
Thomas Laizer ameyataka makanisa kujiwekea utaraibu wa kufanya maombi kila mara
kwa kuwa sasataifa linapoteza rasilimali watu kutokana na migomo ambayo
inaendelea kila mahala.
Dkt Laizer aliyasema hayo wakati wa ibada ya kuweka wakfu
gari la kanisa la KKKT usharika wa Kimandolu mapema jumapili iliyopita jijini
hapa.
Askofu huyo alifafanua kuwa kwa sasa Taifa la Tanzania lina ingia kwenye migogoro ya aina
mbalimbali hali ambayo kama kanisa haitaliangalia kwa undani sana basi itaweza kupoteza mambo mengi
Alifafanua kuwa ni vema kuhakikisha kuwa kila mara maombi
yanafanyika na kuliombea taifa kwa kuwa hiyo ni kazi mojawapo ya kanisa la leo
na kanisa kama kanisa linanguvu kubwa sana ya
kuweza kutetea jambo hilo
“leo madaktari wameingia kwenye migogoro na wamegoma lakini
ukiangalia suala zima la vifo hasa kwa wanawake na watoto nalo linaongezeka
sana sasa hali hii ni mbaya sana na kama hatutaomba rehema za Mungu juu ya nchi
yetu basi hata kesho utasikia wengine nao wamegoma ingawaje kwa madaktari
wanachokidai ni halali kabisa”alifafanua Dkt Laizer
Alisema kuwa ingawaje madaktari hao wana haki ya kugoma lakini wanatakiwa
kuhakikisha kuwa wanakumbuka kuwa na huruma ya Mungu kwa kuwa wanaokufa hawana
hatia bali yenye hatia ni Serkali na kwa hali hiyo wanatakiwa hata kukumbuka
amri za Mungu ambazo zinadai na kusema kuwa watu wanatakiwa kupendana.
Awali dkt Laizer aliongeza kuwa endapo kama kanisa litafanya
maombi mbalimbali kwa taifa pia linatakiwa kuomba juu ya haki kwa kuwa kwa sasa
kuna baadhi ya maeneo ambayo hayatoi haki kwa watanzania hali ambayo ndiyo
chanzo kikubwa sana
cha Rushwa.
“kwa sasa hivi rushwa imejaa kila mahali watu wananyimwa
haki zao za msingi na hili limejitokeza hata kwenye uchaguzi wa EAC ambapo
kulikuwa na rushwa nje nje na vyombo vy a usalama vilikuwa pale lakini
hawaliangalia hilo na sisi kama tutaruhusu hilo ni wazi kuwa hata jamii zitakosa
haki zao za msingi”aliongeza Dkt Laizer.
Katika hatua nyingine mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Bw Solomon Masangwa alisema kuwa mchakato wa kununua
gari hilo ulianza toka miezi michache iliyopita
kutokana na uitaji uliokuwepo
Bw Solomon alifafanua kuwa uitaji huo ulisababisha washarika
waweze kuchanga zaidi ya Milioni 40 ili waweze kununua gari hilo ambalo wamenunua kwa ajili ya shuguli
mbalimbali za kueneza injili.
Alizitaka sharika nyingine kuiga mfano kama huo ambapo
waumini kama waumini wana uwezo mkubwa sana
wa kununua vifaa maalumu kwa ajili ya kuendesha injili na kuacha kuwategema
zaidi wafadhili.
No comments:
Post a Comment